Civil engineer
@simba
@ccmtz
Naibu katibu mkuu kampeni ya Mama Asemewe Taifa 2025, former DITSO prime Minister, Mjumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM (M) MWANZA.
Mapema leo katika Dua Maalum ya Kumwombea Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Mwasisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, na mmoja wa waasisi wa Taifa letu.
Leo ikiwa ni kumbukizi ya miaka 54 tangu kifo chake, tunamuenzi kwa ushiriki wake katika kazi kubwa ya kuweka msingi wa ujenzi wa jamii bora yenye amani, umoja, ustawi na maendeleo yanayogusa maisha ya wananchi wote.
@HecheJohn anasema tutumie reserve yote ya mafuta ndio watangaze bei mpya, na vipi kuhusu hatari ya upungufu wa mafuta nchini hasa ikitokea bei ya mafuta itaendelea kupanda juu zaidi huko duniani?
Vipi ikitokea usafirishaji wa mafuta ukaarithiriwa zaidi? Na tushamalza reserve.
@HecheJohn tunajua wewe ni mwalimu, fikiria kuhusu chama chenu kuajiri wachumi, wakusaidie kufanya analysis kabla hujazungmza na watanzania kuhusu masuala ya kiuchumi.
Kiufupi jana umeongea mambo mepesi sana, hayafananii na ukubwa wa chama chenu unao jinasibu kila siku.
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya moto ulioteketeza Soko la Mawasiliano (Simu 2000) lililopo katika Kata ya Sinza, Wilaya ya Ubungo, mkoani Dar es Salaam, jana Aprili 4, 2026.
Ninatoa pole kwa wafanyabiashara waliopoteza mali zao na wananchi wote walioathirika na ajali hiyo kwa namna mbalimbali. Nimeziagiza mamlaka za uchunguzi kufanya kazi ya kubaini chanzo cha moto huo, kufanya tathmini ya madhara na hasara iliyotokea na kuchukua hatua stahiki haraka.
Huyu ni mtoto wa Ruto rais wa kenya(nchi yenu ya mfano) anaitwa George Ruto, ana mzigo balaa lakini huwezi kusikia wakenya wakipiga kelele mtandaoni.
Kutana na wanaharakati wa bongo, wanataka mtoto wa rais abdul apande daladala,
Ukiwa kwenye umri wa miaka 20 mpaka 35 usijenge nyumba yako binafsi kwanza(nyumba ya kuishi)
Utaichoka, mazingira yatakuchosha sababu ya kukaa eneo moja kwa mda mrefu na ukiwa na umri mdogo
Lakini pia itakuwa imepitwa na wakati kabla hata hujafikisha miaka 40.
Kama mjenzi
MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI, KWA KANDA YA ZIWA RAIS SAMIA UMEWEKA HISTORIA
Na Mwl Udadis, Nyakato-Mwanza
Rais Samia anaendelea kuonyesha upendo wa dhati na dhamira thabiti kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kupitia miradi mikubwa inayobadilisha maisha, biashara na uchumi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.
Amezidua meli kubwa na ya kisasa zaidi Ziwa Victoria, MV New Mwanza, iliyojengwa kwa gharama ya Sh120 bilioni. Meli hii ina uwezo wa kubeba abiria 1,200, mizigo tani 400 pamoja na magari, na inahakikisha usafiri salama, wa haraka na wa bei nafuu. Hii itachangia kuimarisha biashara, uvuvi, utalii na ustawi wa jamii zinazozunguka Ziwa Victoria.
Mwaka jana Juni 2025, Rais Samia pia alizindua Daraja la Kigongo–Busisi, daraja refu zaidi la aina yake Afrika Mashariki lenye urefu wa kilomita 3.2. Daraja hili limepunguza sana muda wa kusafiri, limeondoa msongamano wa feri za zamani na kufungua njia mpya za biashara, kilimo na mawasiliano baina ya jamii za pande zote za ziwa.
Aidha, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwanza unaendelea kuboreshwa kwa kasi, hasa kwa kuimarisha vifaa vya cold storage vinavyohifadhi samaki, mazao na bidhaa zinazoharibika haraka. Uboreshaji huu unawasaidia wavuvi na wafanyabiashara kupeleka bidhaa zao nje ya nchi kwa urahisi zaidi, na kufanya Mwanza kuwa kitovu muhimu cha usafiri wa anga katika eneo linalozunguka Ziwa Victoria.
Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka unaendelea kwa kasi kubwa. Reli hii ya umeme itapunguza gharama za usafirishaji wa mizigo, itaunganisha Kanda ya Ziwa na uchumi wa taifa nzima na nchi jirani, na kuleta maendeleo makubwa ya kiuchumi.
Miradi hii yote inathibitisha wazi upendo wa Rais Samia kwa watu wa Kanda ya Ziwa. Anajenga kesho bora, anaongeza ustawi na anaongeza fahari kwa wakazi wa eneo hili lote. Mwanza inakua kwa kasi, na chini ya uongozi wake thabiti, maisha bora na mustakabali mzuri unakuja kwa wananchi wa ziwa!
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mzee Edwin Mtei, Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Mzee Mtei atakumbukwa kwa mchango wake muhimu katika ujenzi wa Taifa letu, hususan katika kuimarisha misingi ya mipango, uchumi, fedha na demokrasia.
Ninatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Amina.