Tunajivunia ninyi. Mmetuheshimisha. Tunapoheshimiwa pasipo ninyi kuwepo, sifa na heshima husika ziwafikie popote mlipo na mtakapokuwa. Mmeyafanya hayo uwanjani, mmetufundisha yote yanawezekana kila Mtanzania akitenda ipasavyo, sehemu alipo katika kutimiza majukumu yake.
Hongereni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh Waziri Waziri Kindamba kuzindua boti ya abiria kwa safari za Tanga -Zanzibar. Ni matunda ya mazingira bora kwa uwekezaji na wawekezaji nchini yanayoboreshwa na serikali ya Mh Rais Dk Samia Suluhu Hassan.
Hongereni Kikundi cha Sanaa cha Wadatoga mliohamia kijijini Msomera kwa hiari yenu kutoka Ngorongoro, kwa fursa ya burudani kwenye ufunguzi wa kikao cha 77 cha Kamisheni ya Haki za Binadamu na Watu Afrika kilichifanyika Arusha. Hii ni moja ya ishara ya fursa nyingi mlizozikosa.
Rajab Athuman. Umebuni Jambo jema Sana kijamii, kiuandishi na kimawasiliano kutokea huko Handeni. Ubunifu huu utakufikisha mbali kimafanikio. Keep it up kijana wangu. πͺπͺπͺ
Wakati dunia ikikabiliwa na magumu mengi yanayopunguza upendo kwa watu, Rais Mh Dk Samia Suluhu Hassan kwake ni kinyume kabisa. Anatoka kwenye eneo maalum kwenda kuchangamana na abiria wengine.
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kutujalia Kiongozi mwenye utu na upendo wa kweli kwa watu
Mnaposafiri takribani kilomita 500 kutoka Handeni kwenda Manyara kushiriki hafla ya kuzima Mwenge wa Uhuru 2023, vijana Wazalendo kutoka Handeni mkoani Tanga mmedhihirisha ufahamu mkubwa na uthamini mlio nao kwa alama na ishara za matumaini, upendo, amani na maendeleo ya nchi.
Kipa namba 2 wa timu ya RS Tanga 'akipasha' kabla ya mechi. Leo ameshindwa kuendelea kwenye mechi dhidi ya timu ya Nishati katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea Mjini Iringa, kutokana na rafu aliyochezewa na mshambuliaji wa timu ya Madini. Matokeo yalikuwa 1-1.
Mimi na Mama yako Herieth Nkuruvi , Kaka yako Kennedy, wadogo zako Brian na Shazma na dadako Miriam tunakuombea mitihani mwema wa kuhitimu elimu ya misingi Benedict Bonifas, utakaofanyika kuanzia kesho. Tunamshukuru Mungu, kupitia kwa walimu wako, ukasoma na sasa umefika.AMINA
Hongera Doto Kadoshi na tumshukuru Mwenyezi Mungu kutujalia mavuno kwa ndugu zetu wa Msomera na Handeni kwa ujumla. Uwe na afya njema katika kutuletea habari njema kama hii.
Kufurahi ni miongoni mwa viashiria msingi vya upendo wa kweli na amani ya kweli katikati ya watu nchini. Hongereni viongozi wetu Mh Rais Daktari Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa JKT, Meja Jenarali Rajabu Mabele kwa kutufanikishia adhimisho la Miaka 60 ya JKT.