WANANGU, Tuwe busy tupambanie maisha yetu, wao ajira zao zipo ndani ya nguo zao wengi wao, sisi ajira zetu zipo ndani ya jasho letu mpaka mwisho Mwanangu. TUWE BIZEE.
Watu wanaweza kukutia moyo, lakini hawataweza kubeba ndoto zako.
Nguvu ya kweli iko ndani yako katika nidhamu yako, maamuzi yako, na hatua zako za kila siku.
Kuna siku utachoka, utapoteza hamasa… lakini hapo ndipo unapotakiwa kuendelea zaidi.
Kwa sababu hakuna mtu atakayekutaka ushinde kama wewe unavyotakiwa kutaka kushinda.
Mtu akiambiwa achugue kimoja wapo kati ya Ajira na biashara wengi huwa wanakimbilia ajira ila kiufupi ajira huwa zinakuwa ni ngumu Biashara inakupa uhuru wa kuishi
Wakati wao wanatoa chafu wavae safi waende makazini, sisi tunatoa safi ili tuvae chafu nasi pia tuingie kazini.. katika hayo yote kamwe usichukulie poa mahali unapatia Ridhki✍.
Ivi serikali ikataka kupunguza umaskini kwa wananchi wa nchi yake ifanye kipi ambacho kitasaidi👇
1️⃣Kuongeza mishahara kwa waajiriwa?
2️⃣kuwapa wananchi mitaji?
2️⃣au kuwaandalia masoko na sehemu nzuri ya Kufanyia biashara?