#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 260
Mhe. Tundu Lissu anaendelea kutoa ushaidi wake
Anasema nilikuwa Msemaji Mkuu wa masuala ya katiba na sheria ya kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Masuala ya Muungano na nilikuwa shadow Attorney General.
Naomba Mahakama irekodi kwamba nilifanya kazi yangu kwa uaminifu mkubwa na umahiri mkubwa sana.
Waheshimiwa majaji katika kipindi cha 2011 hadi 2014 nilikuwa mjumbe maalumu wa Bunge la Katiba kwa kipindi hicho cha 2011 hadi 2015 niliongoza harakati za kupigania Katiba Mpya na mfumo huru wa uchaguzi, niliongoza hayo mapambano bungeni na kwenye Bunge la Katiba kwa uaminifu na umahiri mkubwa sana, hivyo ni ushahidi wangu kwamba kilichotuleta hapa ni mgogoro wa kisiasa, ni vita ya kisiasa na sio Uhaini.
Waheshimiwa Majaji nje ya ubunge nimekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kuanzia Machi hadi Septemba 7, 2017 na huwi Rais wa TLS kama wewe ni mtu wa hovyo hovyo mhaini mhaini.
Nje ya uongozi wa mawakili wenzangu hapa nilipo ni Makamu Mwenyekiti wa Internationa Democrats Union (IDU).
IDU ni muungano au shirikisho linalojumuisha vyama karibu 80 kutoka dunia nzima.
Mimi pia ni mjumbe wa International Executive Committee ya IDU, mimi ni Makamu Mwenyekiti ninayewakilisha bara zima la Afrika
Waheshimiwa majaji ni ushahidi wangu kwamba mimi ni mtu wa heshima ndani ya nchi hii na kimataifa na heshima niliyonayo ni kutokana na msimamo wangu wa kupigania Demokrasia, Haki za binadamu na Utawala wa sheria sio kwasababu nyingine.
Waheshimiwa Majaji mwezi Mei 2011 nilipewa tuzo ya heshima ya kuwa mwenza wa kimataifa wa Chuo Kikuu cha Bridgeport (International Fellow) jimbo la Connectcut lilipo nchini Marekeni, walisema ni kwasababu ya kupigania haki za binadamu, mazingira na demokrasia katika nchi ya Tanzania na Barani Afrika.
Mwezi Desemba 2020 nilitunukiwa heshima nyingine na IDU tuzo inayoitwa Bush Thatcher Award Freedom (kwa jina la Rais wa 41 wa Marekani) sababu yake au citation yake ilisema Tundu Lissu umekuwa ni kielelezo cha msimamo thabiti wa kupigania Haki, Demokrasia na Utawala bora katika nchi za Afrika.
Ni muhimu vilevile iingie kwenye ushahidi kwamba pamoja na kukaa gerezani kwa muda wote, heshima yangu ndani na nje ya nchi haijapungua in fact imeongezeka.
Taasisi nyingi sana za kitaifa, kikanda na kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ulaya, Jumuiya ya Madola zimesema haya mashtaka ni mashtaka ya kisiasa hakuna jinai yoyote na wamedai niachiliwe huru bila masharti yoyote.
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limeeleza sio tu kwamba niachiwa bali nilipwe pia fidia kutokana na usumbufu wote uliojitokeza tangu nilipokamatwa.
Waheshimiwa Majaji naomba iingie kwenye ushahidi kwamba nchi za Jumuiya ya ulaya zimesimamisha misaada kwa Tanzania kwasababu ya mashtaka haya, takribani dola million 700 nchi ya Marekani imesimamisha kwa Serikali ya Tanzania kwa takwimu nilizonazo kwasababu ya mashtaka haya.
Bunge la Marekani linajadili muswaada wa kuiwekea serikali ya Tanzania na Viongozi wake vikwazo kwasababu ya mashtaka haya.
Waheshimiwa majaji dunia haiwezi ikakupigania hivi kama wewe ni mtu wa hovyo hovyo
Watu wanatabasamu sana na kucheka 😂😂😂😂😂😂
Mhe. Lissu anaendelea kusema Dunia inaweza kukupigania hivi kama wewe ni mtu wa heshima.
Part 261 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
Kwa hali hii kodi za watanzania hazitaachwa kuliwa, kama Bimsumi anakiri kabisa hajui pesa ngapi zinatolewa na serikali yake haramu hadi akifika kuzindua mradi, jiulize tumepigw ngapi
Ni uozo kila mahali
“Mchakato wa Katiba uanze ilipokwamia rasimu ya Warioba kwa kutumia Kamati ya Wataalamu kama walivofanya wenzetu Kenya na ikawaasaidia kutoka kwenye mkwamo wa kutengeneza Katiba mpya”-; @ThobiasMessang1
Mkurungenzi wa Jukwaa la Katiba.
🚨 BREAKING:
Famous British comedian Mr. Bean:
I feel ashamed on behalf of the United Kingdom for allowing Israel to besiege two million people in Gaza, cutting off electricity, water, and medicine from them, and then claiming to defend human rights.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Afrika Kusini EFF Julius Malema amevishukia vyama tawala barani Afrika vilivyohusika na vuguvugu la uhuru ikiwemo CCM, ZANU-PF, SWAPO, FRELIMO na ANC kuwa kitakachowamaliza ni kifo cha asili ambacho hakikwepeki kwani havitaweza kujivua gamba ili kuendeleza ajenda ya ukombozi.
Mwaka 1991 Pepe Kalle na bendi yake ya Empire Bakuba walikuja Tanzania kufanya onesho katika jiji la Arusha. Walipowasili Arusha, walikodi taksi iliyokuwa inaendeshwa na mwanamama Hidaya Khamis Massawe.
Wakiwa kwenye taksi wakawa wanazungumza kilingala wakimsifia dereva bila kujua kuwa kumbe bi. Hidaya (dereva Taxi) alikuwa anakijua kilingala kwani kutokana na mihangaiko yake ya kimaisha huko Zaire (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo). Pepe Kalle akastaajabu sana kumsikia Hidaya anazungumza kilingala. Alipomaliza onesho lake Arusha, Pepe Kalle akajiapiza kurejea Tanzania kwa ajili ya Hidaya.
Mwaka uliofuata, 1992, Pepe Kalle akarudi kweli Tanzania Arusha na akatunga wimbo kwa ajili ya Hidaya. Mume wa Hidaya, Mzee Massawe, alipong'amua kuwa ule wimbo "Hidaya" umetungwa mahsusi kwa ajili ya mke wake, alimpa talaka siku hiyo hiyo.
Hidaya khamis masawe alifariki mwaka 2021 Arusha, Mtaa wa Kaloleni.
CHANGIA BARAZA KUU LA UMMA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Zinedine Zidane ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Ufaransa – Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) ⚽️
Yajue mambo muhimu juu yake:
🔹 Akiwa na umri wa miaka 54, ana asili ya Algeria. Mtoto wake aitwaye Luca Zidane anachezea timu ya taifa ya Algeria.
🔹 Katika kipindi cha uchezaji wake, Zinedine Zidane aliichezea timu ya Ufaransa zaidi ya mechi 100, akishinda Kombe la Dunia la 1998 na Euro 2000. Pia alitunukiwa tuzo ya Ballon d'Or mwaka 1998.
🔹 Kama kocha, aliongoza Real Madrid mara mbili (miaka 2016–2018, 2019–2021), na akaibuka na mataji matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
📄 Mkataba wake una muda wa miaka 4, kwa mujibu wa shirikisho.
Zidane anamrithi Didier Deschamps, ambaye aliiongoza "Les Bleus" kwa miaka 14. Timu ya Ufaransa ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye Kombe la Dunia la 2026, ikichapwa 0–2 na Uhispania.
📽️ Video kutoka mitandao ya kijamii: Zidane akiwasili kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kutangazwa kwa uteuzi wake.