#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 240
Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Shahidi wa Kificho bwana P.
Anasimama Wakili wa Serikali anasema.... Tunaomba muongozo, ana cross wakati hajatenda document.
Mhe Lissu anajibu anasema naweka mambo sawa, sijaanza kucross, nataka nionyeshe kama kilichofanyika ni uzembe.
Wakili wa Kificho na yeye anasema Waheshimiwa Majaji kuna mambo mengine ni makosa ya kiubinadamu tu ila hizi taarifa zangu hazipaswi kuonekana.
πππ Ni kama upande wa Jamhuri walisahau kuficha taarifa za huyu Shahidi wa kificho kwa maana ya jina, anwani n.k sasa amejihami maana huko juu kasem zimefichwa wakat hazijafichwa, anahisi huenda Mhe. Lissu atachana mkeka.
Mhe Lissu: Waheshimiwa Majaji mimi nataka kuwaonyesha uzembe wao, wamedharau amri ya Mahakama, waliambiwa wafiche hawakuficha.
Jaji: Tuendelee
Mhe. Lissu: Anaanza kusoma kielelezoβ¦
Mhe Lissu: Anaainisha maelezo yake aliyoyatoa Mahakamani ambayo anatarajia kumkanusha ukilinganisha na maelezo ya kielelezo, na hapa Mhe. Lissu ameainisha maeneo 7 ambayo atamkanusha.
Shahidi wa Kificho P: Sawa (anakubali kukanushwa)
Mhe Lissu: Sasa ili nifanye hiyo kazi nahitaji haya maelezo yawe ushahidi, sasa nakuuliza kama unaridhia kuwa haya maelezo yatumike kama kielelezo cha ushahidi hapa Mahakamani.?
Shahidi wa Kificho P : Ndiyo
Majaji : Eeh? (huku wakiwatizama Mawakili wa Serikali )
Mawakili wa Serikali: Hatuna pingamizi Wahesh Majaji.
Jaji: Kielelezo kimepokelewa na kupewa alama ya D16
Mhe Lissu na Mawakili wa serikali: Asante Waheshimiwa Majaji.
Majaji : Tuendelee
Mhe Lissu: Waheshimiwa Majaji naomba shahidi apewe kielelezo D16
Anaendelea kusema sasa shahidi hayo maelezo ni ushahidi mbele ya mahakama, Sawa sawa?
Shahidi wa Kificho P :Sawa
Mhe Lissu: Sasa shahidi,
Kwenye ushahidi wako leo, umesema tarehe 3/42025 ulipewa maelekezo na boss wako John Maro ukiwa na wenzako watano na ukamtaja mmoja ambaye ni P1 kwenda Mkutano wa Chadema, Sawa Sawa.?
Shahidi wa Kificho P : sawa
Mhe Lissu: Sasa nataka usome maelezo yako hapo anzia hapo watu ulioongozana nao.
Shahidi wa Kificho P : Anasoma..... Niliongozana na P2
Mhe Lissu: sawa, nimesema leo tutaongea ukweli mtupu.
Mhe Lissu anaendelea....
Kwenye maelezo yako umesema wazungumzaji walikuwa Mwenyekiti, Makam mwenyekiti na Katibu mkuu, sasa onyesha hayo maelezo kwenye iko kielelezo???
Shahidi wa Kificho P : Hakuna, ni wewe peke yako
Mhe Lissu: Sawa Sawa
Anaendelea Mhe. Lissu kwenye shahidi wako ulisema kuwa mazungumzo yao ilikuwa ni namna gani wataenda kuingia kwenye uchaguzi, hapo kwenye kielelezo yapo au hayapo?
Shahidi wa Kificho P : Hayapo
Mhe Lissu: Tarehe 7/4/2025 ukiwa Dodoma kikazi ulipokea simu kutoka kwa boss wako John Maro sasa eleza kama kwenye maelezo yako polisi ulisema hayo hata kuitaja tu hiyo tarehe 7/4/2025?
Shahidi wa Kificho P : Hapana
Mhe Lissu: Sasa sema kuna sehemu ulipigiwa simu na boss wako John Maro akikueleza uende kituo cha polisi Dodoma? Eleza kama hayo maneno yapo.
Shahidi wa Kificho P : Hapana hayapo
Mhe Lissu: Kwenye ushahidi wako umesema uliambiwa ukakabidhi memory card yako ya video ya Chadema, uliyochukuwa tarehe 3/4/2025, sema kama maelezo hayo yapo?
Shahidi wa Kificho P: Hayapo
Mhe Lissu: Sasa shahidi, umesema baada ya kupigiwa simu ulienda Kituo cha Polisi na kukutana na polisi uliyemkabidhi memory card na akakuandika maelezo, sasa eleza kama yapo kwenye kielelezo D16?
Shahidi wa Kificho P : hayapo
Mhe Lissu: Kwenye ushahidi wako hapa Mahakamani ulisema nilikuwa nimevalia combat lakini rangi hukumbuki, sasa elezea kama hayo maneno ya yaliyokuwa yanaelezea nilivyovalia yapo?
Shahidi wa Kificho P : Hayapo
Mhe Lissu: Ulisema walizungumza maneno mengi lakini ulisikia hili la walilokuwa wanarejerea Uchaguzi mkuu, yapo.
Shahidi wa Kificho P : Hayapo
Part 241 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 239
Jaji Ndunguru anamuuliza Mhe. Lissu kama ana maswali ya Dodoso?
Mhe. Lissu anaanza kumshona Shahidi wa kificho bwana P bila ganzi.π
Mhe. Lissu : Ni kweli ama siyo kweli nyie Jambo TV mmefanya kazi na mimi kwa muda mrefu sana?
Shahidi wa kificho P: Ni kweli
Mhe. Lissu: Na ni kweli au si kweli kuwa, mmekuwa mkitangaza Mikutano yangu karibu nchi nzima.?
Shahidi wa kificho P : Ni Kweli
Mhe Lissu: Na mmekuwa mkicover habari zangu nchi nzima?
Shahidi wa kificho P: Ni kweli
Mhe Lissu: Na waeleze hawa Majaji kuwa hata nilivyotoka Ubelgiji mlinisindikiza hadi nyumbani kwangu?
Shahidi wa kificho P: sikumbuki
Mhe Lissu: Nitakukumbusha, ilikuwa ni waandishi habari Oscar na Shadrack Simba?
Shahidi wa kificho P: Ni kweli
Mhe. Lissu: Hata siku nilipokamatwa nilikuwa na hao waandishi wa habari Oscar na Shadrack Simba.?
Shahidi wa kificho P : Ni kweli
Mhe Lissu: Waeleze majaji kuwa ziara zote hizo tumekuwa tukienda safari moja?
Shahidi wa kificho P: Ni kweli
Mhe Lissu: Tumekuwa tukifikia hoteli moja na kula pamoja, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P : Ni kweli
Mhe Lissu: Nitakosea nikisema kuwa nyie waandishi wa habari pamoja na boss wenu John Maro tumekuwa tukifanya kazi kwa ukaribu sana?
Shahidi wa kificho P: hujakosea
Mhe Lissu: Nitakuwa nakosea nikisema mmekuwa marafiki zangu?
Shahidi wa kificho P: Hujakosea
Mhe. Lissu: Wakati vyombo vingine vikiogopa kucover habari yangu nyie hamkuoogopa kucover habari yangu.?
Shahidi wa kificho P : Ni kweli
Mhe Lissu: Ni kweli/ Si kweli kuwa mlifunguliwa kesi TCRA mara tu baada ya kurusha huo Mkutano wangu?
Shahidi wa kificho P : Sikumbuki juu ya hilo
Mhe Lissu: sasa baada ya hayo, elezea kama kuna mwanachadema yoyote amekutishia au kukudhuru kwa namna yeyote ile?
Shahidi wa kificho P : Hapana
Mhe Lissu: Waeleze wahe. Majaji kama toka uliporusha hayo matangazo kuna mtu yeyote/ afisa yeyote/ mamlaka yeyote ambako umewapa taarifa kuwa umetishiwa kwa namna yeyote ile?
Shahidi wa kificho P : Hapana.
Kwa msiofahamu Mawakili wa Serikali waliomba huyu Shahidi atoe ushahidi kwa Siri kwasababu walidai kwamba kuna Wanachama wa CHADEMA walimtishia maisha, leo anasema hajawahi kutishiwa kwa sisi Wanawake hii ni kama mtu kakupa umbea halafu badae anakukana anasema aku mie sijakwambia.ππππ
Anyways tuendeleee
Mhe Lissu: Waeleze wahe. majaji kama una hofu yoyote au uoga wowote wa kutoa ushahidi hadharani?
Shahidi wa kificho P: Nina hofu
Mhe Lissu: Ooh kwanini una hofu shahidi? Eleza ukweli wa Mungu wako.???
Shahidi wa kificho P : Nina hofu kwakuwa hili suala ni very sensitive, Viongozi mnaweza msiwe na shida ila watu wengine ikawa tatizo.
Mhe Lissu: kama nimekuelewa shahidi umesema hujawahi tishiwa na mwanachama yoyote wa Chadema na sasa umesema viongozi siyo tatizo, ni sawa sawa?
Shahidi wa kificho P : Ndiyo
Mhe Lissu: Eleza kama aliyekuandika maelezo ni Inspector Endrew
Shahidi wa kificho P : Ni kweli
Mhe Lissu: Sasa shahidi nitakusomea maelezo yako na nitakuonyesha maeneo ambayo umejichanganya na kisha nitaomba uiombe Mahakama kuyatoa kama kielelezo
Mhe Lissu: Waheshimiwa Majaji nataka kum- impitch shahidi, Naomba wakili apewe kielelezo
Mawakili wa Serikali wamekuwa busy kidogo na file la vielelezo.
Mhe Lissu: Naomba niseme off record, Mahakama ilitoa order kuwa taarifa za mashahidi zifutwe, lakini naona mawakili wa serikali ndiyo wanafuta muda huu.
Shahidi wa kificho P anapewa kielelezo na Mawakili wa serikali.
Mhe Lissu: Shahidi eleza mahakama hayo ni maelezo yako?
Naomba ueleze kama sehemu ya makazi, eneo, mtaa, no. ya simu kama imefichwa?
Shahidi wa kificho P : Ndiyo
Mhe Lissu: Eleza kama mwaka wako wa kuzaliwa na jina la mzee limefichwa?
Shahidi wa kificho P : Ndiyo limefichwa
Mhe Lissu: Shule ya msingi na Sekondary ulizosoma zimefichwa?
Shahidi wa kificho P :Ndiyo
Part 240 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 13, 2026
Jana tuliishia part 236 so leo tunaendelea na -;
Part 237
Hatimaye, mida hii ya saa. 11:07 Asubuhi, Mahakama inaanza.
Wanaingia Mawakili wa Serikali,
Anaingia Mhe. Lissu na kundi la askari magereza, leo akiwa na vibe la kutosha kama kawaida yake anasalmia ile salama yake (Peopleβs power πͺ) anazungusha mkono, anawasalimia waliopo kule juu kwenye kighorofa then anamalizia kwa waliokaa hapa chini.
Inapigwa High Cooooooourt ya kikakamavu watu wote tunasimama.
Wanaingia Majaji wapo watatu kama kawaida yao then wanaketi kwenye viti vyao.
Karani anasoma case No.β- Jamhuri vs Tundu Lissu
Anasimama Wakili wa serikali anatambulisha jopo la mawakili wa Serikali kisha kawambia Majaji mtuhumiwa yupo.
Wakili wa Serikali anaomba radhi kwa kuchelewa anasema sababu ni kwamba walikuwa wanatafuta Shahidi na kwamba shahidi alipata changamoto za usafiri, hivyo wako tayari kuendelea.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa yani Mhe. Lissu kama yupo tayari kuendelea na kesi.
Mhe Lissu anasema mimi niko tayari kuendelea lakini huu utaratibu wa kuchelewa naomba msiuruhusu, hii ni case ya Uhaini na ndo kosa kubwa lililotamkwa mpaka kwenye Katiba ya Nchi yetu, siyo kosa la wizi wa mbuzi.
Kesi inamshtakiwa mmoja lakini mpaka sasa ina mwaka mmoja na zaidi naomba Mahakama iwe inafuata amri zake.
Wakili wa Serikali leo tuna shahidi mmoja anaitwa P huyu ni Shahidi asiyejulikana (Shahidi wa kificho)
Shahidi wa kificho anaingizwa kwenye kizimbani lile banda kama la kuku niliwahi kupost hapa.
Jaji: Shahidi tutakuuliza na utatujibu unaumri gani, dini yako?
Shahidi wa Kificho (P) : Miaka 26, dini yangu ni Muislam
Shahidi wa kificho (P) anapewa msaafu na kuapa
Wakili wa Serikali Thawabu Issa anamuongoza shahidi wa kificho (P)
Wakili wa Serikali: P unajishughulisha na nini?
Shahidi wa Kificho (P) : Mwandishi wa habari Jambo Tv, nimekuwepo kuanzia 2023 mpaka sasa, majukumu yangu ni kuchukua matukio ya video na picha.
Wakili wa serikali: Ujuzi wako kwenye hiyo kazi?
Shahidi wa kificho P : Eeeeeeh Ujuzi wangu eeeeh
Shahidi wa kificho (P) anaweweseka, ni kama hajaelewa swali.
Wakili wa serikali: Shahidi elimu yako?
Shahidi wa kificho P : Elimu yangu ni Diploma ya uandishi wa habari, niliipata Chuo cha Habari DSJ mwaka 2023.
Wakili wa serikali: Kwa namna gani unafanya hizo shughuri??
Shahidi wa kificho P : Nafanya kwa kutumia vifaa ambavyo ni camera aina ya Sony NX
Wakili wa serikali: Umesema matukio ya picha na video., hiyo unatumia kwenye matukio gani?
Shahidi wa kificho P : Kwa video pekee, kwa matukio ya picha natumia Canon.
Wakili wa Serikali: Shahidi unakumbuka tarehe 3/4/2025 ulipata jukumu gani?
Shahidi wa kificho P : Siku hiyo nilipewa jukumu na boss wangu kwenda kucover Mkutano wa Chadema kule Mikocheni nikiwa na mwenzangu P1, Boss wangu ni John Marwa.
Wakili wa serikali: Mkutano ulikuwa wapi?
Shahidi wa kificho P : Makao makuu Chadema
Wakili wa serikali: Tuendelee hapo...
Shahidi wa kificho P : Tulipack vifaa na kujiandaa na tukio husika, ilikuwa mishale ya saa 4 asubuhi.
Wakili wa serikali: hali ilikuwaje mlipofika?
Shahidi wa kificho P : Tulikuta kuna wanachama wa Chadema lakini pia Waandishi wa habari wa channel zingine kabla ya viongozi wa Chadema kufika.
Wakili wa serikali: Kwa siku hiyo ulijiandaa kwa matukio ya aina gani?
Shahidi wa kificho P : Ilikuwa kwa ajili ya kuchukua matukio na kwenda mubashara.
Mawakili wa serikali wananong'onezana...., hapa ni kama shahidi hakuelewa swali.π
Wakili wa serikali: Mlikuwa mnarusha kwa njia gani?
Shahidi wa kificho P : Tulikuwa tunarusha kutoka kwenye matukio ya picha na kuyarusha YouTube.
Wakili wa Serikali: Majina mnayotambulika nayo kurusha mubashara???
Shahidi wa kificho P : kimyaa kidogo.....kisha anajibu; Jambo TV.
Part 238 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 11, 2026
Last time tuliishia Part 225 so leo tunaendelea na-;
Part 226
Jana Shahidi wa upande wa Jamhuri ACP Amin Mahamba alianza kutoa ushaidi wake na leo Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross-examination.
Mhe. Lissu : Unaweza kuiambia Mahakama kwamba ulifufuka lini?
ACP Amin Mahamba : Sijaelewa
Mhe. Lissu : Mke wa Amin Mahamba anasema kwamba Amin Mahamba alifariki, sasa iambie Mahakama ulifufuka lini?
ACP Amin Mahamba : Huyo Amin Mahamba anaetajwa sio mimi.
Mhe. Lissu : Kwahiyo ni ushahidi wako kuwa huyu Amini Mahamba ni mwengine sio wewe?
ACP Amin Mahamba : Ndio ni mwingine tena yeye ni mstaafu na wanasema alishariki kweli kama unavosema.
Mhe. Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama ulimshirikisha RSO kwenye upelelezi wako?
ACP Amin Mahamba : Sikumshirikisha
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama ulimshirikisha afisa yoyote wa TISS.
ACP Amin Mahamba : Sikumshirikisha
Mhe. Lissu: Unafahamu Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa?na kama uliishirikisha kamati ya ulinzi ya mkoa wa Dar es salaam?
ACP Amin Mahamba :Naifahamu na sikuwaashirikisha
Mhe. Lissu : Ulishirikisha ikulu?ofisi ya VP au Waziri mkuu?
ACP Amin Mahamba : Sikuishirikisha na sikuwaambia lolote.
Mhe. Lissu : Ulishirikisha ofisi ya DPP ndio nilishirikisha kanda maalum NPS.
Mhe. Lissu :Ulimshirikisha nani?
ACP Amin Mahamba: Incharge Mayenga
Mhe. Lissu : Umesema kokote kwenye nyaraka yako?
ACP Amin Mahamba : Sijasema na sijamtaja
Mhe. Lissu : Kwa mujibu wa sheria ya NPS mwenye jukumu la kuratibu upelelezi ni DPP na Mastate Attorney wake.
Waeleze ni DPP yupi au State Attorneys yupi?
ACP Amin Mahamba : Kimya
Mhe. Lissu : Jibu swali wewe Polisi
ACP Amin Mahamba : Sijaelewa swali.
Mhe. Lissu : Swali langu linahusu nani aliecordinate upelelezi?
ACP Amin Mahamba : Ni DPP Mwenyewe, aliteua mtu nilisema jana kuwa sijui jina lake alitoka ofisi ya DPP Dodoma na nilisema ana jina la kibantu nimesahau.
Mhe. Lissu : Tutaenda kwa DPP Mwakitalu atupe hilo jina tuko kwenye serious matters.
πππ inachekesha sana maana jamaa hajui jina la mpelelezi ambae alishirikiana nae kufanya upepelezi pamoja na kufungua faili la kesi hii.
Mhe. Lissu : Umesema wewe ni mpelelezi wa muda mrefu umewahi peleleza kesi ya kisiasa?
ACP Amin Mahamba : Sijawahi
Mhe. Lissu : Kesi ya uhaini ni kesi kubwa sana ni highest in the land kwahiyo hujawahi kabisa na hii ndo kesi ya kisiasa ya kwanza.??
ACP Amin Mahamba : Sijawahi hii ndio ya kwanza
MheZ Lissu : Umewahi peleleza kesi ya mtu alikuwa mbunge na kiongozi wa Chama kama lissu?
ACP Amin Mahamba :Sijawahi
Mhe. Lissu : Umesema kitengo chako kinashugulika na makosa ya mtandao
ACP Amin Mahamba : Ndio
Mhe. Lissu: Ushapeleleza kesi ya cybercrime?
ACP Amin Mahamba : Ndio nimewahi.
Mhe. Lissu : Kesi gani shahidi?
ACP Amin Mahamba ; Nakumbuka nikiwa RCO Kinondoni
Naona kasita kama dakika 5 hivi then akasema kesi ya Mbowe na Mzee wa karatu Slaa
Mhe. Lissui : Waeleze ilikuwa inahusu nini na iliishaje?
ACP Amin Mahamba ; DPP hakuwa na interest ya kuendelea na kesi ikaisha hewani.
Mhe. Lissu : Una kesi zingine zaidi ya hizi kwenye cybercrime?
ACP Amin Mahamba ;Hapana
Mhe. Lissu: kwahiyo hauna kesi nyingine zaidi ya hiyo iliyofutwa?
ACP Amin Mahamba : Ninazo nyingine nyingi siwezi kuzikumbuka nikiwa RCO na OCCID.
Mhe. Lissu : Kwahiyo jana kweye ushahidi wako unasema mimi ndie niliechapisha video yangu hapa mtandao wa Jambo tv?
ACP Amin Mahamba : Ndiyo nilisema.
Mhe. Lissu ; Unafahamu maana ya neno kuchapisha mtandaoni?
ACP Amin Mahamba : Ndio nafahamu lakini sheria ambayo imetumika kukushitaki sio Cybercrime.
Mhe. Lissu : Waeleze waheshimiwa majaji kama mm ndie nilisambaza video za YouTube kwenye mtandao wa Jambo tv?
ACP Amin Mahamba : Ndio ni wewe ulisambaza hizo video.
Part 227 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 24
Anaendelea John Seka
Seka Anamuongelesha anasema unanisikia au hunisikii. Anatumia sauti ndogo sana. Umenisikia?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nakusikia
John Seka: Pale ofisi ya Admission si kuna Meza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Ukubwa wa meza zilizopo hapo admission ukoje?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sikumbuki.
John Seka: Katika maisha yako uliwahi kumuona wakili na mteja wake gerezani wanaongea?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Huwa wanakaaje?
Ntamamiro (Bwana jela) : Wanakaa kutazamana katikati yake kuna meza?
John Seka: Sasa narudi hapo. Kabla ya kesi hii uliwahi mfahamu Nashon Nkungu, Paul Kisabo?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nimewahi kukutana nao.
John Seka: Ulikutana nao wapi? Katika mazingira yapi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Akija kuongea na mteja wake gerezani.
John Seka: Ulituambia stage za wakili akifika. Anaandika jina nje, kitabu kinaletwa kwako. Unaruhusu. Sasa tuambie unamuona wakati gani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ofisi zote ni zangu.
Jaji: Jibu ni wapi hapo Gerezani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nilikutana nae Kwa Recha.
John Seka: Kumbe hata Kisabo ulimfahamuje?
Ntamamiro (Bwana jela) : hivyo hivyo kumuona akizungumza na mteja.
John Seka: Umewahi kuwaona wakifanya mahojiano?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
John Seka: Umekumbuka wakati Lissu anafanya mahojiano nani na nani anakuwa ndani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Wanakuwa nje wote. Lakini wanachungulia kwa mlangoni.
John Seka: Unakumbuka tarehe ipi na ipi ulikuwepo na ipi haukuwepo?
Ntamamiro (Bwana jela) : Siwezi kukumbuka.
John Seka: Sasa nitakupitisha tarehe moja hadi nyingine?
Jaji: Amesema hakumbuki nafikiri huko muache acha libaki hivyo.
John Seka: Nitakuwa sahihi nikisema wewe hujawahi hudhuria majadiliano kati ya Lissu na mawakili wake?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
John Seka: Mengi yaliyotokana na hayo wewe hukuwa unahusika moja kwa moja zaidi ya mrejesho.
Ntamamiro (Bwana jela): sio lazima feedback
John Seka: wewe hujawahi hudhuria mazungumzo ya Lissu na wanasheria wake. Huwa unapita tu. Unayoyaona.
Ntamamiro (Bwana jela) : nakagua napita.
Jaji: Hebu sikia kati ya wewe na hao akina Recha, Mumbii anaeweza kuelezea?
Ntamamiro (Bwana jela): Ni sahihi.
John Seka: Sasa tutajie majina yake.
Ntamamiro (Bwana jela): Siwakumbuki.
John Seka: Wakati wote maelekezo yako yalikuwa yanafuatwa ukiwaagiza kwenda kusimamia?
Ntamamiro (Bwana jela) : Mimi ni Mkuu wa Gereza sio lazima niambiwe feedback naweza kujua kwa namna nyingine.
John Seka: Kumbe ulijua kuwa mahojiano na Lissu na mawakili wake yamefuata taratibu kupitia mbinu zako zingine.
Ntamamiro (Bwana jela) : ndio
John Seka: Hao waliokufikishia hizo taarifa au hizo mbinu zako zingine umezielezea kwenye kiapo chako?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hapana.
John Seka: Paul Kisabo na Nashon Nkungu. Wakiwa kwenye mahojiano kunakuwa na askari wanakaaa kulia na kushoto kwa Lissu na Kwa Nashon na kisabo nyakati zote.
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio kweli.
John Seka: Ulikuwepo muda wote mahojiano yanapofanyika?
Ntamamiro (Bwana jela) : Napata taarifa kupitia vyanzo yangu.
John Seka: Nimemaliza Majaji. Aendeleee Edson Kilatu.
Anasimama Wakili Edson Kilatu
Adv Kilatu: Ukifika ukonga getini kuna kitabu cha ku register magari?
Ntamamiro (Bwana jela): Sahihi
Adv Kilatu: Anayeshughulikia registration zote sio wewe kwenye vitabu vya kuingia vya magari, raia wa kawaida na kitabu cha mawakili?
Ntamamiro (Bwana jela): Ni sahihi
Adv. Kilatu: Ni sahihi hakuna kiapo cha mtu anayesimamia hizo registration pale Ukonga? Hakijaja hapa mahakamani.
Ntamamiro (Bwana jela) : Hakipo.
Adv. Kilatu: Hii Register book uliyoileta hapa Mahakamani SUPP 1,2,3 ni nyaraka ya magereza hakuna sahihi za mawakili mle. Ni nyaraka yenu tu.
Ntamamiro (Bwana jela): sahihi
Part 25 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 23
Wakili wa waleta maombi John Seka anaendelea kumdodosa Shaidi ambae ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Andrew Shaban Ntamamiro (Bwana jela)
John Seka: Moja ya sheria ni sheria ya magereza ambae umeisomea na kuibobea?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
John Seka: Kanuni za magereza je?
Ntamamiro (Bwana jela) : Nazo ni muhimu sana. Zinatumika.
John Seka: Kwenye kanuni hizo unapaswa kutii kanuni ya 13 ya uendeshaji wa kanuni za Magereza?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Ibara ya 29(1) inasemaje?
Ntamamiro (Bwana jela) : Kila mtu anayo haki ya msingi ya kufaidi haki za binadamu kama zilivyofafanuliwa ibara ya 12 hadi 28 ya Katiba hii.
John Seka: Ni nani na nani wana haki ya kufaidi haki mbalimbali?
Ntamamiro (Bwana jela) : Watu wote.
John Seka: Hata wewe?
Ntamamiro (Bwana jela) : hata mimi.
John Seka: Hata Tundu Lissu:
Ntamamiro (Bwana jela) : Hata Lissu.
John Seka: Hata Kisabo?
Ntamamiro (Bwana jela): Hata Kisabo
John Seka: Hata Maduhu na Nashon
Ntamamiro (Bwana jela) : Hata Maduhu
John Seka: Nashon Je?
Ntamamiro (Bwana jela): Hata Nashon.
Watu wanacheka. Wanamuona zamwamwa sijui πππ
John Seka: Haya rudi ibara ya12 sasa kule.
John Seka: soma ibara 29(2) na useme inasemaje?
Ntamamiro (Bwana jela) : kila mtu ana haki ya kupata hifadhi sawa chini ya sheria.
John Seka: Hadi Lissu akiwa mikononi mwako Ukonga?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sahihi
John Seka: Nenda Kanuni ya 13 ya kanuni za Magereza na utuambie miaka 31 ya uzoefu wako ni lini uliifahamu kanuni hii?
Ntamamiro (Bwana jela) : Tangu nilipoanza Kazi.
John Seka: Isome kwanza.
Ntamamiro (Bwana jela) : mfungwa atapewa haki ya kuongea na wakili wake kwa faragha lakini awe anaonekana lakini sio kuwasikiliza.
John Seka: Umeielewa kweli hicho kifungu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio mfungwa atapewa nafasi ya kuongea na wakili wake na kufanyika kwa kuona lakini sio kusikiliza.
John Seka: Kuna haki ya mfungwa na kuna haki ya mshauri wa kisheria kwenye kanuni hiyo?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Haki ya mfungwa kusaidiwa kupewa nafasi ya kuongea na mshauri wake wa kisheria yaani Wakili.
Ntamamiro (Bwana jela): Ndio
John Seka: haki ya pili ni ya mawakili kupata fursa ya kuongea na mfungwa kwa faragha bila ya kusikilizwa ni kutazamwa tu.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Hii haki huwa unasomewa au ni uzoefu? Hii kanuni ya 13.
Ntamamiro (Bwana jela): Sijaelewa swali.
Seka: ili uwe na ujuzi huo wa kutazama bila kusikiliza kuna chuo kinachofundisha? Au ni uzoefu wa kazi?
Ntamamiro (Bwana jela) : Katika uzoefu wa kazi unasema hapa natazama na sisikilizi.
John Seka: Kwahiyo utekelezaji wa jambo hili unategemea mtu na mtu?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hakuna standard zilizowekwa.
John Seka: Kwenye nyaraka zako na maelezo yako ulikuwa unasema simamia? Maana yake ulikuwa unasema simamia lakini wasisikilize.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio.
John Seka: Ukubwa wa Chumba cha Ofisi yako ukoje?
Ntamamiro (Bwana jela) : wakutosha tu.
John Seka: Huwezi kukadiria?
Ntamamiro (Bwana jela) : Ndio
Jaji: Ofisi yako hujui ina ukubwa gani?
Ntamamiro (Bwana jela) : Wakutosha.
Jaji: Tunatosha wote humu ndani tukija ofisini kwako?
Ntamamiro (Bwana jela) : Hamuwezi kuingia.
Jaji: Bado unasema ni ukubwa wa kutosha?
Ntamamiro (Bwana jela) : Sio
Jaji: Haya jibu swali sasa.
Anasimama Nalindwa Sect. 93 ya Prison Act inasema ramani ya gereza isitolewe. Ukubwa wa hizo ofisi ni hatari.
Jaji Mruma: Hakuna ramani ya gereza wala kifungu hakisemi hivyo. Shahidi jibu swali tunataka sana kujua ukubwa wa ofisi yako ni jambo muhimu sana.
Ntamamiro (Bwana jela) : Ni ofisi iko umbali kutoka hapa nilipo hadi hapo kwako.
John Seka: Sasa ofisi yako ya kaimu wako Recha ni ofisi ya nani kubwa?
Ntamamiro (Bwana jela): Yakwangu ndio kubwa.
Part 24 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Duo ya Singida na Musoma ni Ugali moto Mboga moto haijawahi kutokea Tanzania,,, imagine mtu kabanana Behind Bars hadi leo wala hawazi na hamna kuleta unyonge
M/kiti Bendera Chuma,,, Makamu Mlingoti Chuma lazima uteme Bungo πππ
Hatutasahau kuwa October 2025 Samia Suluhu ali terrorise nchi nzima akauwa watu zaidi ya elfu 10 akijilazimisha kuwa rais.
RIP to our fallen heroes.
Tutadai uwajibikaji hadi tone la mwisho.
#MO29#TanzaniaMassacre