@chapanombombwi@Sativa255 Duuuu shambani ni mikazo, ukifuata maelezo ya kwenye mtandao,utadhani kesho uta amka tajiri kupitia shamba ,njoo sasa kwenye vitendo utajuta.
@WakiliTv Mimi nadhani kuwahoji watu ambayo,elimi Yao iko chini mnatukoaea sana,hivi hii katiba tuliyonayo nani alieleweshwa na akafauru kwa tz yetu ?na huyu anataka watu waelimishwe kwa kiwango Gani?ili hiyo katb mpya ipatikane,KATIBA MPYA NI SASA.
Ni muhimu wananchi na wanachama wa vyama vya siasa, ikiwemo vyama vyenye wafuasi wengi kama CHADEMA, kuelewa kuwa nguvu ya mabadiliko pia inategemea uwezo wetu wa kuchangia na kujitolea kifedha kwa shughuli za pamoja. Kwa uhalisia, tuna uwezo mkubwa wa kuchangisha fedha ikiwa tutakuwa na nidhamu ktk wajibu huu.
Tatizo kubwa tulilonalo si ukosefu wa fedha pekee, bali ni changamoto ya mtazamo (mindset) na vipaumbele vyetu. Tunaweza kuchangisha mamilioni ya shilingi kwa sherehe na shughuli za kifahari, lakini tunashindwa kuchangia kiasi kidogo kwa ajili ya kusaidia wakati mwingine wagonjwa au kuimarisha harakati za haki na maendeleo.
Hili linaonyesha wazi kuwa changamoto yetu kubwa ni fikra zetu zaidi kuliko hata masuala ya kikatiba. Tukibadilisha mtazamo wetu, tutaweza kujenga nguvu ya pamoja inayoweza kuleta mabadiliko ya kweli.
Tunaomba kuwe na moyo wa kujitolea kifedha kwa wote wanaotaka kuona haki, maendeleo na demokrasia ya kweli nchini. Inaumiza na kutesa nafsi sana kuomba pesa kwa jamii ambayo inapaswa kujua kuwa kuendesha vyama vya siasa kama CHADEMA ni wajibu wao. Hapa , usiandike Mh tuko pamoja. Changa pesa Mangi !!
Si kila mzungu mkoloni,si kila mwafrika Rafiki,wakoloni wengi ni weusi kwenye mataifa yao wakiongoza waafrika wenzao, Bad enough wanatesa,wanakili,wanahati,wanatesa,
Kuliko mkoloni, Mbaya zaidi wanajipa wealth
#TANZANIA: CHADEMA MJIAMINI, WATANZANIA WANAIMANI NA NYIE, MSIPIGE MAGOTI - MARIA SARUNGI
Mwanaharakati machachali nchini Tanzania, @MariaSTsehai leo Aprili 09, 2026 akiongea katika mjadala wa kidigitali uliyoandaliwa na chama cha @ChademaTZ2 katika siku 365 tangu kukamatwa Mwenyekiti wao wa Taifa, @TunduALissu amesema kwa sasa CHADEMA iko imara sana na Watanzania wanaimani kubwa na chama hicho.
Aidha, Maria amewaeleza CHADEMA kuwa wasikate tamaa kwa kuondokewa na wanachama wao walioamua kukimbia mapambano ya kudai haki na kuunga juhudi.
Maria amesema CHADEMA hii inawanyima usingizi watawala na ndio maana Lissu amewekwa ndani mpaka muda huu na kufungiwa kufanya siasa kwa chama hicho, amewasihi wasirudi nyuma wala kuipigia magoti serikali kwani Watanzania wana imani kubwa na chama hicho.
Zaidi: https://t.co/PpwQJKWD04
Mwaka jana tarehe 25/7 2025 nilikwenda kumtembelea Mh Bwege hospitalin, Taasisi ya Mifupa Moi.
Japo nimekaa na mh Bwege bungeni na kwenye kambi ya upinzani sikuwahi kuwa karibu nae kama kipindi hiki.
Katika kipindi hiki kifupi nilijifunza na kumjua mh Bwege kama.
1. Mtu anaeipenda Nchi yetu na watu wake kwa moyo wote. Katika hali ya ugonjwa aliokuwa nao, watu wengine huacha kabisa hata kufuatilia siasa, kukata tamaa na kuona hata mambo yakiharibika hayamhusu.
2. Mtu mwenye msimamo wa hali ya juu mno, kuna watu walijaribu kumpa msaada wa matibabu lakini kama vile wanaweka masharti, akawambia niko tayari kwa msaada ila siko tayari kuyumbisha msimamo wangu.
3. Mtu aliependa Mageuzi kwa dhati, hata kabla ya kwenda kumuona Hospitalin, alinipigia simu na kuonesha kuwa amefurahishwa sana na uongozi mpya wa Chama chetu chini ya Mwenyekiti wetu Lissu… na akasema ana imani kubwa na Mhe Lissu na atajiunga na chama kama ishara ya kumuunga mkono.
4. Wiki moja iliyopita alianza opareshini ya kusimika Chadema Kusini, katika hali yake ya ugonjwa. Alitoa gari lake bure na mafuta, akawapigia viongozi kule na kuwakabidhi kwa vijana wa Chadema waliokua wanaendesha oparesheni. Kwa wiki moja maelfu ya watu wamehama vyama vingine kule na kujiunga Chadema.
5. Alijua Siasa hasa ground, Spika wa zamani wa bunge la Marekani Thomas P. “Tip” O’Neill Jr, alipata kusema “all politics is local” Siasa ni mahalia, Ndio maana ukienda Tarime utazungumza kuhusu dhahabu na ukienda kusini utazungumza korosho… Bwege alijua sana Siasa mahalia .. ndio maana ni mbunge wa miaka 10 wa upinzani.
6. Aliipenda kusini kwa dhati, aliipigania na alipigania maendeleo ya kusini na kusini ilimpenda sana Bwege.
7. Mfuatiliaji na anaejua watu kwa majina na meneo wanayokaa, wakati wa watu kuhamia Chadema ananipa namba na kuniambia ongea na huyu, yuko Namangaya , ongea na huyu yuko Kivinje, baadae anafuatilia kuuliza kama umeongea nae.
Alijiunga na Chama chetu, tukasubiri mikutano ifunguliwe tumpokee kwa heshima aliyostahili.. Mungu amemchukua kabla ya hiyo azma yake kupokelewa mbele ya maelfu ya watu.
Pumzika kwa amani kaka gwiji wa siasa za kusini.
TAARIFA KWA UMMA
Sisi mawakili Maduhu William,, Nashon Nkungu na Paul Kisabo tumefungua shauri la Kikatiba ambalo ni Shauri No. 7300dhidi ya Kamishina Jenerali wa Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Shauri hili limefunguliwa katika mahakama kuu masijala kuu ya Dodoma.
Tumefungua shauri hili kuhoji uhalali wa Jeshi la Magereza kuzuia na kuwawekea,,,vingiziti au vikwazo mawakili pale wanapotembelea Magereza kwa ajili ya mashauriano ya kisheria na wateja wao ambao ama ni wafungwa au Mahabusu.
Shauri hili litatajwa kwa mara ya kwanza tarehe 14 Aprili 2026 mbele ya jopo la Majaji watatu ambao ni Mruma,, Dr. Rumisha na Dr. Longopa, JJJ's.
Tutaipigania Heshima na hadhi ya uwakili usiku na mchana na bila kuchoka.
Wakili Maduhu
Serikali ya Uingereza imeifikisha Tanzania katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC), ikitaka kufanyika kwa uchunguzi huru na wa kina kufuatia kile ilichokiita "ukatili wa kushtua" uliotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025, ikiwemo tuhuma za mauaji ya kinyume cha sheria na miili ya wahanga kufichwa.
Hoja hiyo imewasilishwa na Balozi wa Haki za Binadamu wa Uingereza, Eleanor Sanders, wakati wa mdahalo mkuu wa 61 wa Baraza hilo jijini Geneva, Uswizi Machi 2, 2026. Uingereza imetumia jukwaa hilo la kidiplomasia kuishinikiza Tanzania kutoa majibu juu ya mfululizo wa matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu yaliyoripotiwa nchini humo.
Katika tamko hilo, Balozi Sanders ameweka wazi kuwa Uingereza ina taarifa na ushahidi wa matukio ya kusikitisha yaliyojiri kufuatia mchakato wa uchaguzi, jambo ambalo limeutia doa utawala wa sheria na demokrasia nchini.
"Lazima kuwepo na uchunguzi huru, wa wazi na jumuishi wa matukio haya ili kuhakikisha uwajibikaji na kwamba uhuru wa msingi na haki za kikatiba za Watanzania wote zinalindwa," amesisitiza Balozi Sanders.
Hatua hii ya Uingereza ‘kuishitaki’ Tanzania mbele ya Baraza la Haki za Binadamu wakati ambao Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, iliyoundwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikiendelea kukutana na kufanya mahojiano na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa sasa, wastaafu, na wadau mbalimbali ili kukusanya taarifa na ushauri wa kitaalamu juu ya kile kilichotokea.
Mbali na kuisaka haki nchini Tanzania, Uingereza imetumia fursa hiyo kukemea ukiukwaji wa haki maeneo mengine ikiwemo Gaza na Ukingo wa Magharibi ikiitaka Israel kuruhusu misaada na kusitisha ujenzi wa makazi; China, ikitaka kuachiliwa kwa watu waliowekwa kizuizini kiholela Xinjiang na kukomeshwa kwa kazi za suluba; na Ukraine, ikiendelea kuunga mkono mamlaka ya nchi hiyo dhidi ya uvamizi wa Urusi.