Nimepokea kwa majonzi na masikitiko taarifa ya kifo cha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali (Mstaafu) David Bugozi Musuguri. Naungana na wana Butiama, wana Mara na Watanzania kwa ujumla kuomboleza msiba huu wa kaka, baba na kiongozi wetu marehemu. R.I.P 1920-2024
Siku ya Maombi na Dua ya kuliombea Taifa kuelekea Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango. Leo Aprili 22, 2024
Mapema hii leo nilishiriki Mbio za Bunge Marathon zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, Mgeni Rasmi alikuwa Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb). Tarehe 13 Aprili, 2024.
Leo Tarehe 13 Aprili, 2024 Nimeshiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Miaka 102 tangu kuzaliwa Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma, Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango.
baada ya kuwa mtoro kwa muda mrefu kwa sababu ya kukosa mahitaji katika Kitongoji Nyamtangariko, Kijiji cha Kamugegi kata ya Kamugegi Wilaya ya Butiama.
Mkurugenzi wa Shirika la SAGCO @MMwakasasa ametoa msaada wa vifaa vya kujifunzia, begi la shule, pesa ya sare ya shule, mchele kwa ajili ya Sikukuu ya Iddi kwa Mwanafunzi Yohana Nyamarungu anayesoma Kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Kamugegi,
Kipekee nakushukuru sana Mhe. RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini na kuniteua tena kuhudumu katika Serikali yako kwa nafasi ya Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Wizara ambayo ndio msingi wa usimamizi wa Sheria na Haki.
Nitoe pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na Wananchi wote wa Jimbo la Kikwajuni.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina.
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mzee wetu Masauni Yussuf Masauni Baba Mzazi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, kilichotokea leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Kwenye mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa, yaliyofanyika Kijijini kwao Ngarash, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha. Leo Tarehe 17 Februari, 2024