#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 11,
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa naomba nizungumzie kesi yenyewe sasa.
Kwa kuanzia baada ya kusikiliza information ilivyosomwa yote baada ya kusoma haya maelezo yote.
Cha kwanza ninachoweza kusema ni kwamba
Hapa hakuna uhaini.
Pili hapa hakuna kosa lolote la jinai.
Hakuna uhaini na hakuna kosa lolote la jinai.
Mashitaka yanasema nimefanya kosa la uhaini.
Kifungu cha 39(2) (d) cha penal code kinatengeneza kosa la aina gani?
Ni kweli mimi ni raia wa Tanzania lakini nia ya kufanya uhaini ni kuzuia uchaguzi, kuvuruga uchaguzi, imesemwa imerudiwa imerudiwa.
Je kuzuia uchaguzi ni kosa la uhaini? Au wanasema wakiyatoa wapi?
Kifungu cha 39 kinasemaa uhaini ni kutishia Bunge, Serikali na Bunge.
Kuzuia Uchaguzi sio uhaini.
Kwa sheria za Tanzania kuhamasisha kuzuia Uchaguzi sio uhaini labda wawe na sheria zao binafsi huko sirini.
Sheria ya Uchaguzi imetengeneza makosa ya Uchaguzi imeandikwa kiswahili.
Hakuna kosa linaloitwa kuzuia uchaguzi.
Hakuna kosa la kuvuruga uchaguzi.
Sio jinai kwa mujibu wa sheria.
Nashangaaa inakuwaje uhaini kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi?
Hebu nyie mawakili wa serikali mseme inakuwaje uhaini?
Mheshimiwa utakumbuka tangu mapema kabisa kwamba hii kesi sio kesi ya kwanza ya uhaini Tanzania ni kesi ya nne.
Kwahiyo tunayo Precedent ya Mahakama ya afrika mashariki na mahakama ya rufani ya Tanzania zote zinaeleza kuhusu mambo ya uhaini.
Tunamuomgozo wa kesi ya uhaini inavotakiwa kuwa na Muongozo wa Mahakama ya rufani on how to frame a charge of treason.
Mwongozo unasema pawe na statement of the offence, particulars and overt act hiyo nia iwe na tendo la wazi.
It must be pleaded, Utekelezaji lazima uwepo na uelekezwe.
Wamekoroga mashitaka hayaeleweki, haijulikani overt act ni ipi? Walichokifanya hapa ni mkorogo maana hakuna charge hapa.
Jambo lingine muhimu kuhusu hii information ni kwamba maelezo Mheshimiwa Lissu alisema alisema alisema.
Swali ni kwamba Je maneno peke yake yanatengeneza uhaini? Maneno matupu yanatengeneza uhaini?
Kwa mujibu wa mahakama ya rufani Khatibu Gandi ilisema maneno matupu hayatengenezi uhaini isipokuwa yanatengeneza kosa la uhaini.
Kuzuia uchaguzi sio kosa la uhaini na sio kosa la jinai.
Hakimu anasema mimi pia leo nitapata relief wewe kuondoka kwenda mahakama kuu kwahiyo naomba naomba ujielekeze pia kwako na wewe utunze muda.
Mhehsimiwa naomba niendeleee nisipotezewe muda tafadhali sana.
Je Tundu Lissu peke yake anatosha kutenda kosa la uhaini?
Hili kosa nimeshtakiwa peke yangu na hakuna mtu mwingine kabisa.
Kwanza sheria inataka nifanye publication kwa watu wengine kuhusu huo uhaini na mipango yake. Sasa mimi hakuna mahali nimefanya publication. Wanasema JAMBO TV ndio walichapisha hayo maneno.
Hakuna aliyesema kuwa Tundu Lissu amemtishia Rais, Bunge au mahakama? Hakuna hata mmoja amesema hivyo. Wote wamesema tutazuia uchaguzi tutafanya vurugu.
Pia maelezo ya mashahidi hakuna aliyesema zaidi ya maneno niliyosema nilitenda kitendo kingine chochote. Hakuna aliyesema hata mmoja.
Part 12, itaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako.
@fezoomaster 2021 jamaa walikata kulitwa 500k niliwashangaa kumbe na wao walishangaa wanaokubali 500k
Ila nilisha waelewa unajitafuta ni Hela ya kuanzia ila umejipata kiasi siyo Hela ni utumwa Tu kuamka ahsubuhi kwa 500k
@ze_mandevu Nilishawishika kuanzia kucheza ila gafra Moyo uukakataa nikaachana nayo ila kuna Rafiki zangu Kila siku wanakula Hela zao likiwakuta la kuwakauta kwisha