Jana nimemsikiliza SIMBA CHAWENE anavyoiongelea CHUKI ya watanzania kwa Jeshi la polisi ni kama imeletwa na MABEBERU.
ACHA KUJITOA AKILI WE MZEE, haya ni baadhi ya matukio yaliyotokea ndani ya miezi 8 tu, sasa fikiria matukio ya miaka zaidi ya mitano nyuma na yanayoendelea gizani huko kwenye vituo vya polisi.
Leo nimeamka nikujaze akili na najua utapata ujumbe wangu tuu. Nataka ujue kuwa Chuki hii tuliyonayo kwa jeshi la polisi ilipandwa na wao polisi sasa ni muda wa MAVUNO watulie.
Watanzania wamekuwa wakipigwa na kuzuiliwa kuenda mahakamani kinyume kabisa na sheria. Licha ya mahakama kusema mara kadhaa wananchi wasizuiwe Jeshi la polisi liligeuza MAHAKAMA KAMA UWANJA WA VITA DHIDI YA WANANCHI KWA KUKIUKA HATA AMRI YA MAHAKAMA.
Mwezi wa 4 mwaka huu jeshi la polisi lilikusanya watu wote walioenda mahakamani kusikiliza kesi ya Tundu Lissu na kuenda kuwatesa na kuwavunja Miguu na migongo wananchi na kuwatupa kwenye fukwe za bahari na wengine kwenye misitu huko pande.
Murilo alipoulizwa alisema jeshi lake la polisi halihusiki na huku tuliona kabisa wao na magari yao na sare zao wakipiga watu nje ya mahakama na kuondoka nao-majibu ya JEURI kama kawaida yake.
Mkuu wa mkoa HARAMU CHALAMILA alijibu nae kwa jeuri kwa kusema Dar hakuna MAPORI hayo mapori yapo wapi, kwahiyo waliopigwa na kuvunjwa wanaleta Sanaa.
Oktoba 29 jeshi la polisi walikuwa wakifuata vijana majumbani na kuwapiga risasi za vichwa na kupotea nao, miili mingi imepotezwa ndugu wameshindwa kuzika wapendwa wao.
Badhi waliobahatika kuishi waliteswa na kuvunjwa miguuu bila sababu na kupewa kesi za uhaini. Kwa haya machache unataka POLISI AKIFA AU AKIPATA AJALI TUUMIE?
NA UNATAKA TUSHIRIKANE NA HAWA WATU MAGAIDI HIVI WAKINA MAFWELE ,MURILO NA GEORGE AMBAO NDIO WANATOA AMRI YA YOTE HAYA. WATU SIO WAPUMBAVU JIHESHIMU.
TUTAKUWEPO🫵😎
Zipi ni consequences & effects
Kwa vyombo vya dola/Askari binafsi
(Askari Polisi/Wanajeshi/Usalama/Etc)
Pale wanapopewa order/maagizo toka kwa serikali!!(Wakuu wao)
kufanya jambo fulani, then wakakataa kufanya!??
Hasa ikiwa order hiyo inakwenda
kujeruhi/kudhuru/Kuua mtu!!
Je?
-Ni watapoteza tu kazi? Watafukuzwa kazini?
-Watauliwa?
-Watafungwa jela?
-Watahamishwa kituo cha kazi?
Huwa najiuliza sana wanashindwa vipi ku-withdraw hizo order? Na wasipofanya watapoteza nini?
Kuuliwa & kufungwa sidhani sijawahi kusikia!!
Cases nyingi naona ni kuhamishwa kituo cha kazi/Kupunguzwa cheo/Kusimamishwa Kazini/Kutolewa kwenye Payroll!!
Maswali ninayojiuliza, wanapopewa hizo order, kabla ya kutenda wanapima kabisa mzani kuwa…….mfano kapewa order akamuue tu dogo wa miaka 22!
Anawaza🤔🤔Nikikataa hii order naweza hamishwa kituo cha kazi nikapelekwa bush, na kule hakuna michongo….🤔
AAAH BORA NIKAMUUE YULE DOGO TU!! 🔫
So unaua kwasababu tu ukikataa utahamishwa bush?🤔
Au unaua kwasababu ukigoma huna kazi? How?
Wengi wao husema msingi na kiapo cha kazi yao ni kazi ya order……Kazi ya NDIO AFANDE!! Hivyo hakuna neno NO kwa watakachoambiwa kufanya!!
-Wakiambiwa wakaue baba yao mzazi watatii order au watateremsha bunduki na kukubali kupoteza kazi?
-Akiambiwa Akabake dada yake au bint yake atakubali na atachukua wenzake wapande difenda waende kufanya huo ulawiti?
-Akiambiwa akamkamate mama mkwe ataenda kumkamata kwa fujo kama anavyofanya kwa wengine au atamuita kistaarabu?
Hawa watu wasisingizie wanatii order, ukatili mkubwa ni utashi wao binafsi!!
Na ni maselfish, wako tayari kutoa uhai wa mtu ili tu walinde kibarua chao!!
Hata sisi ndugu zetu zaidi ya ELFU KUMI hawakuumwa walifuatwa majumbani kupigwa Risasi Na wengine waliuliwa Barabarani wakidai kesho bora ya watoto zao.
KIFO NI KIFO TUU MSILETE TAHARUKI MITANDAONI.
TUTAKUWEPO🫵😎
Huwezi kuwa msanii wa watawala wakati huo unataka soko la wananchi. Haiwezekani. Hii ni kanuni ya kawaida. Msanii anachagua hadhira yake mwenyewe. Kama watawala na Serikali yao ndiyo soko lako lilipo, wauzie bidhaa zako. Wananchi watawatafuta wasanii wao, watanunua bidhaa zao.