In response to the election protests between 29 October and 3 November 2025 in #Tanzania, security forces used unnecessary or disproportionate force showing a shocking disregard for the right to life and to the freedom of peaceful assembly.
https://t.co/45QJBEcIqm
KENYA.
Kenya Affordable Housing Project (AHP); Mkuru Project. Small studio apartments (bedsitters) inagharimu kiasi cha KSh 640,000 (hii ni sawa na TZS 12,353,416)
Wanunuzi wanalipa kwa miaka 30, na malipo ya kila mwezi ya KSh 3,896. Hii inahusisha usalama, usafi na ukusanyaji wa takataka. Ziada ni maji na umeme wao.
Serikali itatoa ruzuku itakayoshughulikia amana ya 10%. Familia hazihitaji kutunza kiasi kikubwa cha pesa ili kuanza mchakato wa kulipa deni la kununua nyumba.
TANZANIA.
Nyumba za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Magomeni Kota. Chumba kimoja ni Tsh48,522,913 na nyumba ya vyumba viwili inauzwa Tsh56,893,455.
Miaka mitano ya kukaa bure na baada ya hapo nyumba hiyo utairejesha kwa Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) na kuingia mkataba wa malipo kwa miaka 15.
Hakuna ruzuku ya Serikali katika ununuzi wa nyumba. Kwa hiyo, kila mkazi analipa kiasi cha Tsh300,000 kwa mwezi kwa mwaka atalipa kiasi cha Tsh3.6 milioni
NB; mbogamboga, hoja ya msingi hapa ni ‘Affordable Housing Project’. Miradi ya TBA hailengi kumsaidia mwananchi wa hali ya chini. Ni miradi ya wadosi.
Taifa ambalo redioni asubuhi hadi mchana wanajadili michezo. Mchana hadi jua linapozama wanajadili umbea. Jua likizama wanarudi kwenye michezo. Usiku wanajadili ngono hadi pakuche. Hakuna vipindi vya taaluma, ujasiriamali, kilimo, midahalo. Hilo ni TAIFA lipo kaburini kitambo.
Kenya - Affordable Housing Finance Project (AHP)
Wakati Tanzania tunapiga mafataki kusherekea sherehe za SIMBA na YANGA, majirani zetu, KENYA wamepiga mafataki kuzindua Mukuru Affordable Housing Project.
Tanzania tunatumia mijifweza ya Serikali kugharamia magoli ya SIMBA na YANGA, KENYA, wanawekeza fedha za umma kusaidia wananchi wa kipato cha chini.
Tanzania imewekeza kupambana na wananchi wanaokosoa na kukemea mauaji. Wanaonekana maadui. Serikali ya KENYA inajenga makazi kwa wananchi.
Mpango wa Serikali ya KENYA ni kujenga nyumba 230,000 za bei nafuu nchi nzima ili kuwapa Wakenya fursa ya kupata makazi bora kwa gharama rahisi.
Mradi wa Mukuru, utazisaidia familia maskini na zenye kipato cha chini kupata nyumba za kisasa kwa mfumo wa kukodisha-kwa-kumiliki (rent-to-own system).
Ambapo, watalipa malipo ya kila mwezi na kumiliki nyumba. Small studio apartments (bedsitters) inagharimu KSh 640,000 (TZS 12,353,416) kila moja.
Wanunuzi wanalipa kwa miaka 30, na malipo ya kila mwezi ya KSh 3,896. Hii inahusisha usalama, usafi na ukusanyaji wa takataka. Ziada ni maji na umeme wao.
Serikali itatoa ruzuku itakayoshughulikia amana ya 10%. Familia hazihitaji kutunza kiasi kikubwa cha pesa ili kuanza mchakato wa kulipa deni la kununua nyumba.
Mpango huo unalenga waliopo makazi duni hawahitaji kulipa amana yoyote bali wanakaa ndani ya nyumba na watalipa KSh 3,896 kwa mwezi kumiliki nyumba hizo.
Nchi nzima, katika kaunti zote 47 za Kenya, kazi ya ujenzi wa makazi nafuu kwa wananchi inaendelea katika Mpango wa Serikali wa Mageuzi wa Makazi ya bei nafuu.
fikiri kwa TZS milioni 12 ambayo utailipa kwa miaka 30 kwa malipo ya TZS 75,000/mwezi – ikiwepo na ruzuku ya Serikali unamiliki nyumba ikiwa na furnitures ndani.
Kweli, wanapata wananchi wa kawaida wamejisajili kwa kufungua akaunti ya eCitizen na kujisajili katika tovuti ya Boma Yangu (https://t.co/KVmJd3APTm) au kupiga *832#.
Ni soko la mtandaoni kwa washikadau katika Mpango wa Nyumba wa bei nafuu; homeowners, developers, financiers, and Micro, Small, and Medium Enterprises
Hii ni tofauti na ambavyo ingelikuwa Tanzania. Wangelipata wadosi na familia zao. Udalali ungelikuwa mkubwa na kama mradi upo Kariakoo, ni wahindi.
Kama miradi hiyo itafanyika kwa miaka 10 mfululizo, kwanini KENYA isiwe SINGAPORE ya EAC? Tanzania, Tulimkosea nini Mungu? Hakuna hizi fikra kabisa?
Tanzania watawala wapo katika vita ya kupambana na wanaharakati wa ndani na nje, wanawafungulia kesi wakamatwe na kutupwa gerezani maana ni kero kwao.
Badala ya kuwekeza nguvu katika mambo muhimu kama ‘Affordable Housing Program’ wanawekeza nguvu kupambana na waandamaji wanaotaka maisha bora
Unakumbuka mradi wa Dege Eco Village uliopo Kigamboni? Mradi wenye thamani ya TZS 1.3 Trilioni katika ekari 302, nyumba 3,759 umetelekezwa
Ujenzi wake ulianza 2014, hadi ujenzi unasimama 2016 unatajwa kutafuna TZS 179 Bilioni na ulikuwa ukitekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Mradi wa Dege Eco Village ulikuwa na nyumba kifahari, hoteli, baa, migahawa, maduka, shule, hospitali, kumbi za mikutano, nyumba za ibada. Umetelekezwa wote.
2025 Serikali ya CCM ikaenda bungeni na kusema imefanya tathmini na kubaini itakuwa ni hasara kuendelea na mradi huo hivyo unatakiwa kuuzwa.
William Ruto anafanya mambo ambayo CCM (wakoloni weusi) wameshindwa kufanya kwa 64 tangu nchi yetu ipate uhuru wa bendera kutoka kwa mkoloni mweupe.
@mangekimambi@POTUS@realDonaldTrump@grok translate to English and transcribe here all that Mange Kimambi has said in this video for the benefit of non-swahili speakers.
Huyu Mzee ameshapata hakimiliki ya huu ubunifu kweli?🤔🤔🤔
Kuna creativity ya hali ya juu hapa, sio bidhaa ya kuuza elfu tano tu na kuondoka.
Wenye nafasi na utaalam wamsaidie kupata umiliki wa huu ubunifu na kuuthamanisha accordingly.
Tupo kwenye taifa ambalo mtu akiongea jambo fulani kuhusu utendaji wa watawala, ambao ni wajibu wake wa kikatiba kama mwanachi, tayari ndugu na rafiki zake wanajawa hofu kuhusu usalama wake.
Yani tunaishi kwenye taifa ambalo mtu anayeuza madawa ya kulevya yupo safe kuliko anayekosoa watawala.
Kwa nini mtanzania awe na wasiwasi na usalama wake kwa kuhoji kuhusu rasilimali za taifa lake ambazo kimsingi ni mali yake??
Usenge usiokuwa na kichwa wala miguu.
UJAMBAZI WA RASILIMALI ZA TANZANIA UNAENDELEA KWA KASI.
Kwa mtakaokumbuka mtakumbuka kuwa kipindi cha kampeni niliwaambia kuwa Aiport ya KIA inaenda kuuzwa kama ilivyouzwa bandari. Kuna wapuuzi na machawa waliniona mimi mchochezi na kwamba natunga vitu ili kujenga chuki. Haya Oneni hii.
Kipindi cha kampeni wamefungua kampuni kabisa brela, inaitwa Transom Tanzania limited, hii ndio kampuni itakayopewa umiliki wa airport ya KiA. Sasa angalieni shares. Oman wamepewa share 65%, Serikali ya Tanzania imepewa 10% only, hiyo kampuni yenye 25% ni kampuni ya Abdul.
Pale KIA ndio ilipo Tanzanite yenyewe. Kwa kuwapa OMAN airport ya KIA, sasa Tanzanite zitaibiwa na kupitishwa pale airport bila shida yoyote, wanyama wataibiwa, biashara ya pembe za Tembo ndio itapamba moto, madini mengine yataibiwa hapo.
Ni hivi kwa sasa wanasubiria mambo yapoe ndio watangaze kuwa wenyewe mafisadi na wanyonyaji (OMAN) wamejipa airport ya KIA.
Watanzania amkeni…
Watanzania kukosa maji liwe ni kosa la jinai.
Dar es Salaam mahitaji yake ya maji kwa siku moja ni lita milioni 570. Uwezo wa uzalishaji wa maji kwa siku moja katika jiji la Dar es Salaam ni lita milioni 530.
Huu mgao mkubwa wa maji mkubwa unaendelea Dar es Salaam ni kwa sababu kuna upungufu wa lita milioni 270 za njia ya mitambo ya Ruvu chini kutoka Mto Ruvu.
Mradi wa maji Kimbiji, Kigamboni unachangia lita milioni 70 pekee. Hivyo, Ruvu Chini unatoa lita milioni 270 + Kigamboni lita milioni 70. Jumla ni lita milioni 340.
Lita za maji zilizobaki zinachangiwa na mitambo ya Ruvu Juu. Kigamboni ndiyo backup iliyobakia kwa sababu inaleta lita milioni 70 kutoka ardhini, siyo mtoni.
Mwaka 2006 kulifanyika utafiti wa kutambua vyanzo vya maji vinavyoweza kutumika kutoa huduma ya maji Wilaya ya Kigamboni ili kukidhi mahitaji ya watu.
Walitafiti uwezekano wa kutoa maji baharini, kutoa maji katika mtambo wa Ruvu juu au chini, na tafiti nyingine iliangalia uwezekano wa kutumia maji kutoka ardhini.
Tafiti iliitwa ‘Future Water City’ ilibainisha, matumizi ya maji yaliyopo ardhini ndio njia pekee sahihi, nafuu na yenye ufanisi itakayoweza kufikisha maji kwa wakazi.
DAWASA iliipa kazi kampuni ya Serengeti kuchimba visima 3, vya majaribio vyenye kina cha mita 600 kwenda chini kubaini eneo linalotoa maji kwa wingi.
Kupitia utafiti wa Future Water City, walibaini eneo la Kimbiji–Kigamboni lililoonekana kuwa na kiwango kikubwa cha maji chini ya ardhi (ground water).
Machi 2013, DAWASA ilisaini mkataba na kampuni ya Serengeti kuchimba visima 20 vya kuzalisha maji kwa gharama ya TZS 26 Bilioni kata ya Kimbiji na Mpera.
DAWASA ilitilia saini na M/s Advent construction Ltd kwa ajili ya ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhi maji la lita milioni 15 linalojengwa kwenye eneo la Kisarawe II,
Pamoja na kazi ya ulazaji wa bomba lenye urefu wa kilomita 5.7 kutoka kituo cha kusukuma maji hadi kwenye tanki kubwa la maji ambalo lipo Kimbiji.
Ujenzi wa tanki la maji Kimbiji, Kigamboni uligharimu kiasi cha TZS 26 bilioni. Mradi huu ukazinduliwa 11 November 2022. Ndiyo unaosambaza lita milioni 70.
Dar es Salaam yenye wakazi 5,383,728 (8.7% ya watanzania wote) kutegemea maji ya mto Ruvu ni kosa kubwa ambalo Serikali timamu ilitakiwa kufikiria.
Population growth ya Dar es salaam inazidi kasi na uwezo DAWASA katika kutafuta suluhusho la kudumu kwa mahitaji ya maji kwa wakazi wa Dar es salaam.
Mabadiliko ya tabia nchi hayatoi uhakika wa kupatikana kwa mahitaji ya maji sasa na miaka inayofuata. Mvua zinaweza kupotea kwa muda mrefu, mito itakauka.
Kama Dar es Saalam inaishi kwa mradi mmoja wa Kimbiji unaozalisha lita milioni 70, uliojengwa kwa TZS 26 bilioni? Vipi ingelikuwepo miradi 10 kama hiyo?
Kukosa vipaumbele. Uwekezaji mdogo Kigamboni visima 15 pekee vinavyotoa lita million 70 kwa siku. Vipi kama wangelikuwa na visima 200 vya kuzalisha maji?
Tanki kubwa la kuhifadhi maji la lita milioni 15. Hivyo, wanajaza tanki hilo kwa siku mara 5 ili kupata ujazo wa maji lita milioni 70, ambazo ndiyo tunapata mgao.
Ujenzi wa Jengo jipya la DAWASA umegharimu TZS 48 bilioni. Kama kipaumbele kingelikuwa ni maji kwa watu wa DSM, pesa zingejenga matanki mawili ya maji.
ATCL na TRC wamesababisha HASARA ya TZS 315.8 bilioni kwa mujibu wa taarifa ya CAG. Hii hasara ingeliweza kujenga matanki 12 kama ya Kimbiji.
Hasara jumuifu (accumulated losses) ya (ATCL) kutoka mwaka mwaka 2014/2015 hadi mwaka 2023/2024 jumla ni TZS 671.98 Bilioni iliyosababishwa na ATCL.
TZS 671.98 Bilioni unajenga matanki 25 kama hayo ya Kimbiji - Kigamboni na miaka 1,000 inayofuata huwezi kusikia Dar es Salaam kuna mgao mkubwa wa maji.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umelipa vituo vya afya huduma HEWA ya Sh14 bilioni. Unalipa huduma hewa wakati wananchi hawana visima vya maji?
Taarifa ya CAG 2021/22 (NHIF) ulipata hasara ya zaidi ya TZS 204 bilioni kwa kufanya malipo hewa na marudio ya malipo huduma kwa mtu mmoja kwa wakati mmoja.
Hizi TZS 204 bilioni ambazo ni hasara ya NHIF, zingelielekezwa kujenga matanki ya maji kama ya Kimbiji, tungefanikiwa kupata matanki 7 ya maji
Mradi wa maji Kigamboni – Kimbiji ulilenga kusambaza huduma ya maji kwa wakazi wapatao 250,000 pindi mradi huo utakapokamilika mwezi Disemba 2022.
Lakini sasa mradi huo ndiyo unalazimika kusambaza huduma ya maji kwa wakazi wapatao 5,383,728 (8.7% ya watanzania wote). Lazima mgao wa maji uwe mkali.
Mahitaji ni lita milioni 570. Maji yanayopatikana sasa ni lita milioni 70, ambayo yalitakiwa kuhudumia watu 250,000 lakini sasa yanahudumia watu milioni 5.4
Inakadiriwa kwamba, ifikapo mwaka 2050 kutakuwa na watuamiaji wa maji milioni 17 kutoka watumiaji wa maji milioni 7.4 waliopo sasa kwa Dar es Salaam pekee.
DAWASA wameshindwa kuhudumia watu milioni 7.4 wataweza vipi kuhudumia watu milioni 20 ifikapo 2050 kwa kutegemea mvua kunyesha wapate maji?
Katika nchi ambazo watawala wanafikiria ustawi wa watu, wananchi kukosa maji kiwango hiki tu cha miezi mitatu mfululizo, walitakiwa KUWAJIBIKA wote.
DAWASA, kuliko kuleta ratiba yenu ya upatikanaji wa huduma ya Maji kwa mpango wa dharura, ilitakiwa DAWASA kuvunjwa, Wizara ya Maji kufutwa kabisa.
Serikali ya CCM miaka 64 baada ya uhuru imeshindwa kuwapa watanzania maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Karne ya 21 maji ni kitu cha anasa. Loh!
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
. @MwananchiNews MNAMDANGANYA NANI?
Picha hii ilichapishwa mara ya kwanza 6 September 2017 katika ukurasa wa Facebook wa HELEN DAVIES (raia wa Uingereza) alipotembelea Jambiani na Kendwa, Unguja, Zanzibar akiwa na kundi la marafiki zake.
Gazeti kubwa na kongwe kabisa nchini la MWANANCHI linaitumia picha hiyo miaka mitano (5) baadae, 10 December 2025 katika habari yake kuonesha ongezeko kubwa la watalii Zanzibar, wakiwepo wataliano
Gazeti kongwe la MWANANCHI wanataka kutuaminisha nini wasomaji wa habari zao? Je, ni ukweli kwamba printing media imeharibika kiwango hiki? Kwamba wanaweza kudanganya watu katika zama hizi?
Nimeona utetezi wa MHARIRI wa MWANANCHI saa 24 baadae anasema “Katika taarifa hiyo tulitumia picha ya mtandaoni inayoakisi shughuli za Utalii Zanzibar na haikuwa picha mpya”. Picha za sasa zipo wapi?
Kwa akili hizi za huyu MHARIRI wa MWANANCHI ni kwamba, MELI ikizama Tanzania, MWANANCHI watatumia picha za TITANIC iliyozama mwaka 1912 kueleze hali ya meli kuzama Tanzania 2025?
Journalism ethics mmejifunza wapi waandishi wa sasa? A fundamental principle of professional journalism and advertising governs the ethics of misleading information in print media. Hamuelewi hii kitu kweli?
The ethics of mass media should involve being fair to the facts, accurate, responsible, and credible. Don't propagate rumors or myths, and don't make claims that can't be validated by reputable sources. HYFR.
Kitabu cha “The Elements of Journalism” kimeandikwa na Bill Kovach na Tom Rosenstiel (2001) kimeeleza vizuri ‘core principles of journalism’. Journalism’s first obligation is to the truth. Kinauzwa 24K AMAZON.
Nafikiri, vyombo vya habari ni sehemu imeharibika zaidi hata kuliko baadhi ya mifumo ya Serikali. Wahariri wa vyombo vya habari wamekuwa machawa wa Serikali na CCM, wanatumika kufanya propaganda kipuuzi.
MWANANCHI, basi hata mngelitumia picha za (vijana wapiga makachu) mseme ni watalii kutoka Barbados au Trinidad & Tobago wamekuja kutalii na kupiga misamba Zanzibar? ACHENI UPUMBAVU na UTAPELI..
MWANANCHI, meamua kuchagua fungu lenu, fungu la kutumikia uongo. Lakini mtambue, mnapoteza uhalali mbele ya hadhira ambayo ni wasomaji wa magazeti na habari zenu. Rudini katika misingi. Hamjachelewa.
Anaandika Martin Maranja ~
MWANANCHI, MNAMDANGANYA NANI?
Picha hii ilichapishwa mara ya kwanza 6 September 2017 katika ukurasa wa Facebook wa HELEN DAVIES (raia wa Uingereza) alipotembelea Jambiani na Kendwa, Unguja, Zanzibar akiwa na kundi la marafiki zake.
Gazeti kubwa na kongwe kabisa nchini la MWANANCHI linaitumia picha hiyo miaka mitano (5) baadae, 10 December 2025 katika habari yake kuonesha ongezeko kubwa la watalii Zanzibar, wakiwepo wataliano
Gazeti kongwe la MWANANCHI wanataka kutuaminisha nini wasomaji wa habari zao? Je, ni ukweli kwamba printing media imeharibika kiwango hiki? Kwamba wanaweza kudanganya watu katika zama hizi?
Nimeona utetezi wa MHARIRI wa MWANANCHI saa 24 baadae anasema “Katika taarifa hiyo tulitumia picha ya mtandaoni inayoakisi shughuli za Utalii Zanzibar na haikuwa picha mpya”. Picha za sasa zipo wapi?
Kwa akili hizi za huyu MHARIRI wa MWANANCHI ni kwamba, MELI ikizama Tanzania, MWANANCHI watatumia picha za TITANIC iliyozama mwaka 1912 kueleze hali ya meli kuzama Tanzania 2025?
Journalism ethics mmejifunza wapi waandishi wa sasa? A fundamental principle of professional journalism and advertising governs the ethics of misleading information in print media. Hamuelewi hii kweli?
The ethics of mass media should involve being fair to the facts, accurate, responsible, and credible. Don't propagate rumors or myths, and don't make claims that can't be validated by reputable sources. HYFR.
Kitabu cha “The Elements of Journalism” kimeandikwa na Bill Kovach na Tom Rosenstiel (2001) kimeeleza vizuri ‘core principles of journalism’. Journalism’s first obligation is to the truth. Kinauzwa 24K AMAZON.
Nafikiri, vyombo vya habari ni sehemu imeharibika zaidi hata kuliko baadhi ya mifumo ya Serikali. Wahariri wa vyombo vya habari wamekuwa machawa wa Serikali na CCM, wanatumika kufanya propaganda kipuuzi.
MWANANCHI, basi hata mngelitumia picha za (vijana wapiga makachu) mseme ni watalii kutoka Barbados au Trinidad & Tobago wamekuja kutalii na kupiga misamba Zanzibar? ACHENI UPUMBAVU na UTAPELI..
MWANANCHI, meamua kuchagua fungu lenu, fungu la kutumikia uongo. Lakini mtambue, mnapoteza uhalali mbele ya hadhira ambayo ni wasomaji wa magazeti na habari zenu. Rudini katika misingi. Hamjachelewa.
Mdau wa https://t.co/dDd21Ugmlv amehoji kuhusu uhaba wa maji unaojirudia kila Mwaka kwenye Mikoa ya Dar na Pwani, akisema, Viongozi hawawajibiki ipasavyo bali wanahadaa Wananchi kwa kutoa ahadi wanazojua hazitatekelezeka wakati malalamiko yanapokuwa mengi.
Shiriki zaidi https://t.co/FWm7SBMCMh
#JamiiAfrica #JamiiForums #JFMdau2025 #HudumaZaKijamii #JFHuduma