MORUWASA ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mha. Tamim Katakweba leo Oktoba 29,2024 imekutana na kufanya mazungumzo na Mkandarasi M/S PNR Service Ltd kwa lengo la kuhakikisha mradi wa majisafi Mkambarani unakamilika na wananchi kuanza kunufaika na Mradi.
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA), leo Oktoba 03, 2024 wametembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) kwa ziara ya siku ya mbili kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma ya maji.
Mkurugenzi Mtendaji MORUWASA, Mha. Tamim Katakweba amekutana na kufanya mazungumzo ya pamoja na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Morogoro na kuweka mkakati wa pamoja wa kuboresha huduma ya vituo vya maji ya zimamoto 'fire hydrants'.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) imefanya kikao na Wananchi wa Mtaa wa Mbuyuni kata ya Kihonda Maghorofani kwa lengo la kuwashirikisha wananchi hao watakaonufaika na Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za maji Manispaa ya Morogoro
Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA) kupitia klabu yake ya 'Jogging' leo Oktoba 05, 2024 wameungana na vikundi mbalimbali vya mazoezi na wananchi wa maeneo mbalimbali Morogoro katika mbio za fupi zilizoandaliwa na Mhe. Mussa Kilakala.
Katika kuhitimisha ziara yao ya kubadilishana uzoefu wa huduma za maji na MORUWASA, watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA) wamepata elimu ya uhifadhi wa Mazingira na vyanzo vya maji
#kaributenamoruwasa
Watumishi wa MORUWASA wameendelea kuwa mfano bora katika kutunza na kuhifadhi Mazingira, ambapo leo Oktoba 1, 2024 watumishi wanaosherehekea siku zao za kuzaliwa kwa mwezi Septemba wameshiriki zoezi la Kupanda miti katika eneo la Bwawa la kutibu Majitaka Mafisa, Morogoro.
Timu ya Menejimenti ya MORUWASA ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mha. Tamim Katakweba leo Septemba 30,2024 imefanya kikao na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za maji katika maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na Mamlaka.