Unapata nguvu ya kushangilia yanayoendelea? Kwa sababu ya rangi ya bendera yako? Unashindwa kukemea ambayo yanatokea nchini kwetu?Tunalitengeneza taifa la hovyo sana, ambalo watu wanakwenda kuongozwa na watawala ambao hawakuchaguliwa na watu isipokuwa mamlaka. Uchaguzi wa hovyo.
Wakati tunaendelea kupokea taarifa za Uchafuzi kutoka maeneo mbalimbali nchini, huko Michenjele jimbo la Tandahimba ndugu zetu wamevamiwa tena na 'Wazee wa Kujitoa Muhanga' tuwaombee sana ndugu zetu maana mambo sio mambo.