Ahsanteni sana Kigoma.
Kigoma ni Mkoa wa Kimkakati, na kuthibitisha hilo tumeleta shilingi trilioni 11.4 kwa ajili ya miradi ya kijamii na kimaendeleo. Hiki ni kiasi kikubwa zaidi cha fedha kuwahi kutolewa na Serikali kwa mkoa huu.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuthibitisha kuwa ndicho chenye uwezo wa kupanga, kusimamia na kutekeleza mambo makubwa na yenye manufaa kwa wananchi. Kwa miaka mitano ijayo, tutaongeza kasi katika utekelezaji wa miradi na kufungua fursa zenye manufaa kwa wananchi, mkoa huu na Taifa letu.
Ninawapongeza wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioteuliwa kugombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.
Ninawatakia kila la kheri katika maandalizi ya safari yenu ya kwenda kuomba ridhaa ya wananchi kupitia sanduku la kura, kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2025.
Mwenyezi Mungu awatangulie, awaongoze na kuwafanikisha.
👉 “Sheria iko kwa ajili ya wote, si wachache.”
Maana ya ujumbe huu:
Sheria haikutungwa kwa ajili ya kundi dogo la watu au wenye nafasi fulani pekee, bali ipo kwa ajili ya wananchi wote bila ubaguzi.
Kila raia ana haki ya kulindwa na sheria na pia wajibu wa kuifuata.
Hakuna mtu aliye juu ya sheria; wote ni sawa mbele ya sheria.
Ujumbe huu unahamasisha wananchi kutambua kuwa wanapohitaji msaada wa kisheria, si upendeleo bali ni stahiki yao kwa mujibu wa sheria.
Kupitia kampeni hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inahakikisha kuwa huduma za msaada wa kisheria zinapatikana bure kwa wananchi wote, hususan wale wa kipato cha chini, ili kutekeleza dhana ya sheria kwa wote na si wachache.
#WizaraYaKatibaNaSheria #HudumaKwaWananchi #MamaSamiaLegalAid #SSH #kazinaututunasongambele #matokeochanya #SioNdotoTena #HakiKwaWote #HakiSawa #MsaadaWaKisheria #SheriaNiNguvu #ElimuYaSheria #SisiniTanzania #nchiyangukwanza #TanzaniaNiwajibuwetu #Nchiyetufahariyetu #tanzania
👉 “Haki si zawadi, ni haki ya kila mwananchi”
inaweka wazi kuwa kila Mtanzania ana stahiki ya kupata haki bila ubaguzi. Haki hizo si zawadi ya mtu binafsi wala taasisi, bali ni wajibu wa kikatiba na kisheria kwa kila raia kuzipata na kulindwa nazo.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndiye mlezi mkuu wa kampeni hii. Kupitia uongozi wake, Serikali imehakikisha huduma za msaada wa kisheria zinapatikana bure kwa wananchi hasa wale wa kipato cha chini, ili kuhakikisha hakuna anayekosa haki kwa sababu ya ukosefu wa fedha au uelewa mdogo wa sheria.
#WizaraYaKatibaNaSheria #HudumaKwaWananchi #MamaSamiaLegalAid #HakiKwaWote #HakiSawa #MsaadaWaKisheria #SheriaNiNguvu #ElimuYaSheria #SisiniTanzania #nchiyangukwanza #TanzaniaNiwajibuwetu #Nchiyetufahariyetu #tanzania #SSH
👉 “Usinyamaze, haki yako inaanza pale unapoinua sauti.”
Ujumbe huu unahimiza wananchi kutokaa kimya wanapokosa haki au wanapokutana na changamoto zinazohusu maisha yao ya kisheria na kijamii. Kukaa kimya ni kuruhusu kunyimwa haki, lakini kuzungumza na kudai ni hatua ya kwanza ya kuhakikisha haki inapatikana.
Kampeni hii inalenga kuwaelimisha wananchi wote kwamba Serikali kupitia Mama Samia Legal Aid Campaign ipo kwa ajili ya kuwasaidia bila malipo, kuhakikisha kila mmoja anapata msaada wa kisheria pale inapohitajika.
#WizaraYaKatibaNaSheria #HudumaKwaWananchi #MamaSamiaLegalAid #HakiKwaWote #HakiSawa #MsaadaWaKisheria #SheriaNiNguvu #ElimuYaSheria #SisiniTanzania #nchiyangukwanza #TanzaniaNiwajibuwetu #Nchiyetufahariyetu #kazinaututunasongambele
Mapema leo jijini Dodoma, nilipoongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa.
Vikao hivi ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya chama kupata Wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Viti Maalum, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum; kabla ya uteuzi wa mwisho utakaofanywa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) pamoja na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), na kisha kwenda kuomba ridhaa ya wananchi kwa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025.