Mwalimu wa Sekondari Mbeya aripotiwa kushikiliwa na Polisi kwa zaidi ya wiki tatu
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Itunge iliyopo wilayani Kyela, mkoani Mbeya, Anyambilile Ibrahim Mwamwile, anayejulikana pia kama Nickodem Kitalati katika mitandao ya kijamii, anaripotiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mbeya (RCO) kwa zaidi ya wiki tatu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, kukamatwa kwa mwalimu huyo kunadaiwa kuhusishwa na chapisho aliloliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook lenye ujumbe wa โTundu Lissu aachiwe huru.โ
Licha ya Mkuu Shule ya Sekondari Itunge, Aliko Mwaseba, pamoja na Mke wa Mtuhumiwa kufika Polisi Mara kadhaa kumuwekea kufuatilia suala lake, Polisi wamegoma kumwachia.
Hadi sasa, Jeshi la Polisi halijatoa taarifa rasmi kueleza sababu za kuendelea kumshikilia mwalimu huyo wala kuthibitisha tuhuma zozote zinazomkabili.
Je, unaonaje suala hili? Je, vyombo vya dola vinapaswa kutoa taarifa rasmi mapema pale mtu anaposhikiliwa kwa muda mrefu?
Maisha kwa wanaume yana mafumbo sana unapambana unapata magari makali, nyumba kali, mke mkali.
Siku isiyo na jina wala taarifa unafariki ghafla tu na kuviacha vyote kuanzia nyumba, magari,watoto na mke.
Maajabu ni kwamba ukiwa haupo duniani na hujui yanayoendelea huku nyuma unashangaa mali zako zinaleta ugomvi watu waliokuwa wamekaa tu wanapambana wachukue jitihada zako zote.
Mke wako nae anaolewa na mtu mwingine na huenda wakaishi kwenye hiyo nyumba yako kali๐
NB:Hatutishani mapambano yaendelee ila ni moja ya ukweli mchungu kuhusu maisha๐
Nimempoteza BRO WANGU MDUDE kwenye hizi harakati.
Leo kwasababu ya Njaa zangu nianze kujali tumbo langu nikatishe tamaa watanzania ambao wanaamua kuandamana kumpigania ndugu yangu?
Mimi miaka miwili nahudhuria clinic za TAYA yangu kwasababu ya KUPIGWA RISASI YA KICHWAโmnajua gharama ngapi naingia kujitibia?
Leo kwasababu ya njaa zangu nianze kukatisha tamaa watanzania wenzangu walioamua kuandamana kunipazia sauti kukataa haya mambo ya KUTEKA NA KUPOTEZA WATANZANIA?
Mimi sina BEI kwenye haya mapambano, bei yangu ni HAKI itendeke, kinyume na hapo NITANYOOKA NA NYIE MPAKA NAKUFA.
Nipo tayari kuishi mafichoni milele.
Nipo tayari kuendelea kuishi kwa mashaka milele.
Nipo tayari kuendelea kuishi kwa tahadhari milele.
Haya yote ambayo yananiumiza leo nipo tayari kuyageuza kuwa maisha yangu ya milele ila najua siku moja USHINDI UNAKUJA.
Kwahiyo ndugu zangu MAANDAMANO YA 7/7 NAYAUNGA MKONO ASILIMIA 200โHII NCHI LAZIMA TUIKOMBOE TUANZE UPYA.
#77Tunatoka
#FreeTunduLissu
#TUTAKUWEPO๐ซต๐พ๐