Dua na salamu kwa wananchi wa Pasiansi mara baada ya kuwasili mkoani Mwanza mchana wa leo ambapo pamoja na mambo mengine nitahitimisha Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru pamoja Wiki ya Vijana.
@jokateM Hongera sana Dada yangu Kipenzi na Kiongozi wangu Katibu wa UVCCM TAIFA Ndugu @jokateM kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha unatutia vijana nguvu ktk yale tunayoyaendea. Mungu akulinde uishi miaka 100 , Huna Baya Madam JUM
Nikupongeze sana kwa hili, huu ni mfano hai wa kijana anayejitoa kwa ajili ya kufanikisha wengine na hiki ni kielelezo kizuri kuwa tuna Taifa lenye vijana wanaojali kwa dhati ya mioyo yao na ambao wako tayari kujitoa kwa hali na mali kusaidia wengine kujikwamua kiuchumi na kutoka kimaisha. Na hili limekuja wakati muafaka tunavyoelekea kwenye wiki ya vijana kitaifa.
Nitakushika mkono kwa kutoa Milioni 3 ili kwa pamoja tuwasaidie vijana hawa na kuwatoa kwenye vikwazo wanavyokutana navyo.
Kila kijana wa kitanzania aki share ujuzi na mwenzake bila choyo wala hiyana kwa moyo mkunjufu kwa pamoja tunaweza kusonga mbali zaidi.
Utanisaidia kujua unapataje mchango wangu ila kwa kukusaidia pia huwa napatikana Makao Makuu ya UVCCM Taifa, karibu pia nikukabidhi.
Kutoa ni moyo na sio utajiri.
Wasalaam,
JUM 💚
Mapema leo katika Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro niliposhiriki Mkutano Mkuu wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa Mwaka 2024 na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jeshi letu limepiga hatua kubwa katika kipindi cha miaka 60. Nimeendelea kusisitiza kwamba huduma bora za kipolisi kwa umma wa Watanzania zitatokana na kubadilika kifikra, usimamizi wa sheria na matumizi ya TEHAMA. Serikali itaendelea na kazi ya kulijengea uwezo kimiongozo na kibajeti.
Kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia na mali zao ikiwemo haki ya uhai ambayo inalindwa na Katiba yetu. Kote duniani kupokwa kwa haki ya uhai hukemewa na Serikali na kuhakikisha vyombo vyake vya ulinzi na usalama vinafanya uchunguzi na kupata majawabu, kama ambavyo nchi yetu pia inafanya.
Maisha ya mwanadamu yeyote yule yana thamani isiyomithilika. Katika hali yoyote ile uhai wa mwanadamu ni jambo adhimu sana. Uhai wa kila Mtanzania unalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama inavyoeleza katika Ibara ya 14. Hatuhitaji kuelekezwa na mtu yeyote jinsi ya kutekeleza jukumu hili kwani Katiba yetu tayari ina maelekezo ya kutosha.
Kama Amiri Jeshi Mkuu nimeapa kuilinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndani yake ipo haki ya kuishi, na kwamba nitafanya kila linalowezekana kuimarisha ulinzi na uhai wa kila Mtanzania. Katika hili sina muhali. Falsafa yetu ya 4R inalenga kutuleta pamoja zaidi kama Watanzania na si mwanya wa kuvunja sheria zetu na kuifarakanisha nchi yetu.
Huku Serikali na vyombo ya ulinzi na usalama vikiendelea kutekeleza jukumu lake la kulinda haki hii ya uhai, kama jamii kwa sauti moja tuendelee kukemea na kujali damu ya kila Mtanzania kwa uzito ule ule bila kujali ni nani, anatoka wapi, ama kundi gani. Uhai ni uhai. Tukemee pia uovu wa aina zote katika jamii yetu ikiwemo wale wanaopanga kuvuruga amani ya nchi yetu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Moshi Mkoani Kilimanjaro, leo tarehe 17 Septemba 2024.
TAARIFA KWA UMMA
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunalaani na kupinga vikali vitendo vya kikatili na uzalilishaji vilivyofanywa kwa Binti wa Kitanzania.
Tunatoa pia rai jamii iache kusambaza video clip inayoonesha akifanyiwa vitendo hivi vya kinyama.
#KulindaNaKujengaUjamaa