@ccm_tanzania Kupiga kura siyo kushiriki uchaguzi. Kushiriki uchaguzi ni pale kura yako inapohesabiwa kuwa ni ya mgombea iliyempigia kura na hii inaanzia kwa chama kuwapa wananchi mgombea aliyependekezwa na wanachama siyo kamati kuu.
Vifo vya wateule wako unaviona haraka na kuvitolea matamko, lakini watu kutekwa na kupotezwa huoni. Tena kwa bahati mbaya sasa unaogopa hadi uchaguzi, ulijipitisha kwenye chama chako bila kupingwa wala ushindani. Sasa kwenye uchaguzi mkuu unataka kufanya mchezo huohuo kwa kutumia polisi na makada wa ccm uliowateua kwenye tume. Ukaenda mbali zaidi kumpa Lissu kesi ya uhaini ili asiwepo wakati unajipitisha. Hakika kesho huijui lakini Mungu anaenda kuangusha utawala wako mwaka huu. Mark this words. #FreeTunduLissu #NoReformsNoElection