@comanchechiefIV@ElionaKimaro KKKT, rudini kwa Baba na Mama yenu, RC(Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume).
Hili ni Kanisa ambalo haliwezi kuyumbishwa wala kufanyiwa MATAMBIKO na yeyote yule awaye yote.
@lifeofmshaba Kila anayejiita ni kiongozi wa Dini katika nyakati hizi, ajitahidi sana kutunza kumbukumbu za matendo yake. Saa ikifika, kila mmoja atatakiwa kueleza, alikuwa upande gani wakati ule wa dhiki kuu? Hapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.
@Kishiwatz@HecheJohn Sina maana kwamba wote ni wapumbavu bali walio wengi ndo akina sisi wapumbavu. Tungekuwa tunajitambua angalau hata watu milioni 7 kati ya milioni sitini, tungekuwa tulishakomesha dhuluma kitambo sana.
@meamswahili@HecheJohn Saa ikifika jua kuchomoza, hata ukijifunika blanket ili usilione jua, lenyewe litaendelea tu kuchomoza, whether you like or not.
@Advocate_Jebra Shida ya Nchi hii si udhalimu wa watawala bali ni UPUMBAVU wa wanaotawaliwa. Watanganyika ni kama kuku wa kisasa. Hata wafanywe nini wataishia tu kulalamika na si kuchukua hatua. Kwa hali hii, hata aje mtawala wa namna gani lazima atakuwa walivyo waliopo sasa.
@godbless_lema Kama ni issue ya usalama, tungetarajia MAKANISA, MISIKITI, MASOKO, VITUO VYA USAFIRI, BAR, HARUSI na MIKUSANYIKO yote ingepigwa marufuku.
Bado kidogo CDM itakuwa Dini kuu ya makabila yote Tanzania kwa sababu viongozi wa CDM ni zaidi ya viongozi wengine wengi wa Dini. Huwezi kuwa na wanaojiita viongozi wa Dini wasiosimama katika Haki.
@godbless_lema Mnafanya kazi nzuri sana. Endeleeni kuwaamsha Watanzania. Unakuta watu wananyanyaswa na vijitu vidogo vidogo tu huko mtaani bila kujihami wala kuchukua hatua zingine zozote zile ili kupinga kuonewa. Mtu kama huyo ukimwambia ampambanie Lissu ili kupata haki yake, hawezi.
@godbless_lema Mh. Lema, kupitia mikutano yenu, waambieni watu waache UNYONGE na WOGA lakini pia amsheni akili zao. Kama jamii itajitambua na kuondokana na WOGA na UNYONGE, mtawala hata awe katili kiasi gani hataweza kuiburuza hiyo jamii.
Watu wasikubali uonevu mdogo mdogo kule mitaani.
@HildaNewton21 Dada Hilda, kitu kingine ni kwamba, wanaume wa siku hizi wamekuwa UJI UJI mno. Zamani ilikuwa ukinishida nguvu ukanipiga leo, nakwenda kujipanda. Siku isiyo na jina nitakusulubisha mpaka hutaamini. Ilikuwa ukishafanya hivyo, hakuna mpumbavu atathubutu kukuonea tena.
@HildaNewton21 Mimi narudia kusema tena na tena kwamba, shida si watesi bali ni wateswa. Inawezekanaje mtu wa kijijini hapo hapo anakutesa halafu unakubali kuteswa kijinga namna hiyo?
Kwangu mimi, issue si kupigwa, bali ni Je, aliyepigwa atamchukulia hatua gani mtesi wake?
Mh. John Heche pamoja na wapambanaji wengine wote walio mstari wa mbele, pongezi kwenu.
Mngeweza kukaa kimya, kuungana na wadhalimu au kwenda kuishi ughaibuni. Lakini mmesacrife maisha yenu kwa ajili ya Watanzania. Mungu mkuu na Mungu mwenye nguvu, awalinde na kuwabariki.