KWANINI MAMA?
"Asunta, amka umuandae mdogo wako Sele asichelewe kwenda shule", nilisikia sauti ya mama yangu alfajiri ikiniamsha nimtayaraishe mdogo wangu ambaye bila kusukumwa hawezi kwenda shule kwani anapenda kitanda kuliko kitu chochote kile duniani. Nilijikongoja taratibu
Serikali imepunguza gharama za kupanga na kupima kiwanja kimoja hadi Sh 130,000 katika maeneo yaliyoendelezwa kupitia urasimishaji.
Gharama hiyo ni punguzo kutoka Sh 250,000–400,000, hatua inayolenga kufanya upimaji na urasimishaji wa ardhi kuwa nafuu zaidi kwa wananchi.
LEO KATIKA KUMBUKUMBU
28 Septemba 2021, Dkt. Samia kukutana na Makamu Benki ya Dunia
Tarehe 28 Septemba 2021, Rais Samia alikutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Hafez Ghanem, Ikulu Chamwino, Dodoma.
Mkutano wa 153 wa IPU unaokwenda kuanza Arusha, Oktoba 5–9, 2026, ni heshima kubwa kwa Tanzania na fursa ya kuunganisha sauti za mabunge kutoka duniani kote. Tanzania hakuna matata atakae na aje.
Mkutano wa 153 wa IPU unaokwenda kuanza Arusha, Oktoba 5–9, 2026, ni heshima kubwa kwa Tanzania na fursa ya kuunganisha sauti za mabunge kutoka duniani kote. Tanzania hakuna matata atakae na aje.
📍Dodoma
Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Dodoma uliopo eneo la Nzuguni umefikia asilimia 14 ya utekelezaji wake.
Ujenzi huu unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri wa Muungano waTanzania kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON 2027.
📍 Nanyumbu–Mtwara
Mradi wa Maji wa Miji 28 kutoka Mto Ruvuma umefikia asilimia 97 ya utekelezaji.
Mradi huo tayari umeanza kutoa huduma kwa wakazi 81,000 wa vijiji vya Masuguru na Mangaka, kwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama.
📍 Lyabukande, Shinyanga
Kikundi cha Mshikemshike Kimandaguli ni miongoni mwa vikundi vinavyonufaika na mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, inayolenga kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.
📍 Tabora
Barabara ya Maili Tano yenye urefu wa km 2.35 imekamilika kwa asilimia 100, ikiwa sehemu ya km 10.7 ya barabara za lami zinazojengwa kupitia Mradi wa TACTIC.
Mradi huu ni kichecheo muhimu cha uchumi, biashara na maendeleo.
TANROADS imefanya tathmini ya km 2,071 za barabara na madaraja 1,032 nchini, hatua iliyosaidia kubaini maeneo 49 yanayohitaji ufuatiliaji maalum ili kukabiliana na athari za mvua za El Nino kwenye miundombinu.
TANROADS imefanya tathmini ya km 2,071 za barabara na madaraja 1,032 nchini, hatua iliyosaidia kubaini maeneo 49 yanayohitaji ufuatiliaji maalum ili kukabiliana na athari za mvua za El Nino kwenye miundombinu.
Je, Wajua?
Ubongo wa binadamu hauhisi maumivu?
Ndiyo, ingawa ubongo ndio unaotafsiri maumivu yote mwilini, wenyewe hauna vipokezi vya maumivu.
Hii ndiyo sababu upasuaji wa ubongo unaweza kufanyika kwa mgonjwa akiwa macho, bila kuhisi maumivu #ElimikaWikiendi