@ItsKamala Unaenda kanisani inageuka kikoba Hadi kelo ,Badala ya kusali na kutuliza akili unawaza kulipa Madeni na mashindano ya kutoa sadaka
-Sadaka ya Elimu
-Sadaka ya Ujenzi
-Sadaka ya Adam na Hawa
-Ahadi
-Sadaka kawaida
DALALI akamlaghai NGOSHA ili ajiunge na kandarasi yake ya UDALALI. Akamdanganya asigombee ubunge huko kwao, agombee Urais na kwamba atashinda kwa kishindo. Halafu usiku anageuka na kumdhibiti kinagaubaga ili aenguliwe. DALALI anavaa jezi nyingi sana uwanjani. DALALI amehakikisha NGOSHA anashindwa mahakamani. DALALI akaamua kumnadi mgombea wa veggies kwa vipeperushi mtaani. DALALI anachukia kila kitu kinachofanywa na UPINZANI halisi. Nafikiri, mbogamboga wakimshughulikia kiulalo-ulalo, itakuwa sherehe. Tutapiga mvinyo kuwaenzi wahenga.
Unajiuliza ni mwizi? Hapana! Ana silaha? Hapana! Sasa una jiuliza kwanini itumike nguvu yote ile kwa mtu mmoja ambae anaweza dhibitiwa na watu wawili/watatu bila kutumia silaha?
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 19
Anaendelea Mhe. Lissu
Kupanga njama ya kuzuia uchaguzi sio kosa la jinai kwa sheria yoyote ya Tanzania.
Washemiwa majaji kwenye ukurusa wa 7 wa sheria ya uchaguzi ya 2024 hakuna kosa hata moja la kuzuia uchaguzi.
Vile vile kwenye sheria ya kanuni za adhabu (penal code)
Nje ya kifungu cha 39 kuna vifungu vyenye sura ya uhaini uhaini, Kifungu cha 40,41,45,46,47, 48 Hakuna lolote linaitwa kuzuia uchaguzi.
Anaendelea Mhe. Lissu
Ili Kosa liwepo lazima kuwe na manifestation, matendo yaonekane wazi, sasa Waheshimiwa ukisoma hiyo hati ya mashtaka yangu inataka kusema MANENO YALIYOTAMKWA NI KITENDO?
Nimeandika kwa herufi kubwa maana yeye mwenyewe kaongea kwa msisitizo sana.
Kwenye kesi ya Gandi Jaji alisema maneno matupu hayawi Uhaini isipokuwa hayo MANENO yawe yanaelezea nia ya uhaini.
'Tutahamasisha uhaini, tutavuruga uchaguzi' yanakuwaje uhaini?
Kwenye kesi hiyo Jaji Nyalali alisema MANENO ya mtu mmoja hayatengenezi uhaini na Mimi Mh. Jaji nimeshtakiwa peke yangu.
Maneno yangu hayawezi kuwa uhaini.
Mhe. Jaji, haya maneno yote ninayoambiwa nimesema yanatengeneza Kosa lolote?
Inasikika minong’ono ya watu ni kama kuna kamzozo kanaendelea upande wa juu kule ghorafani ila sijui issue nini, tutajua baada ya kesi.
Anaendelea Mhe.
Je tutahamasisha uasi ni uhaini?
Mheshimiwa Jaji nina kamusi ya BAKITA.
Tuangalie tafsiri kwa mujibu wa Kamusi hii
(a) 'Hamasisha' tia watu msukumo wa kufanya jambo fulani.
(b) Uasi ni KITENDO Cha Uvunjaji wa Sheria kinachofanywa na kikundi Cha watu kwa lengo la kubadili mfumo wa nchi yao na maana ya pili UASI ni Kitendo cha kuwapinga wenye mamlaka au kupinga Sheria na taratibu zilizopo kama vile katika taasisi shirika au chama.
Mheshimiwa Jaji ninayo pia Kamusi ya kiswahili sanifu ya chuo kikuu Cha DSM (TUKI) nayo inatafsiri neno uasi vile vile
Mheshimiwa nna kamusiya kiswahili fasaha ya Baraza la kiswahili Zanzibar (KAMIZA) anasoma maana
Je Mheshimiwa kuna uhaini hapo?
Nikiitisha maandamano nchi nzima bila kibali ni uhaini?
Sio uhaini!
Inaweza kuwa uvunjaji wa Sheria za maandamano au vyovyote vile lakini sio uhaini.
Anaendelea Mhe. Lissu kuhusu kauli yake maarufu ya “TUTAKINUKISHA”
Anasema kuhusu
'Tutakinukisha sana sana, tutakinukisha vibaya sana”
Watu wanacheka sana 😂😂😂😂
Mhe. Lissu anauliza huo Uhaini?
Infact ni kosa?
Anawatazama Majini uso naona Majaji wote wapo busy kuandika.
Mrema kainamisha kichwa chini na upara wake sijui kasinzia au ndo anasikiliza kwa makini darasa la bure la sheria kutoka kwa Mhe. Lissu.
Mhe. Lissu anasema kukinukisha imetokana na neno NUKA au NUKIA kwa mujibu wa Kamusi zote tatu.
Watu wanacheka nadhani itakuwa ni kwasababu kuna muda ilisikika halafu mbaya sana kuna Askari alilala usingizi akachafua hali ya hewa.
Mhe. Lissu anasoma
NUKA : Tokwa na harufu Mbaya/ KITENDO Cha kutoa harufu Mbaya isiyopendeza
NUKIA : Tokwa na harufu nzuri/ Manukato / kutoa harufu nzuri unayopendeza
KUKINUKISHA inaweza kufanya itoke harufu nzuri ya kupendeza ama harufu mbaya.
Sasa hapa kuna kosa la Uhaini?
Kuhusu Uhaini kwenye nchi ya vyama vingi, kupinga walioko madarakank ni kosa la jinai?
Kama ni kosa la Uhaini la kunyonga mtu?
Section 55 (2) PC inaelezea maneno yasiyokuwa kosa la jinai.
Je nikisema katiba ni ya hovyo, mifumo ya uchaguzi ni ya hovyo, inatakiwa tuibadilishe mifumo hii inakuwaje ni uhaini?
Part 20 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
Niko tayari kukaa jela hata miaka 20 kama ni lazima. Hatuwezi kuruhusu wafanye wanavyotaka kwa sababu ya kutafuta uhuru wangu, kila tundu linalocheza na sheria lazima likabiliwe ili msingi wa kesi hii uwe msingi wa kushinda uovu na hila zake na kulinda haki na sheria.
Tundu Lissu
Serikali haina uwezo wa kusoma WhatsApp zako, wala kuingilia DM zako za Twitter au Instagram. Hizi huduma zinalindwa na end-to-end encryption hata wenye kuzimiliki hawawezi kusoma. Uzushi wa vitisho vya kiusalama ni hila za kuzima demokrasia. Hofu isikufunge, endelea kuwasiliana, endelea kudai haki zako. Sauti ya umma haiwezi kuzimwa na propaganda.”
@NellyBlive Wivu umewajaaa ,Wamekalia umbea tuu kuchunguza Maisha ya watu wa Hali ya chini ,Hawapendi tujenge wa kufanya maendeleo .wamewekeza wajinga miongoni mwetu kuchunguza tanaishije .Wameishiwa mbinu .Watu waliozoe kuishi kwa mishahara kamwe hawana mawazo ya maendeleo .Wivu ,wivu wivu