Maisha ya mapambano hasa kwa watu ambao tunatokea familia za kawaida yana hitaji uvumilivu mkubwa sana. Kawaida huwendi popote kuna muda maisha Yanahitaji beki tisa uwanjani.
"Naendelea kuwakumbusha Wazazi,mtoto wa Ki-Afrika mkuze katika misingi ya Ki-Afrika.Usasa usiokuwa na Uadhimu usiteke nafasi maana hauna maana."
Mwl EM Kuliga
✍️🇹🇿
“MUNGU ALIPOWAPA MAELEKEZO YA KUILIMA ARDHI KWA MIAKA SITA, AKAWAAMBIA MWAKA WA SABABU WASILIME ARDHI INATAKIWA KUPUMZIKA;
•MUNGU AKAJA KUWAAMBIA, MNAWEZA MKAJIULIZA JE! HUO MWAKA AMBAO HAMTALIMA CHOCHOTE, MTAKULA NINI? Alafu Mungu huyo huyo akatoa majibu juu ya kile atakachokifanya kwao;-
“Na kama mkisema, Je! Mwaka wa saba tutakula nini? Angalieni hatutapanda mbegu, wala kukusanya maongeo yetu; *ndipo nitawaamria baraka yangu iwe juu yenu mwaka wa sita,* nayo utazaa matunda hesabu ya miaka mitatu.”
Law 25:20-21 SUV
•ANAWAAMBIA ATAIAMURU BARAKA IWE JUU YAO MWAKA WA SITA, MATOKEO YA BARAKA KUWA JUU YAO NI KWAMBA NCHI ITAENDELEA KUZAA KWA MIAKA MITATU!.
•KAZI YAKO NI KUTII KILE ALICHOKUAGUZA BWANA, KAZI YAKO NI KUFANYA; KUNA MAAGIZO MENGINE UKIYATEKELEZA, UTAONEKANA UMEPUNGUKIWA NA AKILI, LAKINI MWISHO WAKE KUNA MATOKEO MAKUBWA SANA!.
BARAKA YA BWANA JUU YAKO!!!.”.
Mwl. Nick
"Sisi ndo wale tuliotabiriwa kimo Cha Zakayo na kupigwa Tama la kushoto, Kope zao zilipofunguka wakatuona Magoliathi tulipowapa la kulia wakashindwa Kupiga."
Mwl EM Kuliga
✍️🇹🇿
"Kuna Siri kubwa Sana katika mioyo wa watoto wetu(kike/kiume),Wawapo nyumbani huishi katika misingi ya kimaadili Lakini ukitaka kuwafahamu wape nafasi ya Uhuru kidogo Tu utagundua ni watulivu machoni tu na si pale wakiwa katika ulimwengu wao."
Tujikaze.
Mwl EM Kuliga
✍️🇹🇿
MSINGI NI FAMILIA.
"Tabia huanza kupikwa katika ngazi ya Kwanza kabisa nyumbani(familia) ikitokea hapo pameyumba basi Kila mmoja atajitafutia utawala wake.Lakini Kumweka MUNGU kuwa wa Kwanza kutaokoa Familia zetu na kupata kizazi kilicho Bora."
Mwl EM Kuliga
✍️🇹🇿