Karibu
Pasaka hii, badilisha mandhari! Jivinjari kwenye misitu yenye utulivu, mandhari ya kuvutia na historia ya asili inayogusa moyo.
Misitu Yetu, Utajiri Wetu
Tembea, jifunze, pumzika na ufurahie uzuri wa TZ kupitia utalii wa misitu.
• Namshukuru Allah kwa kila hatua ambayo haikukamilika, lau kama ingekamilika basi kwangu ingekuwa shari kubwa.
• Namshukuru Allah ambaye ameizuia shari, ila kwa ujinga wangu nilidhani kuwa ni kheri kwangu.
• Namshukuru Allah ambaye anapangilia mambo yangu, anafanya kwa upole na mwingi wa huruma.
• Namshukuru Allah ambaye anachukua kila anachokitaka, kisha ananipa kilicho bora zaidi.
#Muislam
Swala la masiku kumalizika haraka katika ramadhani ni kawaida.
Jambo moja tusifanye mambo kwa mazoea baada ya Eid kila kitu tunaacha.
Hii si sawa na huu sio utaratibu wa uislam..
Tumche Allah ukweli wa kumcha.
Na tujue kila kitu kinaandikwa tuje kula hasara.
Masharti ya Hijabu iliyo sahihi (Hijabu ya Kisheria).
• Jilbaabu / Nguo iwe ndefu, ifunike mwili mzima mpaka miguu, na kama haikufunika miguu basi mwanamke avae soksi.
• Nguo iwe pana, isiwe yenye kuonesha umbo (yaani isiwe yenye kubana popote mwilini).
• Nguo iwe nzito, na sio nyepesi yenye kuonesha mwili.
• Nguo isiwe na urembo wowote wenye kuvutia.
• Nguo haitakiwi ifanane na mavazi ya makafiri.
• Asivae nguo ya fakhari (kwa lengo la kuleta kiburi, kujifakharisha mbele za watu na kujionesha).
• Nguo isifanane na mavazi ya kiume.
• Kutotia manukato (yaani nguo haitakiwi kuwekwa manukato yoyote pindi mwanamke anapotoka nje ya nyumba yake).
Na Allah ni Mjuzi zaidi.
Ndugu yangu ikiwa hii Dunia haipatikani kwa urahisi vipi hiyo Pepo!?
Kama kweli twaitaka pepo na starehe ya milele ni lazima tujipinde kweli kweli na Ibada na mambo ya kheri na kumtii Allāh na kumfuata Mtume swala na salamu ziwe juu yake
Hakuna Njia nyingine zaidi ya hii.
Shaykh Muqbil ibn Hādī al-Wādiʿī [Allah Amrehemu] alisema:
“Maadui wa Uislamu wanajitahidi sana kupotosha wanawake kupitia aina mbalimbali za propaganda za uongo.
Hakika! Sisi ni wa Allāh, na hakika, Kwake tutarejea.
NDUGU ZANGUNI WATANZANIA!
Mna fursa kubwa sana ya kusoma dini kwani neema ya Manhaj Salafi imeenea Alhamdulillah. Ndugu zanguni waislamu ikumbatieni hii Neema kwa kusoma dini yetu. Hakuna udhuru wa kutoelekea kwa vituo vya elimu sahihi. Okoa nafsi Yako kwa kuusoma Dini Yako.
The Messenger of Allāh صَلَّى اللّٰهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ said:
❝No man should be alone with a woman unless there is a mahram with them.❞
[Al-Bukhari and Muslim]
Mtume SAW amesema: Kuna neema mbili ambazo watu wengi hupoteza: (Neema hizo ni) afya na muda wa bure wa kufanya mambo mema.
Maelezo ya Tafsiri:
Hadithi hii inaangazia neema mbili kubwa ambazo binadamu wengi hawazitambui au hawazithamini ipasavyo hadi wanapozikosa. Neema hizi ni afya na muda wa bure. Mtume SAW anatushauri kuwa makini na jinsi tunavyotumia neema hizi kwa sababu zinaweza kuleta faida kubwa ikiwa tutazitumia ipasavyo kwa kutenda mema.
Afya: Wakati mtu akiwa na afya njema, ana uwezo wa kufanya kazi nyingi, ibada, na kutenda mambo mema kwa ufanisi. Mara nyingi, watu hawaithamini afya yao hadi wanapopata ugonjwa au udhaifu.
Muda wa bure: Huu ni muda ambao mtu hana shughuli muhimu au dharura za lazima. Ni fursa ya kujiendeleza, kufanya ibada, kusaidia wengine, au kutenda matendo mema. Wengi hupoteza muda wao bure kwenye mambo yasiyo na faida, badala ya kuutumia kwa mambo mema.
Hadithi hii inatufundisha kuwa waangalifu na busara katika kutumia afya na muda wa bure. Ni wito wa kutumia neema hizi kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu na kufanya mema yanayoweza kuleta faida kwa dunia na akhera.
Amesema Sheikh Swaleh Alfawzani hafidhwahullāh:
ليس لك في الآخرة إلا عملك
ولا أحد يعطيك حسنة واحدة.
((Huna Wewe huko Akhera ila amali zako tu pekee hakuna hata mmoja atakae kupa Wewe walau jema Moja hakuna.))
شرح الدلائل (١٩٣)