Asante MUNGU sijui ni kwanini na sijui kinacho kuja MBELENI wala kutokea Badae ila ASANTE MUNGU kwa kunipa nilicho subiri sana sijui nikipi ila ASANTE MUNGU🙏🏽🙏🏽
Kushare Mali nayo ni Ku risk.
Kuna dada huko kapewa sumu kafariki kisa mgogoro wa nyumba ambapo mume alidemand title deed isome jina lake ilihali mke ndie kajenga hiyo nyumba.
Tuwe makini Bora uitwe mbinafsi ila sharing ni risk .
Jpil kuna account moja Huko IG niliingia nikakuta video moja ikionyesha Russia na uzuri wake mi nikacomment "My Country"🙌 aisee DM yangu ni mwendo Wa "Привет, как дела? Мы можем быть друзьями?" 😂😂
Maombi yako hayajibiwi haraka kwasababu mahusiano yako na Nguvu ya Uungu yanakuwa mazuri pale tu unapokuwa na shida zako au za kimaisha. Sidhani kama wewe ungeweza kumsaidia kwa wakati mtu anayekukumbuka akiwa na matatizo tu. Nahisi ungemtaa kabisa. Badilika.
Dogo wa chuo anatembea na mke wa mtu na alishaonywa akakaza fuvu . Siku mwenye mke Amesafiri kama kawaida dogo akaingia.
Wamefanya Yao wamemaliza , jamaa huyu apa katinga na Chombo Cha moto plus silaha ya moto .
Dogo kuomba radhi akaambiwa sawa kimbia ujiokoe 👇👇
Ninaachia hofu, uvivu, na kila kinachonizuia kufikia potential yangu. Ninajenga maisha yangu kwa nidhamu, hekima, na uvumilivu. Kila hatua ninayochukua leo inanijenga kwa ajili ya legacy ya kesho.
Kati ya kundi linalokuja kwa kasi na halilizungumziwi ni hili la wanawake wanaoitana kwenye vikao na kuanza kuwafundisha wanawake wengine ujinga "usimuonyeshe mumeo mali zako coz wanaume ni matapeli" wewe mmeo unamuona kabisa anaipambania familia yake unabeba ushauri huo🙌🏾
Kadri unavyozidi kuwa na amani ya kweli/halisi ndivyo unavyozidi kuona na kugundua ni kiasi gani watu wanafake kuwa wana furaha na amani ilhali hawana na maybe hawajawahi kuwa nayo. Na weird part ni ukiwaambia ukweli ni wewe utaonekana unachanganyikiwa...
Si tu wenye shida huwa ni ndugu wa upande wa baba peke yao , hata hao ndugu wa kuzaliwa nao tumbo moja nao pia huwa ni wa hovyo na hawakutakii mema 🤔 .