Kama kuvaa nguo za jeshi ni kosa kisheria basi ifike wakati SERIKALI ipige marufuku kwa mtu ambae sio mwanafunzi kuvaa sare za SHULE kwa afya ya vizazi vijavyo.
@Dr_DGwajima
Ukiona familia yenye msiba, tafadhali wafariji na ushiriki kuwasindikiza mashujaa wetu. Pia mlio na access tusaidieni kufahamu miili inayotolewa mortuary inapelekwa wapi. Asante.
Shebi tumezunguka hospital zote hapa DIZIMU kukutafuta lakini hatujakupata, bimkubwa anasema hata akipata mwili wako inatosha akuzike mwenyewe.
Bimkubwa analia muda wote, naogopa hata kumthibitishia kuwa ulipigwa CHUMA mbele ya macho yangu.😭😭
Niliwaambia JWTZ lenu ni Hovyo Hawatashiriki Maandamano kuwasaidia wananchi kwenye Maandamano ya Kesho Order alipewa CDF na ahakikishe SSH anakua madarakani kwa vyovyote Tanzania kupata uhuru mpaka siku Yesu akirudi Maana hakuna mwananchi mwenye akili timamu sisi sote mazombie 🙅
#TANZANIA:WAZEE WA KIKURYA WATAKA JOHN HECHE AACHIWE,WASEMA HAWATAKI UGOMVI NA SERIKALI
Wazee wa Tarafa ya Inchugu wameitisha mkutano mkuu wa kijamii (litongo) wenye lengo la kuwasilisha kilio chao kwa Serikali, wakisisitiza kuwa kilio hicho hakina misingi ya kisiasa, bali ni cha jamii kwa ujumla kinachodai haki, amani na heshima kwa binadamu.
Wakizungumza katika tamko lao, wazee hao wamesema kuwa hawana ugomvi na Serikali, bali wanapinga vitendo vya utekaji, ukamataji holela na uonevu vinavyotokea dhidi ya vijana na viongozi wa jamii, ikiwemo kijana mmoja wao, John Heche, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (@ChademaTZ2 ).
Heche anashikiliwa kwa madai ya kuondoka nje ya nchi bila kufuata utaratibu wa kisheria.
“Vitendo hivi vinavuruga utulivu wa kijamii na pia kuathiri maendeleo ya uchumi wa mji wa Sirari,” wazee hao wamesema, wakiitaka Serikali kuchukua hatua za kulinda haki na ustawi wa wananchi, pamoja na kuhakikisha ulinzi wa raia na viongozi wa kijamii.
Tamko hilo limekuja katika hali ambapo jamii ya Wakurya inaonyesha wasiwasi juu ya hali ya ulinzi wa raia na heshima za binadamu katika maeneo yao, huku ikisisitiza kuwa amani na utulivu wa kijamii ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya miji midogo kama Sirari.