Nilipokuwa serikalini enzi zile tulihamasisha sana uwekezaji kwenye viwanda. Moja ya sekta za kimkakati ilikuwa sekta ya madawa ya binadamu. **Nilikuwa mjumbe kwenye vikao hivi na nilishiriki vikao kadhaa.
Wadau wengine (hususan wale wa serikali) tuliwapa maelekezo tu na walianza kuwekeza, na wengine walishawishiwa (nafahamu wawekezaji kadhaa walipewa hadi mashamba makubwa bure) ili wawekeze kwenye sekta muhimu za kimkakati, na wengine walihamasishwa kuwekeza.
Eneo lililokuwa linavutia sana ni la madawa (dripu nk). Eneo hili lilipata Wadau kati ya 10 na 20. Promise ikiwa serikali itanunua. Mpaka sasa tuna viwanda 6 vya bidhaa hizi.
Serikali kupitia MSD ilikuwa ikiagiza dripu moja kwa bei ya wastani wa TZS 1,200, kabla ya uwekezaji kufanyika nchini. Uwekezaji ulipofanyika nchini, bei ya dripu ikashuka mpaka bei ya TZS 600/700. Wale waliokuwa wanaagiza dripu kutoka China/India wakashusha bei na kuanza kuuza dripu moja kwa TZS 400! MSD akitangaza tenda anatoa kwa lowest bidder!
Wenye viwanda vyetu vya ndani wamewekeza mabilioni ya pesa na wana mikopo ya uendeshaji (overdraft facilities) kwenye benki za ndani, achilia mbali mikopo ya mtaji ya muda mrefu (term loans) waliyotumia kuwekeza. Maana yake ni kwamba, wasipouza kwa MSD hawawezi kulipa madeni ya benki, siku moja watafunga viwanda. Wakifunga viwanda, kiwango cha mikopo chechefu kitaongezeka, risk ya benki kukopesha inakuwa kubwa, benki zinaogopa kukopesha. Kamwe riba haitokaa ishuke! Wanufaika wa mikopo watakuwa wachache sana. Ili uchumi wetu ukue kiasi cha ku-support maisha ya watu na kutoa ajira ni lazima tukuze uzalishaji na benki zetu zitoe mikopo yenye riba ndogo ili watu wawekeze na wafanye Biashara kwa faida.
Wakifunga viwanda, wanaoagiza kutoka nje watarudisha bei ya dripu moja kwenye TZS 1,200 au zaidi.
Aidha, itakatisha tamaa wajasiriamali wetu kuwekeza kwenye miradi mikubwa na ya kimkakati kama hii, sote tutaishia kubanana kwenye viwanda vya maji na juisi tu! Na pesa ya wavuja jasho wa Tanzania itaendelea kukuza ajira na uchumi wa wenzetu.
Nini kinazuia serikali isitoe kipaumbele/ulinzi kwa wazalishaji hawa? Ambao tuliwaahidi soko? Nafahamu MSD iliteuliwa kuwa muagizaji wa bidhaa hizi kwa niaba ya nchi zote 16 za SADC. Kwa nini kwa kuanzia tu tusiwauzie hizi bidhaa za viwanda vyetu? Oops! Lakini ni ngumu kwa kichwa ambacho hakijawaza kununua kwa ajili yake kuweza kufikiria kununua kwa ajili ya rafiki zake! Forgive me folks.
Hii ni ile hadithi ya watani zangu wazaramo kuwa ‘zilongwa mbali zitendwa mbali’. Hebu ndugu zangu mawaziri @ummymwalimu , @mwigulunchemba1 , @JMakamba na @ViwandaBiashara litazameni hili! Kama kuna kodi za kushushwa ili viwanda vyetu viwe more competitive, shusheni lakini tanueni saizi ya soko(volume) kwa kuuza nje kama nchi na siyo kuwaachia wao, na tutakusanya kodi kubwa zaidi (cf. Laffer curve).
Isiwe hadithi ya viwanda vya mafuta ya kula; upungufu zaidi ya 58%, Lakini wakulima hawalimi alizeti wala pamba ya kutosha! (sisi tunacho kiwanda kikubwa kabisa, kipya) lakini hakuna oil seeds za kutosha.
#HK #Fighter #NjeYaBox
The main reason there is no growth in Africa is that the growth factors are neither funded nor understood; those who want to help Africa should fund our transport systems, electricity, raw material processing, and import substitution.
Why are we being funded to import and hold seminars in the name of capacity building?
I, therefore, challenged my African brothers to think about the hemorrhage of Africa. Our populations are increasing, but our economies are stunted. The IDA should tell us why they are funding the modern slavery of Africans, and we should address issues like why Africa is producing what it does not consume and consuming what it does not produce.
BREAKING: Rihanna IS pregnant, her aides have confirmed. So she did that half-time show while carrying a baby which is pretty damn impressive. Congrats @rihanna 👏👏👏👏#SuperBowl
Thank you @reputationpoll I'm deeply honoured to be listed among Africa's 50 Most Reputable CEOs for 2021. I dedicated this to our esteemed customers and my colleagues at @CRDBBankPlc 🙏🏽
Hivi ndivyo hotuba nzito za rais Obama zilivyokuwa zinaandaliwa. Obama alikuwa anamuita muandishi wake pamoja na mkuu wa mawasiliano kitengo cha Usalama kisha wanakaa wakiwa wame relax,wanafikiri kwa kina na kutoa hotuba bora kabisa.Kwenye kazi wenzetu wanasikiliza sana wataalamu