Mpaka sasa ni week moja tangu Jeshi la Polisi Tanzania @tanpol limchukue Kuringe Sawere.
Cha ajabu baada ya kumkamata Kuringe sasa hivi wameamua kufuta account ya Kuringe ya hapa X ili Wananchi tusiendelee kusoma spana alizokuwa anampiga Idd Amin Mama.
#FreeKuringeSawere
Maoni Kuhusu Hotuba ya Waziri Mh Kitila Mkumbo @kitilam na Mustakabali wa Vijana Katika Sekta ya Viwanda
Nimemsikiliza kwa umakini mkubwa Waziri wetu Mheshimiwa Kitila Mkumbo, na kwa dhati napenda kumpongeza kwa namna alivyofafanua kwa kina mwelekeo wa wizara yake katika kuchochea uwekezaji nchini. Maelezo yake yameonesha dira, matumaini, na mwelekeo chanya wa kujenga msingi imara wa uchumi wa viwanda.
Ninaenda moja kwa moja kwenye eneo linalochochea fikra za wengi wetu nafasi ya vijana katika ujenzi wa viwanda. Umeweka bayana mpango wa kuanzisha knowledge and skills hubs, upatikanaji wa maeneo ya kufanya kazi, pamoja na mitaji ya kuanza uzalishaji. Hii ni hatua kubwa na ya kihistoria. Hata hivyo, napenda kusisitiza hoja moja muhimu: viwanda hivi viwe na mwelekeo wa kikanda, kama ulivyobainisha kuwa mpango huu utafika kila mkoa. Hili litasaidia kuibua uzalishaji kulingana na rasilimali, soko, na mahitaji ya kila eneo.
Pili, napendekeza tuanze kwa kubaini bidhaa ambazo kwa sasa tunaagiza kutoka nje ilhali zina matumizi ya kila siku, hususan za nyumbani na kilimo. Mfano: sahani, vijiko, sufuria, majembe, mapanga, visu, toroli, pamoja na baadhi ya vifaa vidogo vya umeme kama tochi, kettle, na heater n.k . Ni jambo la aibu kwa taifa lenye watu, malighafi, na soko kubwa kuendelea kuagiza bidhaa hizi kwa wingi kutoka nje. Kwa hali ilivyo sasa, tumetengeneza jamii ya wafanyabiashara wadogo wa reja reja (machinga) badala ya kuwa wazalishaji wa viwandani.
Katika hotuba yako umezungumzia vyema sana juu ya uzalishaji na ajira. Hata hivyo, kwa masikitiko, sikusikia msisitizo wa kulinda masoko ya bidhaa zitakazozalishwa na vijana hawa. Nilitarajia kusikia kauli ya wazi kwamba, kwa mfano, baada ya miaka miwili, Tanzania haitaruhusu tena uingizaji wa baadhi ya bidhaa ambazo tayari zitakuwa zinazalishwa ndani ya nchi hasa kupitia kampuni za vijana.
Ukweli ni huu: huwezi kuhamasisha uzalishaji bila kulinda soko. Haiwezekani vijana wakapewa mikopo, maeneo, na mafunzo, halafu wakati huohuo soko liendelee kufurika bidhaa za nje zinazoshindana na bidhaa zao kwa bei na wingi. Endapo hali hii itaendelea, ni lazima tukiri kwamba ile mikopo haitarudi, viwanda vitaanguka, na mipango mizuri ya serikali itageuka kuwa white elephant.
Mimi binafsi, pamoja na wenzangu, tunajiandaa kuja kwa umakini mkubwa kuichambua fursa hii. Tuna shauku ya dhati ya kuingia kwenye uzalishaji wa bidhaa ambazo kwa sasa tunaagiza kutoka nje hasa kwa kuwa tuna soko kubwa ndani ya Tanzania na katika nchi jirani. Tuko tayari kuwekeza, kuchukua fursa, na kujenga viwanda lakini tunahitaji sera thabiti za kulinda wazalishaji wa ndani, hasa vijana.
Kwa dhati kabisa, tunapongeza mwelekeo wa serikali katika uwekezaji na viwanda. Sasa kilichobaki ni kuunganisha uzalishaji, mitaji, ujuzi, na ulinzi wa soko kwa wakati mmoja. Hapo ndipo ndoto ya uchumi wa viwanda kwa vijana wa Tanzania itakapokuwa ya kweli, si ya maandishi kwenye makaratasi tu.
Asante.
#Pichani
Ni Mwanachama wa CHADEMA anaitwa @kuringechadema jana usiku amechukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni police wakampakia kwenye bajaj na kuondoka nae hadi sasa hatujui alipopelekewa.
#FreeKuringeSawere