. @HecheJohn Keep standing with the people……….. WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE!!!!!!!!!!!!!
Wewe na Lissu mnashikilia ndoto zetu na matumaini yetu. Kila kitu tumeweka kwenye mikono yenu nyinyi wawili.
Please msituangushe,
Sisi hatutaki maridhiano na waliotuua kabla ya uwajibikaji na ukweli wa October 29. Hatutaki na hatutayatambua maridhiano ambayo hayatosimamiwa na International community. Na bila Tundu Lissu mezani kutuwakilisha Watanganyika hatutatambua maridhiano yoyote. Na wakimnyonga ndio wasahau kuna kitu kinaitwa maridhiano kitakaa kitokee Tanzania. THIS IS A PROMISE!!!!! Ni itakuwa mtifuko mpaka milele!!!!!!
@HecheJohn Sisi wananchi tuliopigwa risasi kama mbwa hatutaki kupeleka pole wala rambi rambi kwa shetani wa miguu miwili alietuua kama kuku.
Tuko tayari kuishi kwa chuki na mshike mshike mpaka haki itakopatikana ila katu hatutaki amani ya kinafki na waliotuua ili washikilie madaraka bila idhini yetu.
Na katu hatutokubali statement za ‘Let Love lead’ tunataka statement za ‘LET JUSTICE LEAD’. Love iliisha October 29 2025, sasa kinachotafutwa ni haki. Haki ikipatikana Love itakuja yenyewe.
Na katu hatutokubali kumtambua Samia Suluhu kama Rais wa Tanzania au serikali yake kama serikali halali.
Huu ndio msimamo wa wananchi, NAWASILISHA!!!!!!
OFFICIAL ANNOUNCEMENT TO THE WORLD
We, the Tanzanian people, do not recognize Samia Suluhu Hassan or Deo Ndejembi as the legitimate President and Vice President of Tanzania.
No legitimate election was held on October 29, 2025. Instead, what happened was a systematic campaign of mass killings, with more than 10,000 Tanzanians killed during a five-day internet shutdown.
Any government that recognizes these two individuals as the legitimate leaders of Tanzania is turning its back on the Tanzanian people and standing against their demand for justice, democracy, and accountability.
Those responsible for these atrocities must be held accountable. The blood of Tanzanians cannot simply be ignored, and the victims and their families must not be forgotten.
We call on the international community to stand with the Tanzanian people as we fight for:
A new, democratic Constitution
A genuinely free and fair election
An end to killings, kidnappings, arbitrary imprisonment, and sexual torture
An end to the suppression and muzzling of the independent media
Full accountability and justice for the victims
Tanzania belongs to its people.
We will continue to demand democracy, freedom, justice, and a government that derives its legitimacy from the will of the Tanzanian people.
The world must stand with the people of Tanzania.
KISWAHILI
TANGAZO RASMI KWA ULIMWENGU
Sisi, Watanzania, hatuwatambui Samia Suluhu Hassan wala Deo Ndejembi kama Rais na Makamu wa Rais halali wa Tanzania.
Hakukuwa na uchaguzi halali uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025. Badala yake, kilichotokea ni kampeni ya mauaji ya halaiki yaliyopangwa na kutekelezwa kwa utaratibu, ambapo zaidi ya Watanzania 10,000 waliuawa wakati wa kukatika kwa intaneti kwa siku tano.
Serikali yoyote itakayowatambua watu hawa wawili kama viongozi halali wa Tanzania inawageuzia kisogo Watanzania na kusimama kinyume na madai yao ya haki, demokrasia na uwajibikaji.
Wale waliohusika na ukatili huu lazima wawajibishwe. Damu ya Watanzania haiwezi kupuuzwa, na waathirika pamoja na familia zao hawapaswi kusahaulika.
Tunaiomba jumuiya ya kimataifa kusimama pamoja na Watanzania tunapopigania:
Katiba mpya ya kidemokrasia
Uchaguzi huru na wa haki
Kukomeshwa kwa mauaji, utekaji nyara, kufungwa kiholela na mateso ya kingono
Kukomeshwa kwa ukandamizaji na kunyamazishwa kwa vyombo huru vya habari
Uwajibikaji kamili na haki kwa waathirika
Tanzania ni ya Watanzania.
Tutaendelea kudai demokrasia, uhuru, haki na serikali inayopata uhalali wake kutokana na matakwa ya wananchi wa Tanzania.
Ulimwengu lazima usimame pamoja na wananchi wa Tanzania.
Niliwaambia na ninawaambia tena maCCM na machawa kuna siku mtaelewa kazi hii mnayoita “kupiga kelele” ina manufaa gani
Uzuri kabla hajatekwa na kuwekwa kizuizini Nchimbi alionyesha kuelewa kuwa wanaharakati hatuna ubaya na tunatakia mema nchi yetu!
Sasa ni hivi Samia Suluhu - acha kuonyesha weakness na MWACHIE Emmanual Nchimbi
Najua unaogopa atatoa siri zenu kama Polepole ila ulitakiwa kuwaza haya kabla hukuanza vita hivi vya ndani! Nchimbi kumteka na kupanga kumpa uhaini ni UDHAIFU mkubwa na mwisho wako kimataifa hata wale uliokuwa unawaomba waje wakusaidie hawaji - unaji isolate kabisa!
Kesi tu ya Lissu imekulemea unatoa milio unaongeza na hii? 🤣
Tunasema Free all political prisoners na sasa Nchimbi amekuwa political prisoner wako kama Polepole huko CCM
Shida CCM mnakaa kimya kuhusu Nchimbi na ninyi mtafikiwa! Mzee Warioba ameshawaonya!
Nauliza tena kwa hiyo tukiondoa wastaafu, pamoja na Polepole na Nchimbi na Gwajima - huko CCM hakuna wanaume mmebaki? Maana mnaendeshwa na genge la wafiraji na makatili na mko KIMYA na kugonga meza! Shameful!
#TutaelewanaTu #SamiaMustGo
Bila kusahau SPECIAL S/O leo kwa Mzee wetu "Mama Anna Tibaijuka." Umetuwakilisha vyema sana.
Leo kuna kauli kaiongea kwamba "Wakina HECHE wanapigana vita ngumu kuliko hata ya NYERERE kulikomboa hili taifa kutoka kwa Mkoloni".
Hili niliwahi kusema na nimefurahi Mzee wetu kulichambua kwa kina. Kiukweli kabisa MAPAMBANO YA LISSU & HECHE kwenye hili taifa siku moja yatasomwa na vizazi na vizazi.
Tunayo BAHATI NZURI KUYAONA lakini pia tunayo BAHATI MBAYA kuyaishi maana hakuna ambae hafikiwi na maumivu makali ya haya mapambano.
Tutashinda na TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Prof Tibaijuka aliniambia tuna kazi ngumu kuliko ya Mwl Nyerere.
Nyerere alipambana na wakoloni kwanza walikua wanafuata sheria.
Lakini hawa wakoloni weusi hawafuati sheria.
Wakaloni walikua hawatoi rushwa.
Wakoloni weusi wanahonga kila mtu.
Ukweli ni kwamba tutawashinda hata wakitumia nguvu gani.
"Chimbuko la matatizo haya ni uchaguzi na watu wanaotaka kubaki madarakani kwa njia ambazo si za kikatiba, tusipotatua hilo nchi hii itazalisha wakimbizi." Mhe. @HecheJohn
Huwa wanasahau hawa wauaji kuwa mi ni mwandishi wa habari tena mzuri tu - na wa kufukunyua
Nchi isingekuwa ya kiwaki ningekuwa top investigative journalist
😁🙌🏽
Acha ikae hivyo!
#TutaelewanaTu
Uchaguzi wa CHADEMA wa 2025 ulipaswa kuigwa.
Na pengine watawala walipaswa kuwauliza viongozi wa CHADEMA waliweza vipi kufanikisha Uchaguzi HURU na HAKI ??
~Jenerali Ulimwengu.
Jambo la kutisha zaidi, sio M/ Rais kujiuzulu kwa namna ya sintofahamu, bali ni kuchukiwa kwake kwa kauli ambazo ni very positive kwa maslahi ya taifa. Yaani kuchukiwa kwa sbb ya kutamka katiba mpya, kupinga mambo ya kuumizana, kuwataja wanaharakati positively, inatisha sana.
Jaji Warioba: Tusipoangalia tutajikuta wakimbizi
Akizungumza katika Jukwaa la Demokrasia, leo Agosti 28, 2026, Jaji Joseph Warioba ameonesha kutokuona uwezekano wa Katiba Mpya kupatikana kabla ya uchaguzi wa 2030.
Warioba ameeleza kuwa mlolongo wa tume mbalimbali unaonesha lengo ni kusahaulisha yaliyotokea Oktoba 29, jambo ambalo ameeleza ni vigumu kutokea.
Warioba ametahadharisha kama nchi ikiingia kwenye uchaguzi wa 2030 bila Katiba Mpya, kuna uwezekano wa kuwepo kwa mlipuko.
"Mimi naona kama hizi tume,ni kama utaratibu wa kwenda mpaka tusahau, lakini yaliyotokea mwaka jana huwezi kusahau. Na tusipoangalia sisi tulikuwa tunasifika kwamba ni nchi ya amani, majirani zetu wengi walikuwa wanakuja kupata hifadhi hapa, kwa sababu kwao hakukuwa na amani. Kama tusipoangalia tutajikuta wakimbizi kwenda mahali fulani," anaeleza Warioba.
Warioba ametoa pendekezo kuwepo na kipindi cha mpito, ambapo marekebisho katika Katiba yatafanyika, kuangazia maeneo matano ikiwemo mgawanyo wa madaraka, muungano, uchaguzi, maadili ya umma, pamoja na mgombea binafsi.
VIDEO:
Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa katika mapambano ya kuleta mabadiliko nchini kwa muda mrefu, akilinganisha juhudi hizo na mapambano ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza leo katika Jukwaa la Demokrasia, Profesa Tibaijuka amesema mapambano ya Mwalimu Nyerere ya kudai uhuru wa Tanganyika yalidumu kwa takribani miaka 7, kuanzia mwaka 1954 hadi 1961, wakati CHADEMA imekuwa ikiendelea na mapambano yake kwa muda mrefu zaidi.
“Hawa wenzetu juhudi inaendelea, tuwape nguvu, lakini kazi ni ngumu kwa sababu kubadili 'establishment' ya ndani, mjue ni ngumu kuliko kuwabadilisha 'external establishment',” amesema Profesa Tibaijuka.
Aidha, Profesa Tibaijuka amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inaweza kufanyiwa mabadiliko ili kutoa nafasi zaidi kwa demokrasia, ikiwemo suala la usajili wa vyama vya siasa akitoa mfano kupitia vijana wanaojaribu kusajili chama cha siasa lakini wamekumbana na vikwazo, huku akieleza kuwa suala hilo sasa liko mahakamani.
“Sasa ngoja niwaambie nyie Wanasheria, wameshindwa hawa vijana, wanataka kuandikisha chama cha Siasa, wamewekewa mizingwi, sasa hivi wako Mahakamani wanapambana,” amesema.
Miongoni mwa mabadiliko aliyopendekeza Prof. Tibajuka kwenye katiba ya 1977 ni pamoja na mabadiliko ya uandikishaji wa Vyama vya siasa pamoja na suala la uraia pacha.
UJUMBE WA MANGE KIMAMBI
1. GEN Z, LEO MMEKUWA VINDICATED! Mpaka wazee sasa wamejoin movement yenu ya kudai haki………
2. Kama hali hii itaendelea Tanzania basi nawahakikishia ndani ya 5-10 years itaibuka armed group Tanzania. Historia inakwambia hili……
3. Jeshi la JWTZ, JESHI LA POLISI NA USALAMA WA TAIFA - VIMETEKWA KAMA CCM ilivyotekwa……
1. GEN Z, LEO MMEKUWA VINDICATED! Mpaka wazee sasa wamejoin movement yenu ya kudai haki………
2. Kama hali hii itaendelea Tanzania basi nawahakikishia ndani ya 5-10 years itaibuka armed group Tanzania. Historia inakwambia hili……
3. Jeshi la JWTZ, JESHI LA POLISI NA USALAMA WA TAIFA - VIMETEKWA KAMA CCM ilivyotekwa……
Nachoshukuru hakuna tena mtu anaongolea maridhino….
Kila mtu kaanza kuelewa kuwa maridhiano is impossible na hii Serikali batili….
Sasa tupambane mpaka tupate haki….