Mahakama Haina Mamlaka ya Kubadilisha (Mkataba) Makubaliano ya Watu Zaidi Inayabariki na Kuhakikisha Yanatekelezwa. Labda Kuwe na Dalili za Udanganyifu na Upotoshaji au kwa Sera ya Nchi Mkataba Hauwezi Kufuatwa Tena.✍🏼 MD 👇🏿👇🏿
Mahakama Haitakiwa Kuingia Kwenye Msingi wa Maombi na Kutolea Maamuzi Maombi Ambayo Hayajimudu (Incompetent)/Yamekuja Mahakamani Ndivyo Sivyo. Ikigundulika Maombi Hayako Sawa, Yanatakiwa Kuondolewa Mapema tu.✍🏼
#WC, QF, Next Fra v. Eng, Fra 👍🏿
Unahisi Unalimiliki Eneo Kihalali, Unajenga Nyumba, Unapanda Mazao na Miti, Anakuja Mtu Hajakupa Hata Notisi Anabomoa Nyumba na Kufyeka Mazao na Miti, Anasema Yeye Mmiliki, Kesi Inaenda Mahakamani Inathibitika Kwamba Hukuwa Mmiliki. Je Utapata Fidia kwa Kanuni ya Usawa (EQUITY)?
Imezoeleka Maombi Mahakamani Huwa Yanasindikizwa na Kiapo, Ni Kosa Kubwa Sana kwa MUAPAJI (DEPONENT) KUTOSAINI KIAPO, Itapelekea Maombi Kuondolewa (Struck Out).✍🏼
Jaji/Hakimu Anatakiwa Kujiepusha Kutengua Maamuzi ya Jaji/Hakimu Mwenzake.
Pingamizi la Awali Lilitupwa na Jaji wa Kwanza, Baadae Kesi Ikahamia kwa Jaji Mwingine, Pingamizi Likaja Tena, Akaona Lina Mashiko, Akafuta Kesi.✍️
Kuna Vitu Vinaonekana Vidogo Ila Usipovifanya Vinagharimu Rufaa Yako Katika Mahakama ya Rufaa.
Notisi ya Rufaa Unatakiwa Kuwapelekea Upande wa Pili Ndani ya Siku 14 Toka Ulivyoifaili Mahakamani. Usipofanya Hivyo, Itakuwa Sababu ya Kuiondoa, Bila Notisi Hakuna Rufaa.✍️
Pia, Barua kwa Msajili wa Mahakama Kuu Ukiomba Nyaraka kwa Ajili ya Rufaa, Ili Ikusaidie Baadae, Unatakiwa Kuiandika na Kuwapelekea Upande wa Pili Ndani ya Siku 30 Tangu Yatoke Maamuzi ya Mahakama Kuu. Usipofanya Hivyo, Itakuwa Sababu ya Kuiondoa (Strike Out) Notisi ya Rufaa✍🏼