If you let people's perception of you dictate your behaviour. You will never grow as a person. But if you leave yourself open to experience, despite what others think. Then you will learn and grow
NIA NJEMA.
Kumheshimu Mungu wangu
Namtolea roho yangu,
Nifanye kazi nipumzike
Amri zake tu nishike
Wazo, neno, tendo lote
Namtolea Mungu pote
Roho, mwili chote changu,
Pendo na uzima wangu
Mungu wangu nitampenda,
Wala dhambi sitatenda.
Jina lako nasifia,
Utakalo hutimia.
Kwa utii navumilia
Teso na matata pia.
Nipe, Bwana, neema zako
Niongeze sifa yako. Amina.
ROZARI TAKATIFU, MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
1. Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
2. Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya jirani.
3. Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara.
4. Tendo la nne; Yesu anatolewa
hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
5. Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.
Ee Baba yetu Mungu mkuu,
Umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba, Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi, nikutii.
Naomba sana Baba wee,
Baraka zako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria
Nisipotee nisimamie.
Mlinzi Mkuu malaika wee,
Kwa Mungu wetu niombee,
Nitake nitende mema tu,
Na mwisho nije kwako juu. Amina.
Chalamila, unamtisha nani? Huna uwezo wa kutoboa hata dakika mbili tukipewa uwanja tuchape sparing? Unasema utatoa mashine? Nani ambaye hana hiyo mashine? Wewe bila ulinzi wa polisi ni debe tupu tu. Pingu? Usiwatishe raia. Hao wanaopiga makofi kwa ujinga huu wana ubongo kweli?
Salamu Maria umejaa neema. Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote. Naye Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu. Utuombee sisi wakosefu. Sasa, na saa ya kufa kwetu, Amina๐