Ukimziba jino Mtanzania na Temporary Material akala vizuri na maumivu yakaisha, kurudi second visit kwa ajili ya Permanent filling labda umfate na polisi 😂🙌
Hivi @SuluhuSamia ? Si wewe mwenyewe ulisema hukusoma uliishia form iv na ukafeli? Sasa kwanini unafikiri kupambana na Lissu? Si ukapambane na vilaza wenzako munaouwa watu? ACHANA NA LISSU SIO SAIZI YAKO
Wewe unajulikana Dunia nzima kwamba ni MUUWAJI
🚨BREAKING NEWS
TAARIFA NJEMA KWA WATANZANIA.
Kamati za mambo ya nje na ya maendeleo wamepiga kura na kupitisha azimio la kuitaka tume ya Umoja wa Ulaya (EU commission) isitishe msaada kwa serikali ya Tanzania.
Kamati zimepitisha kwa kura za KISHINDO ndiyo ni kura 81, kura moja ya hapana na kura 4 kuharibika (hawakupiga kura).
Huu ni USHINDI mkubwa kwa watanzania wote wapenda HAKI. Huwezi kuua maelfu ya wananchi alafu ukaendelea kutawala.
Mungu wetu ni mwema!
Sasa azimio linaenda kupigiwa kura na Bunge zima la Ulaya - ikipita hapo ndio KWISHA HABARI YAO.
MWAGA MOTO MWINGI KAMA MADRAGON WANANGU🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
REPOST 200
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Kwa mujibu wa Jaji Kiande, Master Tindwa alipigwa risasi akauwawa akiwa nyumbani kwake sababu alilipwa na akapewa mafunzo ya kuandamana.
Keep resting in peace, Master!
What a sad day for us!!
MPANGO NA SHERIA YEYOTE INAYOTUNGWA KWANJIA NA SABABU ZA KIBAGUZI NI UVUNJAJI WA SHERIA ,KATIBA NA MIKATABA YA KIMATAIFA.
Huwezi kuzungumzia kupatanisha kampuni mbili za kigeni ili zibaki kufaidi Ngorongoro halafu wakati huohuo ufikirie eti kutafuta suluhisho la kisheria kwa kuwaondoa wamasai Ngorongoro.
Hiyo itakuwa sheria ya kibaguzi na Kikaburu.
Hata ukitunga sheria itakuwa sheria haramu ya kibaguzi nankikaburu inayokiuka Haki ya Wamasai katika Ardhi yao.
Kipaumbele cha kwanza kwa ngorongoro ni kulinda haki na hadhi ya Wamasai katika Ardhi yao ya Asili.
Tunaweza kuweka utaratibu bora wa Ufugaji na Matumizi rafiki ya Ardhi. Ngorongoro is for Maasai .Siyo kwa ajili ya Mahotel na Wawindaji wa Kigeni.
Haki,Ukweli na Uwajibikaji vitaliponya Taifa.
BAK Mwabukusi.
Mwenye hii BAJAJI nitafutieni niipige full tank kisha aniambie malengo ya week kwa boss ngapi nayo nilipie.
Hiki alichofanya ninzaidi ya ushujaa. Pesa yangu ya ushindi wa treni la odds 83 zinanze kwenda kwa wanangu sasa.
NITAFUTIENI HUYU SHUJAA.
REPOST 200
#UPDATES_KUTOKA_MAHAKAMA_KUU
Muda huu ni saa sita nayo dakika 17 kesi ya mchongo ya uhaini dhidi ya Mhe. Lissu bado haijaanza na Mawakili wa Serikali hawaonekani.
Tetesi kutoka kwa msiri wetu zinasema wanapigiwa simu hawapokei na wengine wamezima simu.
Mawakili wa Serikali wamechimba. Majaji na Mahakama imeachwa solemba, haya mambo yanashangaza kabisa.
Jamhuri kama hii kesi imewashinda waiondoe au wakae na Lissu Gerezani bila kesi kuendelea tujue moja maana hapo awali leo Walisema wanahitaji lisaa limoja kutafakari muda huu yamefika masaa mawili. Hawaonekani na hawajulikani walipo.
Unaambiwa hakuna anayefanikiwa kuwapata Mawakili wa Serikali na hawajulikani wameenda wapi?
Sijui ndio kufuata maagizo kutoka juu.😂😂😂😂
Haya ni maajabu na ni mambo yanayoshangaza sana.
MWAGA MOTO KAMA DRAGON WANANGU.🔥🔥🔥🔥
REPOST 200
TUTAKUWEPO🫵🏻😎
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 221
Jaji Ndunguru ameteta sana na wenzake kama dakika 10 hivi.
Sasa anawasha kipaza sauti.
Anasema yafuatayo: tumesikiliza hoja zote hivyo vijembe vyenu msivilete.
Sasa mshitakiwa alisema anapingamizi na tukasema upande wa mashitaka walete open statement ili Mahakama iamue.
Mambo mengine ya kwamba imeambatana na nini na nini kipo wapi hayo sio mambo ya msingi.
Mshitakiwa endelea sasa, hawa upande wa mashitaka mmemaliza hapo, presentation ya notice na justification ya notice.
Watu wanacheka hapa 😂😂😂😂
Nafikiri mpaka sasa Katuga ameelewa nani ni Bingwa wa Sheria.
Mhe. Lissu amasimam, sasa Waheshimiwa Majaji kwa kuanzia niseme hivi waliyosema wenzetu.
1. Upande wa mashitaka unasema notice yao haileti shahidi mpya bali inaongezea ushahidi wa shahidi ambae ushahidi wake ulishatolewa kwenye committal.
2. Wamemtaja huyo shahidi kwa jina kabisa.
3. Wamesema wameleta viambatanisho vinavyotakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 308(2) cha CPA.
Sasa baada ya kusema twende kifungu kinavyosema cha 308
A witness whose statement or evidence was not read during committal......
Kifungu kinasema shahidi mpya.
Kinachotakiwa kuletwa ni jina la shahidi wa ziada, huyu ndio anaweza kutolewa notice.
Wamesema wenyewe hawaleti shahidi mpya bali wanaongezea ushahidi wa shahidi aliyepo.
Sasa huyu shahidi ambae tayari yupo na wamemtaja huyo Shahidi ACP Amin Mahamba.
Sasa waheshimiwa Majaji naomba niwaalike kwenye ukurasa wa 90 na 91 na 99 na 100 wa record ya committal proceedings na ukurasa wa 134 wa record ya Mahakama hii ambapo upande wa mashitaka ulitaja majina ya mashahidi wao.
Huyo Amin Mahamba yupo na mimi maelezo yake ninayo hapa sasa Waheshimiwa majaji hiyo notice inaingiaje mahakamani.
Ushahidi wake tayari upo mahakamani na notice inatakiwa iwe ya shahidi ambae maelezo yake hayakusomwa mahakamani.
Hii sio notice ya additional witness ni notice ya additional evidence ambayo haipo kisheria nimetafuta CPA yote hicho wanachosema hakipo.
Jambo lingine ni kwamba wanaleta ushahidi wa mtu aliyefanya upelelezi wa matukio ya uchaguzi mkuu 2025 sasa Majaji matukio ya tukio ya tarehe 29/10 mimi tayari niko mahabusu
Anasimama Katuga anasema tunapinga anaanza kujadili ushahidi wetu kama mtakubali ni sawa tu.
Lissu: Si ndio kayaleta haya mwenyewe wanakatazaje nisiyazungumzie?
Jaji Ndunguru: Mshitakiwa endelea.
Lissu: amesema mwenyewe kwa mdomo wake hapa Mahakamani. Nilimwambia asibwabwaje sana. Akang'ang'ania kuanza kusema mambo ya tarehe 29/10 ndio maana na mimi nasema hayo ya tarehe 29 mimi nilikuwa jela.
Wanafikiri hayo yatawasaidia maana wanataka kugeuza mashitaka kwa kuleta mambo ya tarehe 29/10/2026. They can not amend the information through the back door. Kama mnataka ku amend information nendeni kwenye kifungu cha 294 ch CPA.
Hiyo wanayoiita notice haipo kisheria. Haitambuliki. Hiyo notice muifutilie mbali. Yaani notice na yaliyomo.
Na mwisho, Wahe. Majaji hiyo notice ikiachwa ikawa sehemu ya record ya Mahakama itafungua sanduku la pandora ambalo lina kila aina ya mambo mabaya ambayo sidhani kama itaweza kushughulika mambo hayo.
Wanataka tuzungumze mambo ya October 29 mtakuwa mmefungulia balaa na isije ikawa shida. Mkifungua huo mlango tutaenda huko. Tutazungumzia mauaji ya kimbali na tutaulizana nani aliyeua watanzania. Hii kitu haina mashiko. Are they ready? Mimi niko tayari. Isiruhusiwe ikiruhusiwa niko tayari?
Jaji tafadhali naomba tusiende huko.
Katuga aliambiwa na Lissu kuwa huwezi kunifundisha Sheria akakataaa. Baada ya Lissu kumaliza hapa. Katuga amekuwa mdogo sana yani. Ni kama anataka kulia.
Katuga anasimama anasema napaswa kufanya nini reply au rejoinder
Mhe. Lissu anasema fanyeni reply halafu mimi ndio nitakuja kumaliza.
Wanakubaliana hivyo.
Part 222 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
ASP Geofrey Lutufye: Nilikuta vijana wakila njama za kuzuia uchaguzi Mkuu 2025.
Jaji anasema umesema Walikuwa wanakula nini?
ASP Geofrey Lutufye: Walikuwa wanazungumzia uchaguzi mkuu wa 2025.
Jaji: Kumbe walikuwa wanazungumzia sio kula tena?
Watu wanacheka.😂😂
Repost...
#UpdatesKesiYaRasilimali
Mhe. Jaji Mwanga ameita Kesi ya Issa Mohamed na Wenzake Vs Bodi ya Udhamini ya Chadema Ikafanyikie Chamber Court badala ya Ukumbi wa Wazi, wanaotuhusiwa kuingia Chamber Court ni viongozi wakuu wa chama tu.
Kwanini Kesi yenye Public Interest Inasikilizwa Chamber, sijui ni kwa masilahi ya nani?
Hofu ya nini?
Tundu A.M Lissu hakuwa na shida na chakula mchana ule. Lakini kama ilivyo kawaida yake, ameumbwa katika kupigania haki za wengine, msingi wa maneno yake ulikuwa ni ulimwengu ufahamu kwamba mahabusu/wafungwa wakifikishwa Mahakamani kwa ajili ya kesi zao, wanatakiwa kushinda na njaa/bila kula chakula hadi watakaporudishwa gerezani wakutane na ugali baridi na maharage yaliyosimama kama msumari. Kumbuka, wameondoka gerezani saa mbili asubuhi, msosi wa jela haujaiva, wanarudi jioni/usiku. Literally, TAL anasema, magereza siyo kaburi na huo ni utaratibu wa kikoloni ambao unatakiwa kubadilishwa. Mahakamani zipo canteen, au kama hawataki, ndugu za mahabusu/wafungwa waruhusiwe kuleta chakula siku ya kesi.