Nukuu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 14 Novemba, 2025, mkoani Dodoma.
Nikiwa Mama na Mlezi wa Taifa hili, Ninavielekeza vyombo vya Sheria na hasa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuangalia kiwango cha makosa yaliyofanywa na vijana wetu, kwa wale ambao wanaonekana walifuata mkumbo na hawakudhamiria kufanya uhalifu wawafutie makosa yao. Nimewasamehe wote waliofuata mkumbo. #KaziNaUtuTunasongaMbele
Tanzania’s commanding 2–0 victory over Burkina Faso in the opening match of the CHAN 2024 tournament is more than just a sporting triumph—it is a symbol of national confidence, unity, and social progress.
Sports play a crucial role in nation-building. This win, cheered on by a packed Benjamin Mkapa Stadium, reflects how football serves as a unifying force, cutting across social, economic, and regional divides. Thousands of fans waving Tanzanian flags, singing in one voice, and showing unwavering support for Taifa Stars is a powerful display of patriotism and national cohesion.
Such victories have a ripple effect on social wellbeing. They inspire youth, promote discipline, foster national pride, and offer peaceful avenues for expression and identity. For many young Tanzanians, especially those in vulnerable communities, football represents opportunity—both as a career and as a source of hope. It also enhances international recognition and strengthens diplomatic relations through soft power.
Moreover, the presence of senior leaders such as the Prime Minister of Tanzania and the CAF President at the match shows how seriously sports are being embraced at the national policy level. This kind of high-level support reinforces the idea that sports are not merely recreational activities but strategic tools for peace, engagement, and development.
The win against Burkina Faso isn’t just three points on the table—it’s a boost to Tanzania’s spirit. It affirms the country’s capability to compete, to host, and most importantly, to unite. The celebration that followed, including the CHAN Singeli Festival open to all, symbolizes inclusiveness, cultural pride, and social harmony.
In essence, Tanzania's 2–0 start is not just a result—it’s a reflection of national strength, potential, and the enduring power of sports to build a better, more united society. #sisinitanzania #CAF_Online
📍 Dodoma
▪️RAIS DKT. SAMIA: WATANZANIA TUENDELEE KULIOMBEA TAIFA LIDUMU KATIKA AMANI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuwasisitiza Watanzania waendelee kuliombea Taifa ili amani, upendo, ustahimilivu na mshikamano viendelee kudumu nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Jumapili, Novemba 16, 2025) alipowasilisha salamu za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa waumini na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kisasa, Mkoa wa Dodoma.
“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawasalimu sana. Yuko pamoja nanyi, na rai yake kwa Watanzania wote ni kuendeleza maombi kwa Taifa letu kuwa watulivu na kuiombea amani iendelee kudumu.”
Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kulindwa na kuenziwa, kwa sababu pasipo amani, Taifa halitoweza kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuendesha ibada na shughuli nyingine za kijamii.
“Pasipo amani hatuwezi kutekeleza majukumu mengine yoyote, pasipo amani hatuwezi kuendesha ibada. Hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuiombea nchi yetu. Pakiwa na amani tunaweza kutekeleza yale yaliyo katika matarajio yetu, tunaweza hata kutatua yale tunayoyaona kuwa ni magumu.”
Ibada hiyo imeongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma, Dkt. Christian Ndossa ambaye ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania waishi kwa kumtanguliza Mungu mbele na wawe na matumaini kwake na wajiepushe na maovu.
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameambatana na Mwenza wake, Mama Neema Mwigulu Nchemba, katika ibada hiyo.
Viongozi wengine waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge, Daniel Sillo, Mbunge wa Kilolo, Ritha Kabati, Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya, Mbunge wa Viti Maalumu, Balozi Dkt. Pindi Chana, Mbunge wa Itigi, Yohana Msita na Mbunge wa Kalenga, Jackson Kiswaga.
RAIS SAMIA ANAOMBA WATANZANIA TUENDELEE KULIOMBEA TAIFA- DKT. MWIGULU
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, leo tarehe 16 Novemba 2025, amewasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa waumini na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kisasa, Mkoa wa Dodoma.
Amesema Mheshimiwa Rais anaendelea kuwasihi Watanzania kuendelea kuliombea Taifa, ili amani, upendo na ustahimilivu viendelee kudumu nchini.
“Mhe. Rais anawasalimu sana. Yuko pamoja nanyi, na rai yake kwa Watanzania wote ni kuendeleza maombi kwa Taifa letu kuwa watulivu na kuiombea amani iendelee kudumu,” amesema Waziri Mkuu wakati akitoa salamu kwa waumini wa kanisa hilo.
Aidha, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kulindwa na kuenziwa, kwa sababu pasipo amani, haiwezekani kutekeleza majukumu ya kitaifa ama kuendesha ibada na shughuli nyingine za kijamii.
“Ni wajibu wetu wote kuendelea kumtanguliza Mungu na kuiombea nchi yetu ili iendelee kuwa na amani,” amesisitiza.
Mheshimiwa Nchemba aliambatana na Mke wake, Mama Neema Mwigulu Nchemba, katika ibada hiyo.
Ujezi wa skuli bora na ya kisasa umekamilika kisiwani Tumbatu wilaya ya Kaskazini A unguja chini ya uongozi wa Dkt hussein Mwinyi hakika anastahili pongezi kwani amekuwa mkombozi wa kweli kwa wananchi wa Zanzibar #MSLAC#matokeochanya#Katibanasheria#NchiYanguKwanza#SMZ
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa silaha za jadi Mkuki kutoka kwa Mzee Ndijina Ndilanza Ndilito, mwakilishi wa wazee wa Tanzania Bara pamoja na ngao kutoka kwa Bi. Ubwa Hamis Ally mwakilishi wa Wazee wa Zanzibar kama ishara ya kulinda na kuitetea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kuapishwa katika uwanja wa Gwaride, Chamwino Ikulu mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Ahsanteni sana Mkoa wa Mjini Magharibi.
Kama ilivyokuwa kote nilipopita kwa takribani miezi miwili ya mikutano ya kampeni, nimeona upendo, ukarimu, utu, hamasa, shukrani na kiu yenu ya kuendelea kuona matokeo bora zaidi ya kazi ya kuitumikia nchi yetu. Tuendelee kuhamasishana na kukumbushana, ili ifikapo Oktoba 29 sote tujitokeze kwa wingi, tukapige kura kwa amani na utulivu, na tuchague wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kura yako ni Haki yako. Kura yako ya Ndiyo kwa wagombea wa CCM ni kura ya Ndiyo kwa maendeleo, umoja, amani na mshikamano, na kesho iliyo njema zaidi kwa nchi yetu.
Ahsanteni sana. Mwenyezi Mungu awabariki.
Sambamba na mambo mengine, katika hotuba yangu ya kulifungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nimevielekeza vyombo vya sheria hasa Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwafutia makosa vijana na watoto wetu ambao kwa kutokujua, walifanya makosa kwa kufuata mkumbo Oktoba 29 mwaka huu.
Nikiwa Mama na Mlezi, ninawasihi vijana wote kuendelea kulinda amani na mshikamano wa nchi yetu, na hata siku moja msikubali kushawishiwa kuichoma nchi yenu wenyewe.
Alasiri ya leo jijini Dodoma, ambapo kwa baraka za Mwenyezi Mungu, nimehutubia na kufungua rasmi Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kiungio cha Hotuba
Maandishi: https://t.co/s6vSkJW0JA
Video: https://t.co/kiOjleHS4S