Tunadate na watu ambao wametoka kimwili kwa "ex" zao lakini akili na moyo upo kwa "ex"
Tunadate na watu ambao hawajamaliza kupenda watu wao wa mwanzo tukitegemea kupata UPENDO
Leo imetimia miezi saba tangu Nduli Idd Amin Mama auwe kwa risasi Watanganyika zaidi ya elfu kumi.
Tunamuomba Mungu aendelee kuwapa pumzika la milele mashujaa wetu wote.🙏💔
Moja ya kitu kinaninyima usingizi recently ni hili swala la wanaharakati kuwa wanalipwa!! (Kama ni kweli)🤔
Hizo taasisi au watu binafsi wanaolipa wanaharakati, huwa wanatazama vigezo gani kukulipa?
Influence? au Numbers (Followers)
au uwezo wa kuongea na kuandika au engagement ya social media au nini?
Binafsi nimeanza hii course ya harakati tokea siku namaliza form six na kutoa wimbo wangu wa kwanza Tanzania (2007) nikiwa very young!
Hadi leo nina Teremsha bunduki 2026!
Miaka 19 kwenye hizi harakati
NA SIJAWAHI KUPEWA HATA SHING 10 TOKA KWENYE HIZO TAASISI!!
WALA KULIPWA NA MTU BINAFSI ILI NIFANYE HIKI NINACHOKIFANYA!!
Na kuna muda unakuwa na uhitaji haswa, tena sometimes ni uhitaji wa kufanya projects hizi hizi za kusaidia hizi harakati….. you just end up using your own pocket money!!
Kwenye hizi harakati nakutana na challenge nyingi, nakosa opportunities na michongo kwasababu naonekana niko against na gavoo na kuna muda napoteza hata kidogo nilichobakiza!!
Nabaki empty hadi familia inakwambia si utemane na hizo mbanga……nawajibu I WAS BORN TO DO THIS!!
Ni kama roho/nafsi inakataa ku-give up!!
Tunafanya haya kwa passion,
kuna a driving force tu inatusukuma kutetea, kukemea, kushauri na kupaza sauti tunapoona haki inakosekana, maendeleo hakuna, rushwa na ufisadi kwa viongozi vinakithiri, umasikini unazidi kwetu sisi raia, uongozi na utawala mbovu, shida za ajira na miundo mbinu, watu kutekwa, kufungwa na kuuliwa bila hatia na kucreate awareness kwa raia kuhusu issue za kisiasa na kijamii etc.
Nikisikia mtu anasema kuyafanya hayo ni unalipwa…..nawaza nakosa majibu!!
Wanatumia vigezo gani kukulipa?
Hebu mtu anieleweshe pengine napishanaga na gari la mshahara!!
Followers ninao (1.3M) influence pia si haba nikitoa miwa inapokelewa mtaani!! MBONA MIMI SILIPWI?
Nways tusiache hizi harakati hata kama hazitupi pesa kwa sasa, faida yake mbeleni ni kubwa zaidi kwa nchi nzima na vizazi vijavyo!!
Kama nimeandika kwa hisia sana ee?😁
Nimefikiri na kutafakari kwa muda mrefu baada ya matukio ya ukiukwaji wa haki, utu na dhuluma dhidi ya uhai wa binadamu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025. Siwezi kuendelea kuishi katika huzuni na ukimya tena.
Kwa dhamira yangu binafsi, leo nimejiondoa rasmi kutoka CCM na kurejea CHADEMA kwa kufuata taratibu zote za CHADEMA.
Kwa Watanzania wote, na wanachama wa CHADEMA wale walioumizwa au kukatishwa tamaa na msimamo wangu wa awali, naomba radhi kwa dhati pale nilipokuwa kinyume na matarajio yetu ya pamoja katika safari ya kutafuta haki, utu na demokrasia ya kweli.
Naam, binadamu hukosea, lakini dhamira inapozinduka ni wajibu kusimama upande unaouona kuwa wa kweli na wa haki.
Asanteni Sana.
Alafu kuna mtu anaweza kuzungumzia jambo kubwa kama hili kwa mzaha na lugha ya kawaida.
Ndugu zetu wengi hivi wameuwawa bila sababu!!!
Hii haitakubalika.
Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume linaendelea kutimiza wajibu wake wa kitume. Hili la kuwaombea waliopoteza maisha, waliojeruhiwa na waliopoteza ndugu na jamaa katika vurugu za uchaguzi mkuu ni ibada njema. Ahsante sana Mhashamu Baba Askofu, Jude Thaddaeus Ruwa'ichi, OFMCap, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania…🙏🏾
Jambo moja muhimu sana ktk safari yako ya kurudi katika kazi ya kudai mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli ni pale ulipotubu kuwa huko nyuma na wewe pia ulikosea sana. Toba hii ilikuwa muhimu sana kwako na familia yako. Ulikuwa ni msingi wa fikra ya Mwenyezi Mungu ndani yako. Sidhani kama bado huko hai !! Nina wasiwai sana. Lakini kisasi cha Mungu kinakuja kwa watesi wote wa Nchi hii. Kama sitakuona wala kukusikia tena , tafadhali, lala salama sana na Mungu awatie nguvu Mama yako , familia , ndugu , rafiki na jamaa wote. Hatukustahili Taifa la aina hii hata kidogo. Bado muda kidogo hasira ya kudai haki itaamka kwa kwa kila mwenye pumzi.