ni kujidanganya kudhani kwamba huduma za umma zinaweza kuboreshwa pale ambapo watu waliokabidhiwa jukumu la kuhakikisha hilo linatokea hata hawatumii huduma hizo. kama kitu hukitumii wewe, wala mtu yoyote unayemjali kama mtoto wako, hamasa ya kukiboresha unaitolea wapi?
Well said!
Kwa kukazia hapo hapo, naona hii ni matokeo ya utendaji duni ama uwajibikaji uliozorota katika mfumo.
Kila kiongozi katika wadhifa wake hawajibiki kwaajili ya wananchi na hivyo basi hakuna changamoto zozote ninazotatuliwa kwa ufanisi stahiki.
Wanajiamulia mambo.
Tulipofikia sasa ni tumebadili kabisa tafsiri ya uongozi kwenye serikali.
Uongozi/Position/Cheo hatuvichukulii tena kama ni jukumu la kuwatumikia raia, tunachukulia ni fursa ya kufanikiwa kimaisha!!
Mtu akiteuliwa kwenye position fulani hatumpongezi kama anaenda tumikia wananchi, tunampongeza kama ameshatoboa kimaisha!!
Hata mtu akikosa uteuzi eneo fulani utaona anaumia sana kwasababu fursa ya tobo la maisha yake imezibwa!! Huwezi kuumia kisa umenyimwa fursa kutumikia watu!!
Au kiongozi unamskia anasema, niligombea ubunge nikakosa, nikavumilia miaka 5π Nikaja teuliwa kuwa DC.
Nikasota kwenye uDC π³ miaka 7 leo Mungu mkubwa nimekuwa waziri!
(Yaani kwanini unaita ni kusota)π€·ββοΈ
(Umesota kutowatumikia wananchi?π how?)
(Nini ulivumilia?
Unavumilia kutowatumikia wananchi) How!!?)
Huu ni utamaduni mbaya sana!!
Dawa ya hii ni kupunguza mishahara ya viongozi na kupunguza privileges kwao!!
KATUGA BABA π₯π₯
β KATUGA: Unasema wewe ni mtaalamu wa sheria za uchaguzi, siyo?
π΄ LISSU: Ndiyo.
β KATUGA: Basi unajua kwamba haki ya mtu mmoja haiwezi kutumika kuondoa haki ya mtu mwingine?
π΄ LISSU: Inategemea mazingira.
β KATUGA: Mazingira gani yanayoruhusu mtu kuzuia mwingine kutumia haki yake ya kupiga kura?
π΄ LISSU: Kuna haki ya maandamano.
β KATUGA: Siku ya uchaguzi, ukiandamana na kuzuia vituo vya kupigia kura visifunguliwe, unakuwa umezuia watu wengine kupiga kura?
π΄ LISSU: Hilo si lazima litokee.
β KATUGA: Sijakuuliza kama lazima litokee. Nakuuliza: ikiwa maandamano hayo yatazuia watu kupiga kura, je, haki yao itakuwa imekiukwa?
π΄ LISSU: Hiyo ni tafsiri yako.
β KATUGA: Ni tafsiri ya Katiba au yako?
π΄ LISSU: Katiba ina mambo mengi.
β KATUGA: Lakini swali langu ni rahisi: Je, kuzuia mtu kupiga kura ni kuingilia haki yake?
π΄ LISSU: Kama mtu anazuia kwa njia isiyo halali, ndiyo.
β KATUGA: Kwa hiyo kuna namna ya kuzuia uchaguzi ambayo ni halali?
π΄ LISSU: Ndiyo, kupitia njia za kikatiba.
β KATUGA: Njia hizo za kikatiba zinahusisha kuzuia wapiga kura kufika vituoni?
π΄ LISSU: Hapana.
β KATUGA: Zinahusisha kuwatishia wapiga kura?
π΄ LISSU: Hapana.
β KATUGA: Zinahusisha kuwarushia watu mawe?
π΄ LISSU: Hapana.
β KATUGA: Zinahusisha vurugu?
π΄ LISSU: Hapana.
β KATUGA: Basi tunakubaliana kwamba vurugu si njia ya kidemokrasia ya kupinga uchaguzi?
π΄ LISSU: Vurugu ni suala tofauti.
β KATUGA: Tofauti kivipi?
π΄ LISSU: Sijui unataka kuniuliza nini.
β KATUGA: Nakuuliza kilekile nilichokuuliza tangu mwanzo. Je, kuchochea vurugu ni demokrasia?
π΄ LISSU: Hapana.
β KATUGA: Je, kuzuia watu kupiga kura kwa nguvu ni demokrasia?
π΄ LISSU: Hapana.
β KATUGA: Je, kuwatishia watu ili wasiende kupiga kura ni demokrasia?
π΄ LISSU: Hapana.
β KATUGA: Basi kwa nini unapozungumzia βkuzuia uchaguziβ hutenganishi wazi kati ya maandamano ya amani na vitendo vya kuzuia wapiga kura kwa nguvu?
π΄ LISSU: Kwa sababu hotuba lazima itazamwe kwa muktadha wake.
β KATUGA: Na ndiyo maana nimekuuliza kuhusu muktadha. Lakini kila nikikuuliza kuhusu kitendo chenyewe, unarudi kwenye hotuba.
π΄ LISSU: Kwa sababu hotuba ndiyo msingi wa jambo hili.
β KATUGA: Au kwa sababu ukijibu swali moja kwa moja, majibu yako yanaweza kukinzana na unachodai kuhusu demokrasia?
π΄ LISSU: Sidhani hivyo.
β KATUGA: Huna uhakika?
π΄ LISSU: Nina uhakika.
β KATUGA: Basi jibu swali langu la mwisho: Je, demokrasia inakupa haki ya kuzuia watu wengine kutumia haki yao ya kupiga kura?
π΄ LISSU: Kuna mambo mengi yanayohusika...
β KATUGA: Ndiyo au hapana, Mheshimiwa?
π΄ LISSU: Nimekwishasema ninachokiamini.
β KATUGA: Hujajibu swali.
π΄ LISSU: Nimejibu kwa namna yangu.
β KATUGA: Mahakama haikuulizi kwa namna yako. Inataka jibu.
@royalmediatz TAFAKARI
Kwani ni haramu kukubali kua wanafadhiliwa? π€
Kila chama kikubwa nchini kinapata ufadhili wa kutoka nje kuendesha shughuli zake.
Pengine wanakanusha kwakua ni kweli hizo fedha wanatumia kufadhili MAASI na sio MABADILIKO
Kazi ya ualimu ina frustration sana, haswa pale mazingira ya kazi yanapokuwa magumu.
Wakati mwingine ni vigumu sana kuepuka kuwa na hasira katika kutimiza nia ya dhati kabisa ya kusaidia watoto kufanikiwa.
Ni ama upuuzie au ulazimike kuenforce nidhamu ya hali ya juu kwa mabavu ili kufanikisha lengo.
Mwalimu hana vitabu vya kutosha, kwa hiyo analazimika kutumia viboko kulazimisha watoto kukopi notes n.k.
Mwalimu mmoja anapangwa zamu kusimamia wanafunzi elfu moja. Hapo analazimika kutandika viboko ili kufanya classical conditioning na kucontrol nidhamu ya wengine kibao.
Mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi 100 darasani pasipo namna yoyote ya kutoa one-on-one support. Analazimika kucompensate kwa kulazimisha watoto wafanye yale anayohisi yanaweza kusaidia etc.
Frustration ya yote haya mwisho wake ndio unaleta ajali kama hizi, wakati mwingine pasipo kukusudia kabisa.
Ukiangalia kwa umakini zaidi, hata kwa experience yetu tu kipindi tukiwa shule, unaweza kuona kwa kiasi kikubwa wale walimu waliokuwa wanaonekana kujali kwa dhati maendeleo ya watoto, ndio waliokuwa wakali kupindukia.
Sina maana ya kuwatetea kwa hili. Hata hivyo najaribu pia kuangalia namna mazingira ya kazi yanavyochangia haya.
Sio excuse though!