We are formal Registered NGO with directed efforts towards providing every rural woman in Tanzania with access to prenatal and postnatal healthcare services.
LIFE CARE FOUNDATION imeshirikina na mashirika mengine katika kutoa Huduma kwenye kambi ya matibabu bure kwa magonjwa yasiyoambukiza kwenye viwanja vya mnada wa zamani Gezaulole-Kigamboni, Dar es Salaam.
#ElimuYaAfya#lifecareTz@wizara_afyatz
https://t.co/oej8aG37a9
Today’s more than 1.1b girls are poised to take on the future. Every day, girls are breaking boundaries and barriers, tackling issues like child marriage, education inequality, violence, climate justice, and inequitable access to healthcare. Girls are proving they are unstoppable
Today is #WorldSuicidePreventionDay 💙
Did you know that #Africa has the highest suicide rate in the world? Some people believe that #suicide is 'not an African problem'. But the facts show otherwise👇🏾
IYD2023, This global celebration serves as a platform to raise awareness among young individuals about the myriad challenges they face and empower them with the tools and confidence to conquer these challenges.
#IYD2023#YouthLead#YouthDay
Read More: https://t.co/vzuRU0mMqI
Vijana OYYYEEEE 🤩
Youth are the backbone of #Tanzania and continue to use their voices to spark action!
No matter who they are or where they are from, every young person deserves to live in a world where they can reach their fullest potential!
Happy International #YouthDay💙
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameitaka Taasisi ya Mashirikia Yasiyo ya Kiserikali TANGO kusaidia wanachama wake katika maeneo ambayo yanawakwamisha kuendesha shughuli zao vizuri hasa matumizi ya takwimu.
Breastmilk is a baby’s first vaccine 💙
Breastfeeding, started within the first hour of birth, gives babies the best and only nutrition they need in their first six months of life, helping to prevent illnesses and boosting their brain development.
#KwaKilaMtoto, a healthy start!
Life Care Foundation imehudhuria jukwaa la mwaka la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NACONGO)M Mkoani Dar es salaam tarehe 28 – 29 Julai, 2023. Mkutano ulifanyika katika Ukumbi wa Maktaba – UDSM. Mgeni rasmi akiwa Mkuu wa mkoa Mhe Albert J. Chalamila.
@nacongotz@lifecaretz
WAZIRI MKUU APONGEZA UBORESHAJI HUDUMA MUHIMBILI
Na. Mwandishi Wetu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameupongeza Uongozi wa @MuhimbiliTaifa kwa kuboresha huduma na mazingira ya Hospitali hiyo.
Mhe. Majaliwa ameyasema hayo leo alipotembelea Hospitali hiyo kumjulia hali ndugu yake aliyelazwa hapo ambaye anaendelea vizuri na kupata fursa ya kuwasalimia wagonjwa wengine.
"Nimefurahishwa sana jinsi mlivyoboresha huduma, wakati napita kusalimia baadhi ya wagonjwa wamenieleza kuridhishwa na huduma wanazopatiwa, hii inatia moyo sana.
"Nimefurahishwa na uboreshaji wa mwonekano wa Hospitali, mazingira, majengo na hii ndio Hospitali ya Taifa Muhimbili tunayoitaka" amesema Mhe. Majaliwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amemhakikishia Mhe. Majaliwa kuwa Menejimenti itaendelea kuimarisha huduma zake katika nyanja mbalimbali.
Wito wangu: Pimeni Vinasaba vya Sikoseli kabla ya Kuoana au Kuanzisha Familia.
----
Sikoseli (Seli Mundu) ni ugonjwa wa kurithi unaoathiri chembechembe nyekundu za damu. Ugonjwa huu husababishwa na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi wote wawili. Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 15 hadi 20 ya watanzania wana vinasaba vya ugonjwa huu hivyo wana uwezekano wa kupata watoto wenye ugonjwa wa Sikoseli iwapo watakuwa na wenza wenye vinasaba vya Sikoseli.
Nchini Tanzania inakadiriwa kuwa kila mwaka takribani watoto 11,000 huzaliwa na ugonjwa wa Sikoseli. Takwimu hizi zinaifanya Tanzania kuwa nchi ya 5 duniani yenye wagonjwa wengi ikitanguliwa na Nigeria, India, DRC Congo na Angola.
Sikoseli sio ugonjwa wa kupuuza! Watoto wenye ugonjwa huu mara nyingi hupata maambukizi ya bacteria, kupata maumivu kwenye mifupa (misuli) na kupungukiwa damu mara kwa mara. Hali hii huathiri ukuaji wao na maendeleo yao shuleni kwa kuwa wanashindwa kuhudhuria masomo mara kwa mara kutokana na kuumwa. Aidha watoto wengi wanaozaliwa na Sikoseli (hadi asilimia 70) yaani watoto 7 kati ya 100 hufariki dunia kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano!
Serikali imeendelea kuboresha huduma za Wagonjwa wa Sikoseli kwa kufanya yafuatayo:-
1. kuanzisha Klinic za Sikoseli katika Hospitali za Rufaa za Mikoa na baadhi ya Hospitali za Halmashauri na Vituo vya Afya. Mwelekeo wetu ni kuhakikisha Klinic za Sikoseli zinaanzishwa katika Hospitali zote za Halmashauri na Vituo vyote vya Afya nchi nzima. Lengo ni kuimarisha huduma za ugunduzi wa mapema kwa watoto wachanga
2. Kuendelea kutoa Elimu kwa jamii kuhusu Ugonjwa wa Sikoseli ambapo tutaongeza nguvu ya kutoa Elimu kwa Vijana kuhusu umuhimu wa kupima vinasaba vya Sikoseli kabla ya kuoana au kuanzisha familia ili kuvunja mduara wa ugonjwa huu.
3. Kuimarisha upatikanaji wa Dawa ya Hydroxurea ambapo mwaka 2017 ni asilimia 1 tu ya watoto wenye sikoseli ndio walipata dawa hii kupitia bima ya NHIF. Hivi sasa watoto wanaopata dawa ya hyrodroxurea kupitia NHIF imefikia asilimia 32. Lengo letu ni kuhakikisha watoto wote wenye Sikoseli wanapata dawa hii bila kikwazo.
4. Kuimarisha huduma za kubadilisha damu (Exchange blood transfusion) kwa wagonjwa wa Sikoseli wenye uhitaji.
5. Kuanzisha huduma za kupandikiza Uloto (Bonne marrow transplant) kwa watoto wenye sikoseli katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ambapo mwaka huu 2023 watoto watatu wamepandikizwa uloto. Hii ni hatua nzuri kuelekea kupatikana kwa tiba ya kudumu kwa wagonjwa wa Sikoseli. Mwaka 2023/24 Serikali chini ya Rais @SuluhuSamia itagharamia watoto 20 kupandikizwa Uloto
6. Mafunzo na Tafiti ili kuboresha huduma na kupata takwimu na maamuzi ya kisera yenye udhibitisho wa kisayansi unaoendana na mahitaji ya nchi yetu ili kuwa na kizazi kisichokuwa na ugonjwa wa Sikoseli.
#SikoSeli #_SeliMundu #SickleCellDiseaseDay2023