One of #MicheweniFM's objectives is to enable Micheweni communities to participate in the design and implementation of effective communication strategies for enhanced debates, partnerships, and networking for their improved wellbeing.
#ReachWhereOthersDont#CommunityContent
"Tunajua mnafanya jambo kubwa kwa jamii na nchi yetu kwani kama kuna jambo ambalo nchi inapata hasara ni kwenye matibabu. Na matibabu ya maradhi yasiyoambukiza kwahakika ni ya ghali sana na nyinyi nyote ni mashahidi," Mhe. Othman Masoud, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
📍"Niwaombe tuweke kanuni za kusiamamia maadili zitakazondoa dhana potofu kwa jamii ili tuweze kuwavutia watu wengi kushiriki mazoezi kukwasababu hili jambo ni jema zaidi," Mhe. Othman Masoud, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Bonanza la #MichezoKwaWote
📌Wanamichezo kutoka sehemu mbalimbali wameungana alfajiri ya leo kushiriki Bonanza la Gombani Pemba lililoongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman.
Tunahimiza ushiriki wa makundi yote katika mazoezi na michezo #MichezoKwaWote
“Twende mbali zaidi kutoa ya elimu lishe kwa jamii. Kwani wengi tumeacha sasahivi vyakula asilia. Mwingine anaona pengine vyakula asilia sio usasa.” Mhe. Othman Masoud, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.
#MichezoKwaWote
📍Ukosefu wa miundombinu na vifaa wezeshi vya mazoezi ni kikwazo katika ufikiaji wa usawa wa kijinsia kkwenye michezo na kuomba serikali na wadau kusaidia kuboresha miundombinu hiyo ili kuwezesha kila mmoja kushiriki bila kikwazo.
#MichezoKwaMaendeleo
"Tuwe mifano mizuri ya kuwa na heshima katika jamii, kwasabau sisi tuna nafasi ya kupata mawaidha sehemu mbalimbali ya stadi za maisha. Hivyo tuna kila sababu ya kuendeleza kuimarisha na kuhamasisha michezo kwa wote," Dkt @mzuri_issa, mkurugenzi TAMWA ZNZ. #MichezoKwaMaendeleo
Karibu Viwanja vya Mnazi mmoja uungane na watoto kwenye Mtoto wa Afrika Marathon 2024 ujifunze mbinu za michezo shirikishi za kukuza usitawi wa jamii.
#MichezoKwaMaendeleo#KimbiaNaMtoto@zafela@NorAmbTZ
TAMWA ZNZ inawashukuru wadau wote walioungana nao jana katika tukio muhimu la Mtoto wa Afrika Marathon 2024 kuhamasisha ushirikishwaji wa jinsia zote katika michezo #MichezoKwaMaendeleo.
Hakika watoto walifurahia sana.
Tuendelee kushirikiana kujenga usitawi bora wa watoto.
Kongamano lilijadili sana matumizi ya Akili Mnemba (AI) katika kurahisisha utendaji kazi na fursa zake kwenye vyombo vya habari. Hata hivyo, wachangiaji walisisitiza umuhimu wa kuwa makini dhidi ya upotoshaji wa taarifa na picha, hasa wakati wa uchaguzi.
Mabalozi wa nchi za Nordic ambazo ni @NorAmbTZ, @DKAmbTanzania, @SwedeninTZ na @FinnishEmbTZ mwishoni mwa wiki hii waliungana na wadau Zanzibar kuadhimisha wiki ya Nordic ambapo wadau walipata fursa kubadilishana maarifa ikiwemo upishi wa vyakula kwa kutumia rasilimali za majini.
Katika hafla iliyowakutanisha viongozi wa serikali, mabalozi na wakuu wa taasisi za serikali na za kiraia katika hoteli ya Emerson mji Mkongwe, Balozi wa Norway nchini, Balozi Tone Tinnes amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi rasirimali za bahari kwa maendeleo endelevu.
Hafla hiyo fupi yenye lengo la kukuza mwamko wa kiutamaduni kwa vyakula vya baharini (#Seafood) ilishereheshwa na vijana kutoka chuo cha hotel Maruhubi Zanzibar kwa kuandaa mapishi mbalimbali na kusimulia hadithi iliyopo katika vyakula hivyo.
Wahariri wa Vyombo vya habari Pemba wakishiriki michezo wakati wa mafunzo ya #MichezoKwaMaendeleo yaliyoandaliwa na TAMWA ZNZ.
Je ni mchezo gani wewe unapendelea kuucheza?
Leo June 3, TAMWA ZNZ inakutana na wahariri wa vyombo vya habari kisiwani Pemba kujadiliana masuala ya #UsawaWaKijinsia kwa vyombo vya habari kuzalisha maudhui bora yanayohamasisha ujumuishi wa makundi yote kushiriki katika #MichezoKwaMaendeleo.
Unapenda kushiriki mchezo gani?
"Waandishi wa Habari na wana Asasi za Kiraia hapa mkoani Shinyanga tusaidiane kupeana mbinu pale ambapo tunaona kuna viashiria vya uoga wa mtu kujieleza ili tuisadie jamii kupata haki". Glory Mbia - Mratibu wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania Trust), Mkoa wa Shinyanga.
#FreedomOfExpression #CommunitySeminar
"Vyombo vya Habari ni washirika wa maendeleo, hivyo kuwa na sera na sheria bora itawawezesha waandishi wa habari kuwa na mazingira rafiki katika kutekeleza
majukumu yao," Salim Said, mwandishi wa habari mkongwe Z'bar. #UhuruWaHabari
Ni vikwazo gani hasa vinawakabili waandishi?
Nasaha za Ukombozi wa Afrika
Mwl. J.K Nyerere - 1968; "Hii mipaka ni mikubwa kuliko Afrika, Tuitukuze mipaka Hii?"
Sikiliza Hotuba hii iliyoasha ari na morari kwa Msumbiji, Zimbabwe, Namibia na Afrika ya Kusini kupata Uhuru wao
@urithiwaukomboz, Fahari ya Afrika