Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Afya, jijini Accra, Ghana tarehe 22 Julai, 2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Mhe. Samuel Okudzeto Ablakwa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana, tarehe 21 Julai, 2026 kwa ajili ya kushiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Afya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Afya, katika hoteli ya Elisa, jijini Accra, Ghana, tarehe 22 Julai, 2026.
Leo nimeungana na viongozi wengine wa Afrika katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Afya nchini Ghana. Kupitia jukwaa hilo, nimehimiza nchi za Afrika kuongeza uwekezaji wa ndani katika sekta ya afya ili kufikia malengo ya upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, kutokomeza UKIMWI, kuboresha huduma za afya ya uzazi na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza.
Nimeeleza hatua ambazo Tanzania imechukua kuimarisha sekta ya afya, ikiwemo kuwekeza katika viwanda vya dawa na vifaa tiba, kuongeza bajeti ya afya kila mwaka, kutekeleza programu Bima ya Afya kwa Wote na kuboresha miundombinu ya huduma za afya. Maboresho hayo yanawahakikishia wananchi huduma bora za afya wakati wowote, mahali popote.
Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi nyingine na jumuiya za kikanda na kimataifa kuimarisha sekta ya afya na kutafuta suluhisho la pamoja kwa changamoto za afya zinazotukabili.
Strong health systems begin in communities.
By investing in primary health care, we bring essential services closer to every family.
Encouraging to see Zimbabwe strengthening community-based care and advancing towards health for all.
20 Years. One Enduring Vision.
In this special segment, our CEO, Dr. Ellen Mkondya Senkoro, reflects on the Foundation's 20-year journey and the milestones we have achieved together.
🎥 Watch the message🔽
@mohznz1@wizara_afyatz#mkapafoundationat20
Mapema Leo nimembelea Naibu Mwakilishi Mwenzangu wa Norway 🇳🇴 na Kaimu Mwakilishi (Chargée des affaires) Bi. Marita Sørheim-Rensvik hapa Geneva. Mazungumzo yetu yalilenga katika masuala mbalimbali yakiwemo:
Kwanza, Mwaka huu Tanzania 🇹🇿 itakuwa ni moja ya nchi zitakazofanyiwa Universal Periodic Review (UPR), na kama kawaida nchi rafiki hupewa nafasi kuzungumzia Tathmini# husika.
Pili, Tanzania imemteua Jaji Dkt. DEO Nangale kuwa mgombea wa nafasi ya Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC). Uchaguzi huu utafanyika New York Disemba 2026.
Tatu, Tanzania inagombea kwa mara ya Pili nafasi ya Mjumbe wa ITU Council katika Uchaguzi utakaofanyika Doha, Qatar mwisho wa mwaka huu.
Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania 🇹🇿 na Norway🇳🇴 yameanza tangu mwaka 1964 #diplomasiayakimataifa
Benki ya NMB (@NMBTanzania ), imewekeza takribani Dola za Marekani Milioni 100, sawa na Shilingi Bilioni 224, katika mkopo wa pamoja wenye thamani ya Dola Milioni 500 kwa ajili ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita, hatua inayoiweka kuwa Benki kubwa zaidi kutoka Tanzania kushiriki katika ufadhili huo na kuimarisha mchango wake katika maendeleo ya sekta ya madini nchini.
Mkopo huo wa pamoja umeratibiwa na Nedbank Corporate and Investment Banking kwa ajili ya AngloGold Ashanti kupitia Mgodi wa Dhahabu wa Geita.
Ushiriki wa Benki ya NMB unaonesha uwezo unaoongezeka wa taasisi za fedha za ndani kuhamasisha mtaji kwa ajili ya uwekezaji mkubwa wa kimkakati unaochochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya taifa.
Ufadhili huo unaendana na Agenda 2030 ya Benki ya NMB, ambayo imeitambua sekta ya madini kuwa miongoni mwa vichocheo muhimu vya ukuaji wa uchumi. Kupitia uwekezaji huo, benki inachangia kuimarisha mapato ya fedha za kigeni, minyororo ya thamani ya ndani, ajira, ununuzi wa bidhaa na huduma kutoka kwa wazabuni wa ndani pamoja na ushindani wa Tanzania katika uzalishaji na mauzo ya nje.
Hatua hiyo pia inaunga mkono Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kujenga uchumi wenye ushindani, unaojumuisha wananchi wengi zaidi, unaoongozwa na sekta binafsi na unaotegemea ukuaji wa viwanda, biashara na mauzo ya nje.
Mgodi wa Dhahabu wa Geita ni miongoni mwa miradi mikubwa ya madini nchini na wazalishaji wakubwa wa dhahabu barani Afrika. Ufadhili huo utawezesha kuendelea kwa uwekezaji katika mgodi huo na kusaidia kudumisha uzalishaji, mauzo ya nje, ajira, ununuzi wa ndani na thamani ya muda mrefu kwa uchumi wa Tanzania.
Akizungumzia hatua hiyo, Ruth Zaipuna ambaye ni Mkurungenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, alisema muamala huo unaakisi mkakati wa benki wa kuelekeza mtaji katika sekta zenye uwezo mkubwa wa kuleta mageuzi katika uchumi wa Tanzania.
“Muamala huu unaonesha uwezo wa Benki ya NMB kushiriki katika ufadhili mkubwa na wenye miundo ya kitaalamu sambamba na taasisi zinazoongoza za kifedha za kikanda na kimataifa, huku tukihakikisha mtaji wa Tanzania unakuwa sehemu muhimu ya uwekezaji wa kimkakati wa taifa”
#KitengeUpdates
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Afya, jijini Accra, Ghana tarehe 22 Julai, 2026
"Maisha ya binadamu hayakamiliki bila lile shaka moja, jambo moja au tatizo moja linalomuumiza kichwa na ambalo hana majawabu yake ya moja kwa moja au ujasiri wa kulikabili kwa wakati huo na kuamua kuliweka katika mabano ama kuliahirisha. Kila binadamu ana lake. Hauko peke yako!"