Selikari inabid iwekeze Sana katika elimu ya ufundi na ubunifu,Lakin pia itengeneze system ya kuwafinance machampion kwenye ubunifu na kuwaendeleza zaidi katika Nchi ambazo zimeendelea technologically
I urge Heads of State and the leaders of nations to listen to the cry of the poorest. There can be no peace without justice. The poor remind us of this in many ways, through migration as well as through their cries, which are often stifled by the myth of well-being and progress, which does not take everyone into account.
OMG!! 😭😭😭😭 hii ni Mortuary ya Mwananyamala. Alieachia video hii anahofia mnooo maisha yake ndo maana imemchukua muda sana kunipa video hii.
Anasema kuwa polisi walikuwa wanachukua simu za manesi na madokta wanafuta video na picha na kuwatishia wasirekodi kitu, yeye alikuwa na simu 2 so akawapa simu ambayo alikuwa hajarekodi chochote wakaridhika.
KABLA YA MAZUNGUMZO LAZIMA WALIOPANGA,KUFADHILI NA KUENDESHA MAUAJI YA RAIA WA TANGANYIKA NA KUHUSIKA NA MPANGILIO WA UTEKAJI NA UPOTEZAJI WA RAIA KABLA,WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI WAKAMATWE NA KUFIKISHWA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KWA UHALIFU DHIDI YA UBINADAMU.
WATU WOTE WALIOTEKWA NA KUPOTEZWA WAREJESHWE NA KUUNGANA NA FAMILIA ZAO NA KUACHIWA MARA MOJA KWA TUNDU LISSU NA KUONDOLEWA KESI ZOTE ZA UONEVU DHIDI YA CHADEMA NA VIONGOZI WAKE.
KUTAFUTA MAZUNGUMZO SASA KABLA YA UWAJIBIKAJI NI KUTUKANA NDUGU ZETU WALIO UWAWA BILA HATIA NA KUBARIKI UDHALIMU.
KILA MMOJA ABEBE MSALABA WAKE KWANZA NA AWAJIBISHWE KWA NAMNA ALIVYO SHIRIKI MAUAJI HAYA YA RAIA WASIO NA HATIA .HAKUNA KUSAFISHANA.
BAK MWABUKUSI.
PRESIDENT - TLS
"#Tanzania is sliding into electoral authoritarianism – a system where polls are held, but within a manipulated process where the ruling party retains power through state control, patronage, violence, intimidation and manipulation of electoral systems." https://t.co/jBqlmAwhkG
Tatizo askari wetu wanahisi kama yakifanyika mabadiliko ya kiutawala au upinzani ukichukua nchi basi wote wataachishwa watakosa kazi!!
Upinzani hauji na askari wake jamani, upinzani hauna askari polisi wa kucover nchi nzima, askari mtaendelea kuwa nyie nyie na kazi yenu hamtapoteza.
Kinachopambaniwa hapo ni mabadiliko ya kimfumo, ili tuwe na mfumo bora unaosimamia na kutoa haki kwa raia na mali zake!!
Mfumo wenye maslahi na watanzania wote, watoto na wajukuu zenu na sio kikundi cha watu wachache!!
Ungeni mkono tulete mabadiliko na kwenu hamtapoteza ajira zenu!!
📍London, Uingereza
🇹🇿🇬🇧
▪️WAZIRI KOMBO AKUTANA NA UJUMBE MAALUM WA BIASHARA WA UINGEREZA
➡️ Tanzania na Uingereza Kuimarisha Ushirikiano wa Kibiashara na Uwekezaji
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na kuzungumza na Mjumbe Maalum wa Biashara wa Uingereza kwa Afrika Mashariki, Mhe. @KateOsamor (Mbunge), katika Jumba la Commons, jijini London.
Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza, kupitia miradi inayoendelea na mipango mipya inayohusisha nishati, madini, uchumi wa buluu, fedha za kijani, ubunifu wa kidijitali na kilimo cha mazao ya biashara.
Waziri Kombo alisisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji, pamoja na kuhakikisha miradi inayoungwa mkono na taasisi za kifedha za Uingereza, ikiwemo UK Export Finance (UKEF) na British International Investment (BII), inatekelezwa kwa ufanisi.
“Tanzania inathamini ushirikiano wa kihistoria na Uingereza na inatambua mchango mkubwa wa miradi ya uwekezaji katika kuongeza ajira, kukuza biashara ya kikanda na kimataifa, na kuendeleza sekta za kipaumbele kama madini muhimu, nishati safi, na uchumi wa buluu,” alisema Mhe. Waziri Kombo.
Kwa upande wake, Mhe. Asamor aliipongeza Tanzania kwa hatua inazochukua kuboresha mazingira ya uwekezaji na kusisitiza dhamira ya Uingereza kuendelea kushirikiana kwa karibu katika miradi ya kimkakati. Alieleza kuwa Uingereza iko tayari kusaidia upatikanaji wa masoko kwa mazao ya kilimo, kuimarisha miradi ya miundombinu ya Zanzibar na kusaidia miradi ya kijani na kidijitali.
Mazungumzo hayo pia yaligusia maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, ambapo Waziri Kombo alibainisha kuwa kwa mara ya kwanza uchaguzi huo unasimamiwa na tume huru ya uchaguzi, hatua ambayo itaongeza uwazi na kuimarisha imani ya wawekezaji.
Pande zote mbili zilithibitisha kuendeleza uratibu wa karibu kupitia Tanzania Investment and Special Economic Zones Authority (TISEZA) na kukubaliana kuanzisha timu ya ufuatiliaji (delivery team) ya pamoja itakayokuwa na mapitio ya robo mwaka ili kuhakikisha utekelezaji wa haraka wa makubaliano yaliyofikiwa.
📸 | W/Mambo ya Nje
@dailynewstz@MbelwaK@GileadTeri@UKinTanzania@HabariLeo
🇹🇿🇬🇧
▪️WAZIRI KOMBO KUFANYA ZIARA NCHINI UINGEREZA
Waziri wa Mambo va Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi @mahmoudkombo kufanya ziara rasmi nchini Uingereza kuanzia tarehe 08 hadi 12 Septemba 2025, inayolenga kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na wa muda mrefu baina ya Tanzania na Uingereza.
📃 | W/Mambo ya Nje
@UbaloziUK@MbelwaK@UKinTanzania@MYoungFCDO
Mapesa yanayomwagwa na watawala ni harufu ya ufisadi, lakini tone tone za wananchi ni harufu ya haki na uadilifu. Kila tone la mchango wa mwananchi ni alama ya damu ya kizazi kinachopigania uhuru wa kweli , Rais Samia hawezi kulifuta kwa kejeli.
📍Kigali, Rwanda
🇹🇿🇷🇼
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. @mahmoudkombo (Mb), amekutana na Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame, Ikulu ya Kigali, Rwanda.
Viongozi hao wameangazia ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Rwanda pamoja na matunda ya Mkutano wa 16 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Rwanda, uliofanyika jijini Kigali kwa siku tatu, kuanzia tarehe 24 hadi 26 Julai, 2025.
📸 | W/Mambo ya Nje
📍Yokohama, Japan
🇹🇿🇯🇵
▪️WAZIRI KOMBO AWASILI JIJINI YOKOHAMA (JAPAN) KUSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA TICAD 9
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi @mahmoudkombo (Mb.) amewasili jijini Yokohama, Japan kumwakilisha Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development-TICAD 9) ambao unafanyika kwa ngazi ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika na Japan kuanzia tarehe 20-22 Agosti 2025.
Mheshimiwa Waziri Kombo amepokelewa na Mhe. Hideaki Harada, Balozi wa Zamani wa Japan nchini Namibia ambaye amekasimiwa jukumu la kumpokea Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania; Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Baraka Luvanda ambaye ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bi. Felista Rugambwa na Maafisa Wandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Fedha na Ubalozi wa Tanzania nchini Japan.
Mheshimiwa Waziri Kombo pamoja na kushiriki mkutano huo atafanya mazungumzo na Mhe. Takeshi Iwaya, Waziri wa Mambo ya Nie wa Japan, Bw. Ando Naoki, Makamu wa Rais wa JICA; viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi wa Japan; Wakuu wa Taasisi na kampuni za uwekezaji wa Japan kwa ajili ya kuhamasisha uwekezaji, biashara na utalii hapa nchini.
📸 | W/Mambo ya Nje
📍Ikulu, Zanzibar
🇹🇿🇮🇹
▪️RAIS MWINYI: ZANZIBAR INAHITAJI FURSA ZA UWEKEZAJI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Zanzibar inahitaji fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Buluu, sekta ya miundombinu, afya pamoja na fursa za kibiashara kwa ajili ya kuongeza thamani ya bidhaa za karafuu na mazao ya baharini.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk, aliyefika Ikulu Zanzibar tarehe 19 Agosti 2025 kumuaga baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa sera ya diplomasia ya uchumi ndiyo iliyopewa kipaumbele hivi sasa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo ni vema Balozi huyo kuifanyia kazi sera hiyo ili uchumi wa Tanzania hususan Zanzibar uendelee kuimarika.
Naye Balozi Mbarouk amemhakikishia Rais Dkt. Mwinyi kwamba ataendelea kuimarisha zaidi mahusiano pamoja na kutafuta fursa mbalimbali za ushirikiano.
📸 | IKULU
Happy birthday, Mheshimiwa Balozi! 🎂🎈
I wish you a day overflowing with joy and celebration! Thank you for your incredible all-seasons mentorship and unwavering support; you’re truly a blessing!
Kama kuna kigezo/sababu za kuondolewa kwako katika mbio hizi za ubunge; ni USHAWISHI wako usiotetereka kwa wanachama wa CCM na Watanzania katika misimu yote. Wapo wapi ulioingia nao top 5 Mwezi Julai 2015? Tumshukuru Mwenyezi Mungu.
Umekuwa gumzo ukiwa bungeni, na serikalini; kwa nini wewe!!!
Umeshinda uwoga wao, unafiki, mizengwe na shoti zisiso na hesabu.
Ni mtikisiko, si mwisho.
Rutaraka^
🇹🇿🇮🇳
A new chapter had begun for Tanzania-India tourism relations as Tanzania Tourism Board (TTB) hosted H.E. Bishwadip Wey, India’s High Commissioner to Tanzania and top business leaders for a high-impact dialogue with the Minister of Natural Resources and Tourism, Hon. Pindi Chana.
The dialogue focused on joint marketing, culinary exchange, capacity building, and tourism investment opportunities, with Tanzania and India charting a new path of collaboration in travel, culture, and trade.
It was emphasized that together, we’ll build a stronger, more inclusive tourism future.
📍Dar es Salaam
🇹🇿🇰🇷
▪️SEKTA YA UTALII KUIMARISHA ZAIDI USHIRIKIANO WA TANZANIA NA KOREA KUSINI
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania Mhe. Eunju Ahn kwenye kikao kilichofanyika katika Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dares Salaam mapema leo Julai 11, 2025.
Mazungumzi katika kikao hicho yalijikita katika namna bora ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi mbili kupitia sekta ya utalii; ambapo moja ya mawasilisho yaliyowasilishwa katika kikao hicho linalenga kuboresha Chuo cha Taifa cha Utalii katika nyanja tofauti.
📸 | W/Maliasili na Utalii
📍 Malabo, Equatorial Guinea
▪️WAZIRI KOMBO ASHIRIKI KIKAO CHA 47 CHA BARAZA LA MAWAZIRI AU
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi @mahmoudkombo ameshiriki katika kikao cha 47 cha Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika (AU) kinachoendelea jijini Malabo, Equatorial Guinea.
Baraza hilo limejadili Ripoti ya Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu wa AU (Permanent Representative's Committee - PRC) ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imechangia hoja mbalimbali za muhimu ikiwemo kuunga mkono kuidhinishwa kwa mapendekezo ya bajeti ya Umoja wa Afrika kwa mwaka 2026 ambayo imezingatia hali halisi ya uchumi wa nchi wanachama.
Pia, Tanzania imesisitiza umuhimu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kukamilisha Mpango Mkakati wa Miaka Mitano ili kuhakikisha mipango ya mwaka mmoja mmoja inaendana na vipaumbele vya Mpango wa Pili wa Miaka Kumi ya Utekelezaji wa Agenda 2063.
Aidha, Tanzania imetoa rai na ushauri kwa AU kutumia vyema fursa ya Jamhuri ya Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa mkutano wa G20, 2025 kupenyeza vipaumbele vya Bara la Afrika hasa kwenye maeneo ya upatikanaji sawa wa ufadhili wa maendeleo, mageuzi kwa taasisi za fedha za kimataifa, na ufumbuzi wa haraka wa udhaifu unaoongezeka wa madeni barani Afrika, kupata ufadhili wa muda mrefu wa miundombinu, na kukabiliana na hali ya hewa, na mseto wa kiuchumi.
Mkutano huu wa 47 wa Baraza la Mawaziri unautangulia Mkutano wa Saba wa Kamati ya Uratibu ya Umoja wa Afrika utakaohudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kamati ya Uongozi ya Umoja wa Afrika (AU Bureau of Assembly), na Wenyeviti wa Jumuiya 8 za Kikanda happ Julai 13, 2025.
📸 | W/Mambo ya Nje