Jiunge katika makala za Daktari @YasiniMustafa kuhusu Ugonjwa wa Kisukari na Ramadhani.
Kuna makundi ya hatari matatu na Leo anazungumzia kundi ambalo LAZIMA lifunge maana funga kwao ni SALAMA.
@wizara_afyatz
Je Mgonjwa wa Kisukari anatakiwa kufunga mwezi wa Ramadhani?
Ungana na Daktari @YasiniMustafa katika wiki hizi kuelekea Ramadhan na mwezi mzima wa Ramadhani akitoa “Darsa” kuhusu Kisukari na Funga ya Ramadhani
DALILI ZA KISUKARI: MATATIZO YA NGOZI! 🩺
⚠️Visunzua, weusi kwenye makwapa na singoni, ngozi iliyokauka na machacha sio dalili za kupuuza.
😣Kama unakutana na dalili hizi, ongea na mtoa huduma wako leo kuhusu vipimo vya kisukari. 🩸🔬 Hatua za mapema ni muhimu!
@wizara_afyatz
“UTI” sugu, “Fangasi” na vidonda sugu (vidonda ndugu😂) sio dalili za kupuuza.
Ongea na mtoa huduma wako kwa vipimo na mashauriano ikiwemo uwezekano wa kuwepo ugonjwa wa Kisukari.
@YasiniMustafa
🔍 DALILI ZA KISUKARI: MAAMBUKIZI NA VIDONDA SUGU ⚠️
🚨 Maambukizi ya mara kwa mara kama UTI sugu, fangasi sehemu za siri 🦠 au vidonda visivyopona kwa muda mrefu 🩹 vinaweza kuwa ishara za kisukari!
⛔ Usitumie dawa kiholela! Zungumza na mtoa huduma wako 🏥
@wizara_afyatz
@CarolNdosi Pole sana
Juhudi za makusudi zinahitajika kuelimisha umma, wagonjwa na watoa huduma kuhusu jgonjwa huu ambao takwimu zinaogofya.
Tumekua na Dr. @YasiniMustafa mgonjwa wa kisukari wa miaka mingo na daktari mbobezi wa kisukari mwanafunzi - na anajitahidi pakubwa katika hili.
SIO KILA KUCHOKA NI KAWAIDA
Uchovu uliopitiliza, usioelezeka au usiokwisha hata baada ya kupumzika SIO KAWAIDA.
Jiunge na @YasiniMustafa akifafanua zaidi.
DALILI ZA KISUKARI - UCHOVU KUPITA KIASI / USIOELEZEKA
🛌😓 Kuchoka baada ya kazi ni kawaida, lakini KUCHOKA KUPITILIZA hata baada ya kupumzika si jambo la kawaida!
🍬⚡ Hii inaweza kuwa dalili ya kisukari, ambapo mwili wako unapata changamoto kutumia sukari kama nishati.
⏳🩺 Ukiona dalili kama hizi, usisubiri! Tembelea mtoa huduma wako wa afya HARAKA kwa uchunguzi na ushauri wa matibabu.
💙✅ Afya yako ni muhimu!
@kisukari_com@samsiria@Nehemiah_mtitu@wizara_afyatz@FrankFedric@BDonD_
Miguu kuwaka moto, kuchomachoma, “kushikwa” misuli mara kwa mara na hata miondoko isiyo ya kawaida vinaweza kuashiria athari za Kisukari kisichodhibitiwa.
Msikilize dakatari @YasiniMustafa akifafanua zaidi.
#DiabetesCare#diabetes#kisukari
Miguu kuwaka moto🔥, kuchomachoma📌, au kuburuzwa🦶 sio kawaida! ⚠️
Dalili hizi zinaweza kuwa ishara ya matatizo ya mishipa ya fahamu yanayosababishwa na kisukari😩
Usikae kimya, chukua hatua mapema! ⏳ Mtembelee mtoa huduma ya afya 🏥 kwa uchunguzi na ushauri wa kitaalamu.
Afya yako ni kipaumbele! 💪❤️🩹”
#kisukari #diabetes #DiabetesCare #afya
@wizara_afyatz@samsiria@Nehemiah_mtitu@rash_mdaki@FrankFedric@kisukari_com@BDonD_
Ni muhimu kumuona daktari wa kinywa na Meno angalau Mara moja kila mwaka hata kama huna dalili zozote za magonjwa ya kinywa na meno.
Ungana nasi @YasiniMustafa akieleza namna kisukari kinaweza kuleta dalili za magonjwa ya kinywa na meno
#kisukari#Diabetes
DALILI ZA KISUKARI: Afya ya Kinywa na Meno🦷💉
Je, unajua kuwa matatizo ya afya ya kinywa na meno yanaweza kuashiria magonjwa kama kisukari? 🤔
Ungana nasi leo tukizungumzia dalili muhimu ambazo ni lazima kufuatiliwa kwa karibu na mtoa huduma wako wa afya! 👩⚕️👨⚕️
Dalili za kufuatilia:
•Maambukizi ya mara kwa mara kwenye fizi 🤕
•Kinywa kukauka kupita kiasi 💧❌
•Vidonda vya mdomoni visivyopona kwa haraka 🩹
•Harufu mbaya ya kinywa isiyoisha 😷
💡 Tip: Tembelea daktari wa meno angalau mara moja kwa mwaka 🗓️ hata kama huna dalili yoyote – ni bora kujikinga kuliko kutibu! ✅
Afya bora ya kinywa ni hatua moja muhimu ya kudhibiti kisukari! 🦷✨
@kisukari_com@FrankFedric@Nehemiah_mtitu@samsiria@BDonD_@KondiBen
#AfyaYaKinywa #Kisukari #DentalHealth #AfyaBora #elimikawikiendi #Diabetes
Ugonjwa wa kisukari unaongoza kwa kusababisha upofu kwa wagonjwa wa kisukari duniani kuliko sababu nyingine yoyote.
Ni muhimu kuzifuatilia kwa makini dalili za matatizo ya macho na kumuhusisha mtoa huduma wako haraka iwezekanavyo.
Ungana na @YasiniMustafa kwenye video hii.
Mwenye Macho Haambiwi Tazama 👁️👓
📌Lakini sisi tunakuambia: Tazama dalili hizi hatari za magonjwa ya macho ambazo zinaweza kuashiria kisukari.
📌Ni muhimu uonapo dalili hizi kukimbia haraka kwa mtoa huduma wako. 🏃♂️💨
📅Hata hivyo tunasisitiza umuhimu wa kumuona daktari wa macho angalau mara moja kila mwaka, hata kama huna dalili zozote.
@wizara_afyatz@kisukari_com@samsiria@Nehemiah_mtitu@BDonD_@FrankFedric
#kisukari #diabetes #SquidGame2 #afya
Usinywe “Alkasusu” au kutumia “vumbi” kabla hujapima Sukari yako.
Msikilize daktari @YasiniMustafa akizungumza nawe kuhusu dalili za kuzingatia na kuhakikisha unazungumza haraka na mtoa huduma wako.
#VunjaUkimya#afya#kisukari#diabetes
💔NGUVU ZA KIUME ❤️🩹NGUVU ZA KIKE🖤
📌Kabla hujanunua “Alkasusu”, “kifurushi” “mazaga” au “vumbi” Tafadhali PIMA SUKARI YAKO.
💃Ewe mlimbwende kuna mambo ya kumwambia “shosti” yako ila sio haya. - KAMA UNAPATA DALILI HIZI - ONGEA NA MTOA HUDUMA WAKO.
📌Jibu linaweza kuwa ni Kisukari kisichodhibitiwa au ambacho hakijatambulika.
#VunjaUkimya Leo - Ongea na mtoa huduma wako.
@wizara_afyatz@kisukari_com@FrankFedric@samsiria@BDonD_@Nehemiah_mtitu
#kisukari #diabetes #afya
DALILI ZA KISUKARI
Macho yako👀, ngozi yako🧴, meno yako🦷, miguu🦵na mikono🖐️ na hata mahusiano yako ya kimapenzi😍 yanaweza kuashiria kisukari.
📌Usingoje dalili kubwa – #VunjaUkimya leo - Ongea na mtoa huduma wako, Pima sukari yako
Jiunge na Daktari @YasiniMustafa
DALILI ZA KISUKARI - SEHEMU YA PILI
Macho yako👀, ngozi yako🧴, meno yako🦷, miguu🦵na mikono🖐️ na hata mahusiano yako ya kimapenzi😍 yanaweza kuashiria kisukari.
📌Usingoje dalili kubwa – #VunjaUkimya leo - Ongea na mtoa huduma wako, Pima sukari yako
Karibu @kisukari_com ujifunze pamoja nasi kuhusu dalili hizi ambazo hutakiwi kuzipuuza.
@wizara_afyatz@samsiria@rkmhealth@FrankFedric@Nehemiah_mtitu
#kisukari #Diabetes #Elimikawikiendi #afya
Macho yako, ngozi yako, hata meno yako hata mahusiano yako ya kimapenzi😍 yanaweza kuashiria kisukari.
Usingoje dalili kubwa – #VunjaUkimya leo - Ongea na mtoa huduma wako, Pima sukari yako 👀🦷
Usikose leo saa Saba Mchana tukijifunza pamoja kuhusu dalili kemkem za kisukari.
“⚠️ Dalili Kuu 4 za Kisukari Usizozipuuzie
💧🚽🍽️⚖️
Ungana nasi leo 📚✨ tukijifunza kwa pamoja kuhusu dalili hizi za hatari.
👉 Tambua dalili mapema, chukua hatua, na linda afya yako kwa muda mrefu! 💪
@wizara_afyatz@BDonD_@FrankFedric@Nehemiah_mtitu@samsiria@nias_nyalada@KondiBen
#UelewaWaKisukari #AfyaBora #LindaAfyaYako #Afya #Kisukari #Diabetes #DiabetesAwareness #ElimikaWikiendi”
Kujikojolea kitandani 🚨 au kuamka mara kwa mara usiku kwenda chooni 🚶♂️🚶♀️ vinaweza kuwa dalili za awali za Kisukari.
Ungana nasi kesho (Jumamosi) asubuhi 🌞 tukichambua dalili 4 kuu za Kisukari na jinsi ya kuzitambua mapema! 🩸💡
@wizara_afyatz@kisukari_com@BDonD_@FrankFedric@samsiria@Nehemiah_mtitu
#Kisukari #DaliliZaKisukari #AfyaYako #JifunzeKuhusuKisukari #DiabetesAwareness #AfyaKwaWote #JaliAfyaYako #Tanzania #ElimuYaAfya”
💊KUNA BAADHI YA DAWA ZINAWEZA KUSABABISHA DAMUSUZIADA NA AINA HII YA KISUKARI.
Ungana na @YasiniMustafa akitukumbusha makundi matano ya dawa ambazo unabidi uwe nazo makini.
#kisukari#diabetes
💊 JE UNAJUA KUNA BAADHI YA DAWA ZINAWEZA KUSABABISHA KISUKARI? 🤔
Baadhi ya dawa, kama steroids, dawa za kupunguza mafuta, au hata baadhi ya dawa za shinikizo la damu, zinaweza kuvuruga viwango vya sukari kwenye damu na kusababisha kisukari kinachosababishwa na dawa. 📈🩺
🌟 Katika video hii, tunakueleza:
✅ Makundi matano ya dawa yanayojulikana kusababisha kisukari kinachosababishwa na dawa?
📌 Tag mtu ambaye anapaswa kufahamu hili.
📲 Usisahau kutufollow na kushare hili na kulisambaza ili kuongeza uelewa. 💙
#kisukari #diabetes #afya
@wizara_afyatz@FrankFedric@samsiria@KondiBen@nias_nyalada@Nehemiah_mtitu
KISUKARI CHA KUZALIWA NACHO - SIYO KISUKARI AINA YA KWANZA
Kuna dhana potofu kwamba Kisukari cha kuzaliwa nacho ni sawa na Kisukari Aina ya Kwanza. Ukweli ni kwamba, hii si sahihi kabisa.
Ungana na @YasiniMustafa akikujuza zaidi
#Kisukari#Diabetes#ElimuYaKisukari#Insulin
KISUKARI CHA KUZALIWA NACHO - SIYO KISUKARI AINA YA KWANZA
Kuna dhana potofu kwamba Kisukari cha kuzaliwa nacho ni sawa na Kisukari Aina ya Kwanza. Ukweli ni kwamba, hii si sahihi kabisa. Kisukari cha vichanga ni aina adimu sana ya Kisukari na ni tofauti kabisa na Kisukari Aina ya Kwanza.
Tofauti kuu? Kisukari cha kuzaliwa nacho kinaweza kupona kabisa, na mara nyingi kinaweza kudhibitiwa kwa kutumia dawa za vidonge badala ya insulin.
Ni wakati wa kuondoa uzushi huu na kujifunza kwa usahihi kuhusu aina hii nadra ya Kisukari. Ungana nasi katika harakati za kutoa elimu na kuleta ufahamu wa kweli!
@samsiria@Nehemiah_mtitu@wizara_afyatz@FrankFedric
#Kisukari #Diabetes #ElimuYaKisukari #Insulin