Je, tuwekeze nguvu na muda zaidi katika kujifunza kwa waliofanikiwa pekee kwa sababu na sisi tunataka kufanikiwa?
La hasha, kuna mengi pia ya kujifunza kutoka kwa watu waliofeli kufikia malengo yao.
Kuna namna itasaidia kung'amua kipi tufanye na kipi tusifanye ili tufanikiwe.
Your life as a MAN is war, it carries an endless challenges and battles.
But one thing I can assure you is that, you are going to win it if you will never give up.
WE MUST WIN.✊️
Paka mwenye ndoto ya kuwa simba ni sharti apoteze hamu ya kula panya.
Ili kufikia hatua kubwa katika maisha yako, ni lazima ubadilishe tabia zote mbaya zinazokurudisha nyuma kimaendeleo.
Hakuna kitu kitabadilika kwenye maisha yako kama hakuna kitu utabadilisha.
Ukishamaliza elimu ya darasani, hapo unakuwa umeshaushinda ujinga na siyo umasikini.
Mtaa unakudai maarifa mengine na una njia zake tofauti na elimu yako ili uushinde umasikini.
Usibweteke na elimu ya darasani pekee, jiongeze kupata ujuzi mpya utakaokujenga kiuchumi.
Nisikilize mwanangu;
Siku ukifa watu watalia sana na kuomba ikiwezekana urudishiwe uhai na muumba wako ili uweze kuishi tena.
Lakini ukiwa hai hakuna ambae atakuzingatia wala kujali kuhusu wewe kwa mema.
Ishi maisha yako bila kujali watu watasema nini juu yako.
Siku nilipogundua kuwa unaweza kufanya kazi kwa bidii kubwa mno na bado ukaendelea kubaki kuwa masikini;
Ni siku hiyo hiyo niliyoanza kuomba na kuamini kuwa ni neema ya Mungu pekee ndiyo itufanikishayo kwenye harakati zetu na utafutaji wetu.
Ladies and gentlemen, brothers and sisters, don't ever get distracted again.
Remember the promises you made to yourself, get back on the right track.
God is with you!
Kila siku ni fursa mpya ya kupambania ndoto zako na kusudi lake wewe kuwepo hapa duniani.
Kumbuka hukuzaliwa bila kusudi maalum na haupo hapa duniani kwa bahati mbaya.
Ulimwengu utakukumbuka na historia yako itaandikwa kwa kile ulichokifanya duniani na kugusa maisha ya watu.
Why are you giving up, how can you give up on yourself?
Your family, relatives and your loved ones are waiting for you to win so that they can enjoy their lives.
Get up, keep grinding, keep fighting, keep hustling God is with you.
You are going to win, you must win.
Umaweza ukafanya kazi kwa bidii na bado ukabakia kuwa masikini wa ku kutupa (SAD TRUTH).
Hapo ndipo tunapohitaji kumuomba Mungu na kumtanguliza kwenye harakati zetu ili neema yake izidi kutufanikisha zaidi katika malengo yetu.
Haka ka ulimwengu huwa kana ushenzi fulani hivi;
Unahitaji mtu mmoja pekee wa kukuamini na atakaeziamini jitihada zako na malengo yako kwa ujumla.
Hawa ndiyo huitwa {Destiny Helpers}, kuwa makini na watu unaokutana nao na kukaa meza moja huwezi jua ni yupi atakaekushika mkono.
Hakuna atakaekuja kukusaidia, maisha yako ni jukumu lako mwenyewe.
Ulimwengu unahitaji matokeo na si visingizio kwa kile unachokipambania.
Endelea kupambania maisha yako 💪.