Dhahabu ya taifa si “pesa iliyoko mezani,” bali kinga ya taifa, inadumisha thamani ya sarafu, inakabiliana na mfumuko wa bei, na inavutia uwekezaji. Kuiondoa kutoka hazina au kuuza zote mara moja ni kujipiga makofi. Ni hatari isiyo na kifani. Hatari hii si ya nadharia tu, bali ni kielelezo cha kupoteza hifadhi ya taifa, kushuka kwa imani ya wawekezaji, na kuathirika kwa uchumi kwa muda mrefu.
Dhahabu ni kinga, si suluhisho la haraka. Kulinda hazina hii ni kulinda uchumi wa taifa na mustakabali wake. Tukipuuza hili, hatari ya kuanguka kwa uchumi ni kubwa na madhara yake yatadumu vizazi.
Mtakumbuka huu UJUMBE , tunaelekea kuwa kama ZIMBABWE.