Klabu ya Bayern Munich imekamilisha usajili wa winga Ivan Perisic kutoka klabu ya Inter Milan kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima huku kukiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja.
#MaongeziUpdates
-Makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela wamewaambia mashabiki wa klabu ya Yanga ambao wamekosa jezi mpya za klabu ya Yanga ambazo zilizinduliwa jana wasiwe na wasiwasi kwani kampuni ya GSM inafanya mpango wa kupatikana kwa jezi nyingi zaidi.
Klabu ya Manchester United imempa ofa ya kumlipa mshahara wa £350,000 kwa wiki mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala katika mazungumzo yanayoendelea hivi sasa ili kumshawishi ajiunge na mashetani wekundu hao.
#MaongeziTetesiKimataifa