@spana_Konki@Big0047 MDAU KUTOKA DM
“Mnaweza dhani binti ndio aliachwa kumbe binti ndio alimuacha mwana, yule binti kwa namna ambavyo huwa anajadili na conversation zake Twitter unaweza sema nimMarxist sana na self conscious hajafungwa na dini wala social constructs ambazo zinatuguide wengi.”
Mwili wa Mwl, Thadei Ole Mushi uliagwa Kanisa Katoliki Parokia ya Muhimbili DSM. Ukasafirishwa hadi KIA. Ukafika saa 1:30 usiku. Leo utazikwa Chombo, Kitandu Shinga, Uru Kusini, Moshi Vijijini
Lakini maeneo yote mawili, mwili wa Mwl, Thadei Ole Mushi haujafunuliwa ili kuruhusu waombolezaji kumuaga kwa kumtazama. Hakuna sababu za msingi zilizotolewa. Ni maelekezo ya wahusika.
Ukifika msibani, unaelekezwa sehemu ya kwenda kuaga jeneza kwa kutazama picha ya Thadei Ole Mushi na jeneza ambalo limefunikwa bendera ya CCM. Hakuna kufungua jeneza kuutazama mwili.
Mwalimu Thadei, waombolezaji wanalizwa sana, hawawezi kukuaga mtoto wao. Wakiuliza kwanini tunazuiwa kumchungulia mtoto wetu wanaelezwa “tusameheni hilo kwa kweli, lipo nje ya uwezo wetu”.
Mwalimu Thadei. Msiba wako umetekwa nyara na CCM wenzako. Leo jeneza lako limefunikwa bendera ya CCM wakati ukiugua kwa kuwekewa sumu, hawakutaka hata kukusogelea. Walikukataa.
Leo nyumbani kwako, Chombo, Kitandu Shinga, Uru Kusini, Moshi Vijijini, viongozi wote wa CCM ngazi ya mkoa na wilaya wapo. Kijiji chako kimeshuhudia gari aina zote za halmashauri. Hadi gari ya zimamoto.
Mwajiri wako, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Hai, amemwaga pongezi kwenye mkeka, umesambaa kweli. Lakini sidhani kama halmashauri ya wilaya ya Hai ilihusika katika matibabu yako.
Pumzika kwa amani Mwalimu Thadei. Ulikuwa muungwana. Sawa na binadamu wengine ulikuwa na utimilifu wa ubinadamu (mapungufu). Tulitofautiana sana lakini bado ulibaki kuwa muungwana.
MMM, Martin Maranja Masese
Rais @SuluhuSamia umesafiri kutoka Zanzibar hadi Mwanza kukabidhi boti na vizimba kwa kugawa vyeti kwa wawakilishi wa wawanufaika? Hii kazi angeliweza kuifanya mkuu wa mkoa au waziri wa uvuvi. Umesafiri na mawaziri. Matumizi mabaya ya fedha zetu. Serikali za majimbo ni muhimu.
Waziri kutoka serikali Tanzania kanunua nyumba mbili za kifahari South Africa,Johannesburg mitaa ya Green Hill
Baada ya siku 7 mbele anafanya transactions kupitia ndugu yake ananunua nyumba nyingine Marekani
Wao wanakimbiza pesa nje ya nchi ila midomoni mwao wanaita wawaekezaji
Mwanaharakati @mdudechadematz AMEKAMATWA na @UhamiajiTz katika mpaka wa NAMANGA alipokuwa akielekea KENYA, Kwa madai eti ana “KESI YA UHAINI”. Kwa sasa anashikiliwa katika kituo cha Polisi NAMANGA. Kwa kuwa MDUDE siyo MKIMBIZI, natoa wito, AACHIWE HARAKA.
Martin Luther King aliwahi kusema ‘Our lives begin to end the day we become silent about things that matter’; akimaanisha mwisho wa maisha yetu (kama jamii, nchi n.k) huanza pale ambapo tunakalia kimya mambo yale ya msingi. Kukaa kimya ni dhambi kubwa katika uonevu, ni dhambi pia wakati ambao jamii inahitaji watu wake kupaza sauti ili mabadiliko ya lazima yafanyike.
Ushiriki wetu kwenye maandamano ya amani, kutoa maoni, kusimama kwenye ukweli ni njia ya pekee ya kuhakikisha tunaikwepa dhambi hii na muhimu zaidi ni hatua muhimu katika kuandika historia mpya na bora ya nchi yetu.
Chini ya katiba ya sasa, Tanzania yetu itaendelea kuwa mikononi mwa watawala na madalali wa siasa. Bila kuwepo kwa katiba mpya na mageuzi makubwa kwenye sheria na mchakato mzima wa uchaguzi Tanzania itaendelea kutawaliwa na viongozi waiba kura, wasio na vigezo wala uchungu na nchi yetu.
Tunaipambania Tanzania ya sasa kuifanya bora na yenye mifumo thabiti kwa ajili ya kizazi hiki na vizazi vijavya. Muda wa mabadiliko umewadia, Mtanzania mwenzangu usiendelee kukaa kimya kwa ukimya wako ni kukata tiketi ya kuimaliza nchi yetu.
Paza sauti kizalendo, tulete mabadiliko kwa pamoja.
Tangu saa saa 08:20 asubuhi nimezuiliwa na @UhamiajiTz katika mpaka wa Namanga katika safari yangu ya kwenda Kenya kwa kile wanachodai kuwa mimi nimezuiliwa kutoka nje ya nchi na serikali ya Tanzania.Hata nilipohoji sababu za kuzuiliwa wanadai wao wamepata tu maelekezo kutoka juu