Leo nimemkaribisha nchini Dada yangu, Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mheshimiwa Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, aliyefika nchini kwa ziara ya kitaifa, ikiwa ni ziara yake ya pili baada ya ziara aliyofanya Mei 2025. Kwake, Tanzania ni nyumbani, kwani aliishi hapa mwaka 1980 hadi 1986, akishiriki harakati za kupigania uhuru wa Namibia.
Licha ya ukubwa wa historia yetu, ushirikiano wetu wa kiuchumi ni mdogo. Kwa msingi huo tumekubaliana kukuza ushirikiano katika maeneo ya kimkakati ikiwemo biashara na uwekezaji, uchumi wa buluu, usalama wa chakula, ulinzi, usafiri wa anga, pamoja na nishati, mafuta na gesi. Kwa kuanza, nchi zetu zimesaini hati nne za makubaliano ya ushirikiano, hivyo ninawasihi wafanyabiashara kutoka pande zote kuchangamkia fursa hizo.
Aidha, ninatoa rai kwa watendaji wa nchi zetu katika ngazi zote kuhakikisha yote tuliyokubaliana leo, na wakati wa ziara iliyopita, yanatekelezwa kwa wakati ili kuchagiza maendeleo ya nchi zetu na ustawi wa wananchi wote.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa, Keffi nchini Nigeria kwa njia ya mtandao, tarehe 11 Aprili, 2026 Ikulu, Dodoma.
Mhe. Rais ametunukiwa Shahada hiyo ya Uzamivu ya Heshima kwa kutambua mchango wake kama Kinara wa Nishati Safi ya Kupikia, Afya ya Mama na Mtoto, Taswira nzuri katika masuala ya Uongozi kwa Wanawake Afrika na Kusimamia Masuala ya Biashara hususani kwa Vijana Afrika.
Pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika, nimekuwa na wakati mzuri kuzungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia, Mheshimiwa Abiy Ahmed Ali.
Tanzania na Ethiopia zina uhusiano wa kihistoria na ushirikiano katika maeneo ya kimkakati ikiwemo usafiri wa anga, nishati, kilimo, mifugo, biashara, uwekezaji pamoja na ulinzi na usalama. Tutaendeleza ushirikiano huu ili kuchochea maendeleo kwa manufaa ya wananchi wetu.
@Sativa255 Kiuungwana nadhani sativa ungeanza kwa kuwapongeza madereva na wataalamu kwa kuona tatizo na kuamua kutopeleka treni ili kuepuka maafa. Pia madaraja yanatengezwa kwenye mito ipi? Maana hausemi ubora au ubovu wa daraja badala unalalama daraja kujengwa kwenye mto mkubwa. Toa hoja
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025.