Bagless choking overrated @KingJames will NEVER WITNESS @Sixers fans pay him this level of respect.
Ever.
Philly has ZERO RESPECT for front-running COWARDS like overrated Lebron.
This is why I laugh when people say Luka is “not athletic enough” to dominate NBA defenses. You don't need elite speed when your brain is operating two steps ahead of everybody else.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 288
Katuga: Pale ambapo kifungu cha Sheria kinatoa adhabu maneno kuwa shall be liable. Ni descretion ya Mahakama?
Mhe. Lissu: Hakuna descretion adhabu ni hiyo hiyo.
Katuga: Je uko aware na kesi ya Shed Mhagama
Mhe. Lissu: Wewe mwenyewe hapo unaangalia kwenye laptop mimi unataka niangalie wapi sasa?
Katuga: Omission na Contradiction maana yake nini?
Mhe. Lissu: Nipe kamusi nitakupa.
Katuga: Unataka Hadi kamusi?
Mhe. Lissu: Sasa umesema ni maneno ya kisheria. Sheria huwa inajibiwa kwa nyaraka nipe kamusi nikujibu.
Katuga: unaweza kutupa tafsiri ya mkanganyiko na kutokuwepo.
Mhe. Lissu: Mkanganyiko na jambo moja lina maelezo tofauti mawili na ommision ni kitu hakikuwepo ila kimeletwa.
Katuga: anaenda kupiga soga na wenzake pale.
Sasa tusaidie tafsiri ya kifungu cha 163 cha Evidence Act. Je contradicting ipo hapo?
Mhe. Lissu: Ipo ndio.
Katuga: Umewahi kufungua kesi kwa jina lako?
Mhe. Lissu: Nimefungua kupitia chama changu.
Katuga: Nimekuuliza wewe
Mhe. Lissu: We have done things, we have fought. Zipo vita nyingi tumepambana.
Katuga: Mambo ya Jaji Chande umesema mengi
Mhe. Lissu: Yapi ya Haki jinai au Oktoba 29?
Katuga: ya 29 nilisema. Alisema kuwa matukio ya tar. 29 yalipangwa na kupangwa kulitokana na masuala ya Uchaguzi.
Mhe. Lissu: Ndio tume huru na mengine
Katuga: Nakuheshimu kuna jambo sitaki kukwambia
Mhe. Lissu: Unaniheshimu wapi acha umbea. Unataka kuninyonga unasema unaniheshimu. Msingenishtaki kwa uhaini kama unaniheshimu.
Katuga: Taarifa ya Jaji Chande tume ile ilisema machafuko yale yalilenga kuzuia uchaguzi?
Mhe. Lissu: Hilo sijui nikumbushe.
Katuga: Je unakumbuka sana ulisema watatukamata watanifungulia kesi ya Uhaini.
Mhe. Lissu: sikumbuki. Nioneshe
Katuga: Ulisema Majaji ni MaCCM
Mhe. Lissu: Nakumbuka.
Katuga: nitakuwa sahihi hapo ndio nia ilianza kujengwa kwasababu mlisema muandamane ili mchukue dola
Mhe. Lissu: Sasa si yangekuwepo kwenye hati ya mashitaka hapo. Mbona hamkuyaweka hayo maneno?
Katuga: Waheshimiwa Majaji tunaomba D1 na zingine hadi D16 sasa muda umeisha. Sijui tunafanyaje?
Majaji wanaandika.
Jaji Ndunguru anasema Tunahairisha kesi hadi kesho saa tatu asubuhi.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 287
Katuga: Turudi kwenye masuala ya wanasheria sasa. Unaijua principle ya constructive possession unaifahamu?
Mhe. Lissu: Siifahamu labda niiambie.
Katuga: Kwamba mtu anaweza kukutwa na kitu ambacho hana lakini amekihifadhi kwa mtu fulani.
Mhe. Lissu: inawezekana ndio
Katuga: Unajua case laws unajua kitu kinaitwa constructive publication kwamba una knowledge na control?
Mhe. Lissu: Sasa mimi sikuwa na control ya publication hiyo ya Jambo.
Watu wanacheka.
Huyu KATUGA anapitia wakati mgumu sana. Majibu ya shahidi utadhani yeye ndio Wakili anamuuliza. Watu wanacheka
Katuga: Nani alisababisha publication?
Mhe. Lissu: Ni PW 17. Hakuna aliyemlazimisha kufanya publication. Angeweza kuamua asipublish.
Katuga: PW 17 alisema kwamba tulipaswa sisi kupitia wewe?
Mhe. Lissu: Sasa tatizo nyie Serikali mnasema nilipublish mimi wakati shahidi wenu alisema walipublish wao kupitia mimi. Huoni shida hapo wewe?
Naomba nikae mvua ya maswali ni kubwa. Watu wanacheka. Anakaa Mh. Lissu. Hajapoteza tabasamu lake lote.
Katuga: Ukitoa hotuba kila mtu ana haki ya kuitafsiri anavyoona mwenyewe?
Mhe. Lissu: Kweli.
Katuga: Maneno kwamba tutazuia uchaguzi, kila mtu ana haki ya kuzuia kwa kadri atakavyoona? Kuvuruga uchaguzi si kila mtu atavuruga anavyoona yeye inafaaa?
Mhe. Lissu: Kila mmoja abebe mzigo wake. Sio kazi yangu.
Katuga: Unakumbuka P3 alivyosema.
Mhe. Lissu: P3 ni nani wewe sema ni PW ngapi huyo P3 wako?
Katuga: PW 13 unakumbuka anasema walipanga kurushia watu mawe na kuzuia uchaguzi
Mhe. Lissu: Alisema ndio hayo ni yake.
Katuga: Uchaguzi upo kisheria?
Mhe. Lissu: Ndio lakini uchaguzi sheria zake zinasimamiwa na tume.
Katuga: Je kuwarushia mawe na kuwapiga watu ni uvunjifu wa amani?
Mhe. Lissu: Sio tu amani ni uvunjifu wa sheria pia.
Katuga: Hiyo mihimili mitatu nani ni custodian wa amani?
Mhe. Lissu: Ni jeshi la Polisi wako chini ya Serikali.
Katuga: Unapotishia kuivunja amani hivyo vitisho huwa vimelengwa kwa nani?
Mhe. Lissu: Swali lako ni la hovyo.
Katuga: Unapotishia unakuwa umelenga nani?
Mhe. Lissu: Nikimlenga huyu Bwana anamuonesha Dr. Nshala kuwa nikimtishia ninakuwa nimelitishia Jeshi la Polisi? Hapana.
Katuga: Waheshimiwa wameelewa tuache.
Mhe. Lissu: Lazima wawe wameelewa nafikiri sio vilaza.
Katuga: Kwenye hayo maneno kwamba mtazuia uchaguzi ulisema itakwua kidemokrasia?
Mhe. Lissu: Ungeleta masaa matatu yote ya hotuba ungeona hiyo Demokrasia.
Katuga: Upo tayari ikuamini unachokisema hiyo video uko tayari tukuoneshe?
Mhe. Lissu: Umeleta takataka mahakama ilikataaa. Mimi siwezi kuwasafishia takataka zenu. Mlileta mambo kienyeji yakakataliwa.
Katuga: Kwahiyo uko tayari tuyalete?
Mhe. Lissu: Mngeleta wenyewe. Mimi nitaitoa wapi hadi nilete.
Katuga: Sasa iambie mahakama demokrasia unayoifahamu wewe kila mtu ana haki ya kufanya anachoona kinamfaaa kwamba siku ya kupiga kura aende anayetaka na asiyetaka asiende. Ni sahihi?
Mhe. Lissu: Demokrasia yangu mimi inasema ukiwa hutaki jambo chukua hatua kulizuia kwa njia halali ndio maana maandamano yameruhusiwa kisheria.
Katuga: Demokrasia ipi hiyo?
Mhe. Lissu: Katiba inasema ukifanya maandamano na kuuzuia uchaguzi ni demokrasia kabisa. Niambie wapi sheria imekataza?
Katuga: Haya sawa mjanja wewe. 😂
Katuga: Katiba ndio imekupa mamlaka kufanya kuzuia? Soma ibara ya 30. Kwamba huwezi kutumia haki yako kuzuia haki ya mtu mwingine?
Mhe. Lissu: Kwanza nimesema kufanya fujo sio kosa lilipo mahakamani. Na katiba sio ibara 30 pekeee. Ziko ibara nyingi humo.
Katuga: haya maswali hayana nia yoyote mbaya si ndio Kaka angu?
Mhe. Lissu: Umenishtaki kwa uhaini unasema maswali yako hayana nia yoyote. Wewe vipi wewe?
Watu wanacheka. 😂😂😂
Katuga: Tuendelee au tuishie hapa shahidi?
Mhe. Lissu: Unaniomba ushauri? Mnyonga na Mnyongwaji tushauriane nini?
Part 288 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 286
Mhe. Lissu: Hiyo Section haipo hiyo lakini kifungu cha 10(2) ipo.
Katuga: Tutakesha hapa.
Mhe. Lissu: Nimekaa mwaka na miezi mitano. Naogopaje kukesha hapa?
Katuga: Anacheka. Haya twende kwenye mapesi. Wametumwa na wambura na kingai ulisema hivyo?
Mhe. Lissu: Ndio nimesema hao akina Wambura kuwa wamenionea muda mrefu.
Katuga: Kwahiyo wametumwa si ndio? Umesikia au umejuaje?
Mhe. Lissu: Wamesema kwa maandishi wenyewe. Wameni persecute kwa muda mrefu sana. Waliaomuru nikamatwe na Kingai na Wambura. Wamesema kwasababu ya maandishi yaliyopo mahakamani.
Katuga: Umewataja kama mashahidi wako akina Wambura na Kingai?
Mhe. Lissu: ndio
Katuga: Kumbe ni wema?
Mhe. Lissu: Nimewaita waje waseme ukweli tu. Habari ya wema au sio wema ni mengine. Najua wewe huwezi kuwaleta. Wataletwa na Mahakama.
Watu wanacheka. 😂😂😂😂😂
Katuga: Ulisema wakati unakamatwa?
Mhe. Lissu: Nilikamatwa. Wewe ambae hujawahi kukamatwa huwezi jua nilikamatwa au vipi?
Katuga: umejuaje?
Mhe. Lissu: Wewe unawafungulia watu makesi ya uongo utajuaje mambo ya kukamatwa.
Katuga: Ulisema waliokukamata hawajaja kwasababu wanaogopa kuja kusema ukweli?
Mhe. Lissu: Ndio
Katuga: Dhumuni la Preliminary hearing ni nini?
Mhe. Lissu: kupambanua maswala ambayo yanabishaniwa na ambayo hayabishaniwi.
Katuga: Wewe je ulifanyiwa hoja za awali?
Mhe. Lissu: Ndio nakumbuka.
Katuga: Unajua mambo ambayo hayabishaniwi hayatakiwi kuleta proof?
Mhe. Lissu: Sahihi.
Katuga: Je ukamataji haukuwa na ubishani?
Mhe. Lissu: Suala la nilikamatwa mbinga ndio lilikuwa halina ubishani lakini mengine yana ubishani.
Katuga: Kwakuwa halikubishaniwa. Wakati unawaambia waheshimiwa wakati unawaambia waheshimiwa majaji kuwa hawakuletwa kwasababau maalumu ulikuwa unataka waje kufanya nini?
Mhe. Lissu: Lugano mwenyewe kwenye maelezo yake alisema kuhusu ukamataji ulikuwaje. Kukamatwa Mbinga sio inshu ila ilikiwa halali au la ni jambo lingine tofauti. Huwezi kutofautisha mambo madogo hivi?
Katuga: Unasema ulitoa hotuba kwa watia nia wa Chadema ile Tarehe 03/04 na ukasema ulitoa hotuba hii mbele ya waandishi wa habari?
Mhe. Lissu: Ni kweli kabisa.
Katuga: je katika ushahidi wako wote kama umewaambia kuwa niliongea mbele ya waandishi wa habari kuwamba wasizipeleke kwa umma?
Mhe, Lissu: Sikuwaambia kabisa. Niwaambie ili iweje sasa wakati nilitaka iende kwa umma.
Katuga: Ulitaka iende kwa wananchi?
Mhe. Lissu: Sana tena sana nilitaka iende. Ilikuwa ni habari muhimu sana.
Katuga: Ulitaka hotuba yako isambae kwa wananchi.
Mhe. Lissu: Ni kweli kabisa.
Katuga: Je ulisema ulitoa mipaka kuwa ulitoa mipaka?
Mhe. Lissu: Sikutoa mipaka.
Katuga: Ulisababisha au uliruhusu?
Mhe. Lissu: sikuruhusu mimi
Katuga: P17 alisema walifanya live streaming na kama maneno hayo ya tarehe 03/04 uliwapa prior yaani kabla?
Mhe. Lissu: Sikuwapa kwasababu sikuzungumza nao.
Katuga: Wangejuaje unaenda kuzungumza nini?
Mhe.?Lissu: unataka niseme walikuwa hawajui? Itakusaidia nini sasa? Ndio walikuwa hawajui nitaenda kuongea nini.
Katuga: Kwakuwa hawakuwa wanajua nitakuwa sahihi nikisema haya maneno kuwa tunaenda kukinukisha, tunaenda kuzuia uchaguzi. Walikuwa hawajui kabla?
Mhe. Lissu: Sahihi.
Katuga: Mashahidi wa Jamhuri walikuwa wanasema ulikuwa umevaa Kombati?
Mhe. Lissu: Walisema ndio.
Katuga: Kuna sehemu ulikanusha kuhusu utambuzi wa appearance yako siku hiyo uliyokuwa umevaa?
Mhe. Lissu: Nakanushaje vazi rasmi la Chama. Ni vazi langu.
Katuga: Kwahiyo ulivaa hivyo siku hiyo?
Mhe, Lissu: Sahihi kabisa.
Katuga: Nitakuwa sahihi mashahidi wa Jamhuri walikutambua kwa usahihi kwenye hiyo video kwa nguo hizo?
Mhe. Lissu: Mashahidi wa Jamhuri wananifahamu siku zote.
Katuga: unajua una akili nyingi sasa nijibu tu swali
Mhe. Lissu: Kweli akili ninazo.
Part 287 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 285
Katuga: Usiende huko
Mhe. Lissu: Naenda kote tu, maandamano najua wewe unataka njia ya Mahakama.
Katuga: Sheria ya maandamano umetaja sheria yako?
Mhe. Lissu: Ibara ya 20(1) ya Katiba inasema tupinge kwa mikusanyiko na maandamano.
Jaji Taratibu jamani tafadhali. Naandika.
Mhe. Lissu: Haya mikutano ya hadhara imeruhusiwa kisheria.
Katuga: Haya nikupe usome?
Mhe. Lissu: Nipatie nisome. Anapatiwa Lissu na anasoma. Inaitwa freedom of association and assembly.
Katuga: unamfahamu Francis Dyanabo
Mhe. Lissu: Julius Ishengoma Francis Dyanabo namjua alienda Mahakamani kupinga sheria za uchaguzi
Katuga: Alishinda?
Jaji hebu rudia hapo kwa Dyanabo.
Mhe. Lissu: Namfahamu personally Julius Ishengoma Dyanabo personally kwasababu alifungua kesi za kupinga sheria ya uchaguzi kwamba kabla ya kufungua kesi ya uchaguzi unapaswa kuweka kiasi cha pesa.
Katuga: Kuhusu Mtikila na mgombea binafsi ilikuwaje?
Mhe. Lissu: Sasa usiniingilie nikujibu umekuja vizuri. Mtikila alishinda Mahakama kuu, Mahakama ya rufani ilitengua na baadae akaenda Mahakama ya afrika na wakasema huko kuwa Tanzania iruhusu mgombea binafsi. Hii serikali unayotumikia haijawahi kurekebisha hilo hadi leo.
Katuga: Sasa nakuuliza ulisema kifungu cha 39 cha Penal Code umesema mambo ya overt act kinasemaje kuhusu njia ngapi za manifestation.
Mhe. Lissu: Ziko mbili.
Katuga: Ipi na ipi?
Mhe. Lissu: Publication of a writing or printing na overt act or deed.
Katuga: inapotumika neno or inamaanisha haya maneno yanatumika in alternative?
Mhe. Lissu: yanaweza kufanana na yanaweza yasifanane. In this case yanafanana ni matendo.
Katuga: Kwahiyo similarities inamaanisha.
Kwamba yako similar. Kwahiyo kati ya neno or au and lipi lilipaswa kutumika.
Mhe. Lissu: Kwamba ingesomeka by overt act and overt act. Maana yake nini?
Katuga: Haya soma hapo.
Mhe. Lissu: Sasa hiki umenipa nini? Chukua haya makaratasi yako.
Watu wanacheka. 😂😂😂😂
Katuga: Wewe ni Kaka angu umenitangulia kwenye taaluma si ungesoma eneo lenyewe kama nimekufunulia ukurasa tofauti.
Mhe. Lissu: Sio kazi yangu mimi ungefungua unapotaka wewe.
Katuga: Sasa soma kifungu cha 13 cha Intepretation Act
Mhe. Lissu: Anasoma.
Katuga: Kwahiyo tuamini nini?
Mhe. Lissu: Sheria haitungwi ili iwe absurd
Katuga: Ulisema kuna mambo yamekukuta kwenye mapambano yako? Nitakuwa sahihi nikisema kuwa wewe ni mtu mwenye chuki dhidi ya serikali.
Mhe. Lissu: Nina chuki na serikali ya nchi hii kwasababu imeonea watu wengi.
Katuga: Kwahiyo ulisema yote hayo una chuki na serikali?
Mhe. Lissu: Nina chuki dhidi ya uonevu wa serikali. Ninayo chuki dhidi ya serikali sahihi kabisa. Wanaonea sana watu.
Katuga: Kama Mwanasiasa nia ya Chama cha siasa ni kushika dola?
Mhe. Lissu: Sio nia pekeee ni nia mojawapo.
Katuga: Tutakuwa hatumalizi.
Mhe. Lissu: Tutamaliza tu.
Katuga: mihimili mitatu ya dola ni ipi?
Mhe. Lissu: executive, Bunge na Mahakama.
Katuga: Kwenye sheria majukumu ya hii mihimili mitatu ni nini? Tuanze na Bunge?
Mhe. Lissu: Kutunga Sheria
Katuga: sasa mbona ulitaka kusema mengine
Mhe. Lissu: Sikutaka uishi kwenye ujinga wa kudhani kazi ya Bunge pekee ni kutunga sheria ziko nyingi sana.
Katuga: Kazi ya mahakama je?
Mhe. Lissu: Kutafsiri sheria na kutengua sheria.
Katuga: Jibu maswali yangu usinielimishe?
Mhe. Lissu: Wewe ndio umesema mimi ni kaka yako unataka nikuelimishe hutaki tena muda huu nikuelimishe?
Katuga: Kazi ya Serikali ni ipi?
Mhe. Lissu: Serikali inaisimamia sheria. Kwahiyo?
Katuga: Umenipa jibu?
Mhe Lissu: kwahiyo kama nimekupa jibu hivi nyie mnasoma sheria wapi?
Katuga: Turudi tena Kifungu cha 39 cha Kanuni ya Adhabu. Pale kanuni ya adhabu iliposema mtu akitengeneza kitendo kwa nia ya kutishia serikali. Je tafsiri kuna takwa kuwa lazima iwe imetishika?
Part 286 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 284
Mahakama imereje
Mwenyekiti Lissu alipata wasaa wa kuongea na Mawakili na mashahidi wake kwa muda wa nusu saa aliongea na Katibu Mkuu wa Chama John Mnyika, Amani Golugwa Naibu na Brenda Rupia.
Anasimama Ajuaye Zengeli amesema wako tayari kumuuliza maswali shahidi ambae ni Tundu Lissu. Wako tayari kuendelea.
Majaji wanaaandika andika hapa.
Mhe. Lissu amekaa zake pale kizimbani. Anaulizwa uko tayari kuulizwa tuanze maana bado uko chini ya kiapo pia.
Tutauliza maswali wote na ataanza Nasoro na baadae wengine:
Anasimama Katuga. Anasema Shahidi Pole na ushahidi mrefu.
Katuga: ulisema kuwa sisi ni ndugu zako?
Mhe. Lissu: Nilisema ndio.
Katuga: ni kitu cha kisheria na hakuna tofauti yoyote ya mimi na wewe?
Mhe. Lissu: Sawa.
Katuga: Wewe ni mwanasheria
Mhe. Lissu: Kweli
Katuga: Una ujuzi wa kisheria
Mhe. Lissu: Ni kweli
Katuga: Kama una kumbukumbu Tanzania ilipata uhuru mwaka gani?
Mhe. Lissu: Tar. 09 December 1961
Katuga: Ni nchi huru?
Mhe. Lissu: Ni nchi huru.
Katuga: Ni chombo gani kina mamlaka ya mwisho?
Mhe. Lissu: Mahakama ya Rufani.
Katuga: Naishia Kwenye Mahakama mimi.
Lissu: Hilo ni lako mimi langu ni Mahakama ya Rufani.
Katuga: Basi kwa mujibu wa ibara ya 108 inasemaje?
Lissu: Ndio ni Mahakama ya Tanzania.
Katuga: Kwahiyo Mahakama haipangiwi na mtu yeyote?
Lissu: Haipangiwi
Katuga: Wewe ni Mwenyekiti wa Chadema?
Lissu: Sahihi
Katuga: Je uliiambiwa mahakama hii kuwa mwenyekiti wa Chadema ni kinga kushtakiwa?
Lissu: Sijaiambia na sina kinga hiyo.
Katuga: ulisema sifa nyingi zinazokuhusu ambazo mimi sizipingi. Je hizo tuzo zilikuwa kwenye utaratibu gani?
Lissu: Zipo ambazo zina maandishi na zingine unapewa kitu kama kombe la Dunia hivi.
Katuga: Hebu wambie Majaji haya matuzo yote haya?
Lissu: sijaleta na sina wajibu
Katuga: Ukienda hivyo tutaenda siku saba.
Lissu: nimekaaa jela mwaka mzima nitaogopa week moja yako kweli?
Katuga: Sasa ulileta ushahidi wako huo wa tuzo.
Lissu: Sijaleta sio kazi yangu ni kazi yako wewe.
Katuga: Sasa usilete ujuaji.
Lissu: Mimi ni mjuaji kweli kweli. Unataka nisilete kivipi sasa?
Katuga: Kamati gani ilisema uachiwe?
Lissu: Kamati ya Haki za Binadamu ya kimataifa
Katuga: Kuna sehemu yoyote umekanusha kuwa maneno yale ya kukinukisha, kuhamasisha uasi na sanasana .... umesema maneno hayo wameyatoa kwenye video yako. Je ulisema sio yako?
Lissu: Mimi nilisema mkitaka kuyaelewa sikiliza hotuba yote.
Katuga: Wewe ni kaka yangu siwezi kukuuliza lile swali la una akili au huna kama unavyowaulizaga watu
Lissu: Ukiona unaweza kusema nani amekukataza. Kama unaona sina akili sema tu au niulize nitakujibu.
Katuga: Haya maneno ni ya kwako au sio ya kwako?
Lissu: Hayo maneno sijawahi yakataa ni yakwangu sana.
Katuga: Historia pia umewahi kuisoma?
Lissu: Nimewahi.
Katuga: Waliwahi kuwalaghai babu zetu kihistoria hebu nikumbushe?
Lissu: Hawakulaghai waliingia nao mikataba.
Katuga: mikataba ya kilaghai ilikuwa?
Lissu: hiyo mikataba ilikuwa ya faida kwa hao viongozi wa kiafrika waliyoingia. Kwao waliiona ina faida.
Katuga: Si walikuwa wakoloni hao?
Lissu: Walikuwa wakoloni walioiumiza afrika kama ambavyo Samia ameiumiza nchi sasahivi.
Katuga: Wewe ni mtetezi wa mali za umma. Unakumbuka ulisemaje kuhusu makinikia. Ulisema hayatoki?
Lissu: Huna unachojua kama unataka niulize nitakwambia nilivyosema
Katuga: Si ulisema Tanzania ilishitakiwa je ilishitakiwa kweli mbona mimi sijui kama ilishitakiwa?
Lissu: Nani kakwambia kuwa kwenye international abitration imeshitakiwa unataka nikupeleke nitafanya hivyo hakuna shida.
Katuga: Kama nilikusikia wewe ni mtaalamu wa Sheria za Uchaguzi?
Lissu: Ni kweli
Katuga: Tanzania kupinga sheria fulani utaratibu wake ukoje?
Lissu: Uko namna nyingi? Mfano kupinga kwa njia ya maandamano kuhamaasisha wanachi waipinge hiyo sheria
Part 285 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.