VIDEO:
Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe , ameeleza kuwa Shule ya Sekondari Tosamaganga imekuwa na mchango mkubwa na wa pekee katika kujenga msingi imara wa safari yake ndefu ya uongozi na kisiasa.
Akizungumza katika maadhimisho ya kutimiza karne moja (miaka 100) tangu kuanzishwa kwa shule hiyo kongwe mwaka 1926, Zitto amekumbuka maisha yake ya uanafunzi na kufichua kumbukumbu ya kuwahi kuwa kiranja mkuu wa siku moja, jambo ambalo linaakisi mbegu za uongozi zilizopandwa ndani yake tangu enzi hizo.
Maadhimisho hayo ya miaka 100 ya Shule ya Sekondari Tosamaganga yametumika kama fursa ya kutambua na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na taasisi hiyo ya elimu katika kuandaa viongozi mbalimbali nchini, huku Zitto akisisitiza nafasi ya pekee iliyo nayo katika historia ya maisha yake binafsi.
VIDEO:
Kiongozi wa Chama mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe @zittokabwe , ameongoza harambee maalum ya kuchangisha Shilingi bilioni moja kwa lengo la kuboresha miundombinu mbalimbali katika Shule ya Sekondari Tosamaganga, ikiwemo ujenzi wa mabweni na utatuzi wa changamoto zingine zinazowakabili wanafunzi.
Katika mchakato huo, huku kukiwa na mafanikio ya awali ya kukusanya Shilingi milioni 500 kutoka kwa wadau na wanafunzi wa zamani waliopitia shuleni hapo, leo wameanzisha awamu mpya ya kukusanya kiasi kilichobaki cha milioni 500, ambapo zaidi ya Shilingi milioni 180 zimeshaahidiwa siku ya leo pekee.
Wakati wa harambee hiyo, wahitimu na wanafunzi wa zamani wa shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1926 na wamisionari wa Consolata walihimizwa kuendelea kujitoa kwa dhati kuchangia maendeleo ya shule hiyo ili kuacha alama ya kudumu na kulinda historia adhimu ya taasisi hiyo iliyotoa viongozi wengi wakubwa nchini.
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa, amepinga dhana kwamba ni lazima kuwepo na wasimamizi au wasuluhishi kutoka nje ili kufikia maridhiano ya kisiasa yenye tija nchini, akitolea mfano jinsi mwafaka uliosimamiwa na Jumuiya ya Madola (Commonwealth) ulivyofeli vibaya kuliko mikataba yote ya ndani.
Akizungumza Septemba 8, 2026, katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Kutafakari Hali ya Siasa nchini unaofanyika mkoani Dar es Salaam, Jussa ameshirikisha uzoefu wa kihistoria wa Zanzibar katika kutafuta suluhu ya migogoro ya kisiasa, akichambua makubaliano mbalimbali tangu mwaka 1995 hadi sasa
Jussa ameeleza kuwa baada ya uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995, kulianzishwa mazungumzo yaliyochangiwa na utatuzi wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth). Mchakato huo ulioanza mwezi Agosti 1996 ulichukua takriban miaka mitatu ya diplomasia kutokana na wasuluhishi kulazimika kwenda upande mmoja na kurudi kwa mwingine kuwasilisha ujumbe, hadi uliposainiwa rasmi mnamo Juni 9, 1999.
Hata hivyo, mwanasiasa huyo ameweka wazi kuwa mwafaka huo uligubikwa na mbwembwe nyingi na haukuwa mzuri zaidi katika utekelezaji. Ameongeza kuwa licha ya makubaliano kuainisha kuwa Jumuiya ya Madola ingekuwa dhamana ya kimaadili (moral guarantor) ya kusimamia utekelezaji, barua zote walizoandikiwa kulalamikia kutoendelea vizuri kwa mambo hazikupata majibu ya maana, na jumuiya hiyo ilionesha nia ndogo sana ya kufuatilia
Tofauti na uzoefu huo wa nje, Jussa ametoa mfano wa Mwafaka wa pili wa mwaka 2001, ambao ameuita kuwa ndio uliokuwa makubaliano madhubuti na yenye mnyororo mpana zaidi wa masuala katika historia ya nchi
Amesema mwafaka huo wa mwaka 2001, pamoja na mazungumzo ya mwafaka wa tatu yaliyojenga msingi wa Maridhiano ya kihistoria ya mwaka 2009 kuelekea 2010, yote yalifanywa na kusimamiwa na watendaji wa ndani pekee bila uwepo wa msimamizi yeyote wa nje au wa kati.
Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, Ismael Jusa, amesema si lazima mazungumzo ya kisiasa ya yasimamiwe na msuluhishi wa nje ili yawe na tija, akieleza kuwa uzoefu wa Zanzibar mwaka 2001 unaonyesha kuwa pande zinazohusika zinaweza kufikia mwafaka zenyewe.
Wanachama 168 wa Chadema wakiongozwa na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Godson John Mmbaga, CUF wakiongozwa na aliyekuwa Katibu wa Wilaya wa Chama hicho Ndugu Ally Ramadhan wamejiunga na ACT Wazalendo na kupokelewa na Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu leo tarehe 23 Mei 2025.
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu amefanya ziara ya Kata kwa Kata kukagua uhai wa Chama katika Jimbo la Same Mashariki kwa kutembelea Kata za Bombo, Vuje, Mtii, Lugulu, Miamba na Ndungu leo tarehe 22 Mei 2025.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, leo Alhamis ya Mei 22, 2025 amehudhuria Akdi ya Arusi, Shughuli ambayo imefanyika huko Masjid Shifaa, Msikiti uliopo Michenzani, Mkoa wa Mjini- Magharibi, Unguja.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, leo Alhamis ya Mei 22, 2025 amehudhuria Akdi ya Arusi, Shughuli ambayo imefanyika huko Masjid Shifaa, Msikiti uliopo Michenzani, Mkoa wa Mjini- Magharibi, Unguja.