Mtu akiweka email yako kwenye hii website inaonyesha location uliyopo, locations ulizokuwepo, mitandao ya kijamii uliyotumia sometimes mpaka namba za simu😳
Mama wa mihogo anapambana na baridi na moto kila asubuhi ili wengine waanze siku vizuri. Wakati mwingine anakukopesha hata akiwa hana. Ukimuona leo, mheshimu. Anauza mihogo, lakini anabeba maisha ya familia yake na watu wa mtaani mabegani. 💔❤️
TEMBELEA HOSPITALI,
Tembelea hospitali,
- ukauone unyonge wa mwanadamu. Ukaone jinsi miili yetu iliyojaa nguvu leo inavyoweza kusalishwa na maumivu. Hata wale waliokuwa na sauti kuu, leo wanalala vitandani wakiomba msaada wa kugeuzwa upande wa pili.
Tembelea hospitali,
- ukaione thamani ya pumzi unayoivuta bure. Utawaona ndugu zetu wanaolipia mamilioni ya pesa ili tu mashine iwasaidie kupata hewa unayoipata wewe ukiwa umelala au unatembea. Utajifunza kuwa uhai si haki yako, bali ni neema tu.
Tembelea hospitali,
- ukauone ukomo wa elimu, vyeo, na madaraka. Katika korido za wodini, hakuna profesa wala fundi, hakuna bosi wala kibarua; wote wamevalishwa mavazi yanayofanana, wakisubiri kudra za Muumba na mikono ya matabibu. Hapo ndipo utajua kuwa cheo ni dhamana, lakini afya ni utajiri mkuu.
Tembelea hospitali,
- ukajifunze maana ya uvumilivu na tumaini. Ukawaone wale ambao wamekaa wodini kwa miezi, wakitabasamu kwa kila hatua ndogo ya nafuu wanayoipata. Utajifunza kuacha kulalamika kuhusu chakula usichokipenda au nguo usizozitaka, maana kuna mtu anaomba tu aweze kumeza tone la maji bila maumivu.
Tembelea hospitali,
- ukauone upendo wa kweli. Utawaona ndugu wanaokesha bila kulala, wakifuta jasho na kuliwaza wagonjwa wao. Utajifunza kuwa watu ni bora kuliko vitu, na kuwa na mtu wa kukushika mkono wakati wa dhiki ni baraka isiyo na mfano.
Tembelea hospitali,
- ukajikumbushe kumshukuru Mungu kwa kila kiungo chako kinachofanya kazi. Utawaona waliofungwa bandeji, waliopoteza viungo, na wale ambao akili zao zimechoka. Utatoka hapo ukiwa na moyo wa shukrani, ukijua kuwa "Mzima ana matumaini, lakini mgonjwa ana hitaji moja tu—kuwa mzima."
Tembelea hospitali,
- ukakumbushwe kutumia muda wako vizuri ukiwa na nguvu. Fanya kazi kwa bidii, saidia wenye uhitaji, na hubiri amani; maana siku za giza zikija, utatamani ungekuwa umefanya mengi zaidi wakati wa nuru.
TEMBELEA HOSPITALI,
- Ukajifunze unyenyekevu na kumpenda jirani yako. Maisha ni kama upepo, yanapita haraka sana. Jitahidi kuacha alama ya wema kila unapopita, ili hata ukidhoofika, kumbukumbu za wema wako ziwe dawa kwa waliovunjika moyo.
*TUMWOMBE MUNGU
atujalie afya ya mwili na roho, na atupe mioyo ya huruma kwa wanaoteseka, tukiwakumbuka daima katika maombi yetu.
Mwenyezi Mungu akutunze na kukulinda na maradhi.
Maneno ya Mwisho ya Sulemani kwa Vijana
1. Ni kheri vijana tumtumikie Mungu tukiwa na nguvu.
2. Kumkumbusha kijana kuwa maisha ni mafupi na mwili huu tulionao unaisha na kuchoka.
3. Sulemani anawaelekeza vijana kwa Mungu kwamba roho anayeimiliki ni Mungu so ni kheri tumpende Mungu tukiwa vijana
Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Marekani Bw. Washington anamwita Ikulu Msiri na Mshauri wake Bw. James Madison ili amweleze nia yake ya kung’atuka madarakani.
Madison anapinga vikali na kumjibu, “…Hakuna mtu mwingine wa kutuvusha kwa sasa ila wewe”!
Mnamo Mei 5, 1792, ndani ya Nyumba ya Rais iliyokuwa katika Mtaa wa Sokoni, Philadelphia, George Washington alimwita Bw. James Madison—aliyepata kuwa Rais wa nne wa Marekani—safari hii kwa mazungumzo mazito. Marekani ilikuwa ndio kwaza imetimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake, lakini rais wake wa kwanza tayari alikuwa akifikiria kuondoka madarakani—na kuiacha nchi ikiwa bado changa kabisa.
Washington, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 60 (alizaliwa Februari 22, 1732), alimweleza Madison kuwa hakuwa na nia ya kuwania muhula wa pili. Alichoka sana na maisha ya utumishi, na alihisi amezeeka sana kuliko umri wake.
Washington alikuwa na sababu nyingine kuu—Alitamani kurejea Mount Vernon, ambako angepata fursa ya kujiendeleza katika kilimo, usimamizi wa ardhi, na maisha ya shamba.
Madison alipinga vikali wazo hilo. Kwa mtazamo wake—na wa viongozi wengi wengine—uwepo wa Washington Ikulu ulikuwa ndio ulioshikilia pamoja jamhuri changa ya Marekani, iliyoundwa na makoloni yanayojitegemea.
Kisa cha Rais Aliyesita Kuwa Rais
Washington hakuwahi kutamani urais tangu mwanzo. Katiba ilipoanza kutumika, Wamarekani wengi waliamini kuwa yeye ndiye mtu pekee aliyekuwa na heshima ya kitaifa, uwezo na uhalali wa kuyaunganisha majimbo yaliyoungana. Washington alichaguliwa kwa kauli moja na akaapishwa kuwa rais wa kwanza wa Marekani mnamo Aprili 30, 1789.
Hata hivyo, tangu mwanzo, Washington alikuwa na hofu kubwa kuwa kushikilia madaraka kwa muda mrefu kungeugeuza urais wa Marekani kuwa sawa na ufalme. Kimsingi, waasisi wote wa taifa la Marekani walikuwa na hofu hii. Hatumaye, Hofu hii ilikuwa kiini cha mawazo ya Washington mwaka 1792.
Salamu ya Kuaga ambayo kidogo itolewe kabla ya wakati
Katika mazungumzo yao, Washington alimwomba Madison amsaidie kuandika hotuba ya kustaafu—hotuba ambayo baadaye imekuja kujulikana kama Hotuba ya Kuaga (Farewell Address). Madison alipinga, akisema kuondoka kwa Washington kungelidhoofisha taifa wakati ambao migawanyiko ya kisiasa ilikuwa ikiongezeka.
Hatimaye, Washington alikubali kubaki. Aliwania tena, akachaguliwa kwa kauli moja, na akaanza muhula wake wa pili mnamo Machi 4, 1793, akihudumu hadi Machi 4, 1797. Ndipo alipostaafu rasmi—akiweka mfano bora na msingi kwa Maraisi wa Marekani kuondoka madarakani kwa hiyari, hali iliyokuza demokrasia na kudumu kwa vizazi vingi.
Maisha Baada ya Urais
Tamaa ya Washington kurejea nyumbani ilikuwa ya dhati. Kule Mount Vernon, alisimamia shamba kubwa na alikuwa akimiliki watumwa wa kutosha. Katika maisha yake, alimiliki mamia ya watu waliokuwa utumwani (ikiwemo wale waliokuwa chini ya umiliki wa mali ya mke wake). Katika miaka ya mwanzoni ya 1790, idadi ya watumwa waliokuwa chini ya mamlaka yake ilikuwa zaidi ya 70, hali inayoonyesha uhalisia wa maisha kwa wakati huo.
Urithi wa Kudumu
Kusita kwa Washington mwaka 1792 kunaonyesha jambo muhimu kuhusu uongozi wake: haukutokana na tamaa ya madaraka, bali uzalendo wake kwa taifa. Kwa uamuzi wake wa awali wa kuondoka mapema—na baadaye kuachia madaraka baada ya mihula miwili—alisaidia kuufafanua urais kama amana ya muda ya umma, si mali ya maisha yote. Kwa kufanya hivyo, aliumba si tu ofisi ya urais, bali pia tabia ya taifa lenyewe hadi hivi sasa.
Wale wakoma hawakumuomba Mungu moja kwa moja, bali walichukua hatua ya ujasiri wakiwa katika hali ya kukata tamaa.
Walisema, “Tukikaa hapa tutakufa, hebu twende kwa Washami.”
Kwa macho ya kawaida, ilikuwa ni uamuzi wa kibinadamu tu, lakini kwa macho ya kiimani, ilikuwa hatua ndogo yenye tumaini na humo ndipo Mungu akaingilia kati.
Mungu hakusubiri maneno yao, bali aliona imani iliyofichwa katika tendo lao.
Alitumia hatua yao ndogo kama chombo cha kuleta wokovu kwa taifa zima la Israeli.
Washami waliposikia sauti ya magari ya vita na kukimbia, ikawa ni ushuhuda kwamba Mungu anaweza kutenda hata kupitia watu waliopuuzwa na walio nje ya kambi ya waamini.
Hii inatufundisha kwamba Mungu si lazima ajibu tu maombi ya maneno, bali anaweza kufanya kazi kupitia uamuzi, ujasiri, na imani kimya kimya.
Wakati mwingine, unachohitaji si sala ndefu, bali kuchukua hatua ya imani kwa sababu Mungu huona ndani ya moyo, na hutumia hatua ndogo za wanadamu kutimiza makusudi yake makubwa.
Hakuna mtu anayekupenda na kuku-treat vizuri kama yule usiyemhitaji kabisa, yaani wale huwa wanapenda kweli kweli mpaka unatamani umbadilishe awe yule anayekuzingua.
Ellen G. White, mwanamke ambaye aliwasha taa ya Kanisa la Wasabato,
Lakini pia alizua wingu la "siri" zinazochukua nafasi kwenye mioyo ya watu hapa Tanzania.
Je, alikuwa nabii wa kweli aliyepewa maono ya kimungu, au kuna ukweli uliofichwa nyuma ya hadithi yake kama siri ya kale?
Siri za Ellen G. White
Thread/Uzi
Follow @udsm_finest