Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, SACP Kaster Ngonyani, ametoa taarifa kuhusiana na tukio la kupatikana kwa Edgar Mwakabela (27) maarufu Sativa ambaye alitoweka Jijini Dar es salaam June 23,2024 na kupatikana usiku wa kuamkia leo June 27,2024 katika Hifadhi ya Katavi akiwa na majeraha, ambapo amesema wameanza uchunguzi na msako na watahakikisha wote waliohusika na tukio hilo wanakamatwa.
Akiongea na @AyoTV_ leo June 27,2024, RPC Ngonyani amesema “Edger katamka mwenyewe kwa kinywa chake mwenyewe kwamba yeye ni Mfanyabiashara, Mkristo Mkazi wa Mbezi Dar es salaam, yeye alisema kwamba sijui kapigwa shingoni lakini kumwangalia maeneo ya shingoni hatujaona amejeruhiwa nadhani juu kidogo ya sikio nadhani kitu chenye ncha kali ndio amepigwa nacho na sasa hivi tunasubiri taarifa ya Daktari yeye atatuthibitishia kama ni kitu chenye ncha kali au kitu kingine chochote”
“Taarifa hiyo ipo na huyu Mtu tumemuona yupo Hospitali, tukio limetokea Hifadhi ya Taifa Wilaya ya Mlele ila sasa hivi yupo Hospitali ya Mpimbwe Kibaoni”
“Amepatikana leo nadhani video clip mmeiona ile clip inajielezea vizuri, na sisi tumemuona ila sasa hivi haongei, anaongea kwa tabu sababu ya hizo dawa, nguo zake hazijaloana damu, damu zipo kichwani, tunaendelea kuwatafuta wote waliomfanyia tukio hilo, Daktari atatupa taarifa ameumia sehemu gani na kitu kilichomchoma ila uchunguzi wa kuwatafuta waliofanya tukio hilo unaendelea”
#MillardAyoUPDATES