Wanaopandisha watalii Mt. Kilimanjaro wanapinga suala la Serikali kutaka kuweka “cable cars” za kuwapeleka watalii kwenye kilele cha Mlima huo. Wamesema suala hili litapunguza ajira, mapato na litaathiri mazingira. Pia wamesema litawanufaisha wawekezaji binafsi na sio watu wengi
Ikiwa HESLB wanaeza mkopesha mtu alotoka tu Form six with no proffession wala kazi inashindikanaje kufanya hivi,
Semester ya mwisho wa chuo huyu mdaiwa apeleke Detailed business Proposal apewe mkopo wa hata 2M on top of deni lake la awali kama mtaji..?
Ukitaka kumuuzia kitu Mwanamke, muoneshe wanawake wengine wanaokitumia.
Ukitaka kumuuzia kitu Mwanaume, mhakikishie hakuna Mwanaume mwingine mwenye nacho.
Kuna kodi inaitwa “kodi ya urithi”, hii inalipwa na mtu anayerithi mali za aliyefariki, ipo kwenye nchi nyingine huko. Mfano Mtoto wa aliyekuwa mmiliki wa Kampuni ya Samsung huko Korea Kusini amelipa Tsh Trilioni 20 kama kodi ya urithi baada ya kurithi utajiri wa baba yake.
Kwenye jumba la Makumbusho na Historia ya soka la Tanzania, jezi ya Clatous Chota Chama itapambwa kwa madini ya dhahabu na Almasi. Mwamba kutoka Lusaka amedhihirisha kuwa yeye ni mchezaji wa daraja la juu sana. Respect sana kwa Chama.
Baba yake alikuwa na asili ya Palestina tena akawa mtu wa kwanza kujenga msikiti El Salvador, mama yake ni Mkatoliki, mke wake ana asili ya Uyahudi. Yeye anasema anaamini katika Mungu na Yesu. Nayib Bukele Rais wa El Salvador anakubalika sana halafu ana style ya pekee ya mavazi
Pale Dom kuna madon wanahela hazina kazi, wakimpenda manzi hata kama ni first year wanampa gari ya kutembelea na mafuta wanaweka.
Hawawazi kama umetoka nae O level, au wewe ndio ulimpokea siku ya kwanza Chuo wanachukua tu 💔
Kabisa, some one can agree with you, kwamba hata UBONGO unaweza kuwa hauna. Wakati mwingine mimi nakuelewa sana. Sema tu , wale wenzangu tu ndio wana shida na wewe sometimes, tena kama wale wakina Bon Yai na Sugu.
Pale Mafinga kulikuwa kuna don mmoja akiingia bar akakuta mmekaa kinyonge anapaza tu sauti kuwa mhudumu nisingependa kuona mm nakunywa kwa furaha huku wengine wamekaa kinyonge zungusha nne nne kwa kila mtu bar nzima.
Akiagiza mchemsho utasikia anaropoka siwezi kunywa mchemsho peke yangu wakati wenzangu wananitizama zungusha michemsho bar nzima sijazaliwa kuwa mchoyo.
Yule mwamba alikuwa anapendwa sana sijui kama bado yupo nilibahatika offer hiyo siku moja nikiwa Mafinga pale🙌
Unafanya biashara yako fulani ambayo inakupa 300k per month, imekuwa ikikupa hivyo kwa miaka mitatu then ikatokea kampuni ikakupa ajira ya 900k per month ukatakiwa uache hyo kazi yako ya 300k.
Je Utakubali au utakataa..?
Kuna wale madingi siku kama ya Leo kwenye familia limepikwa pilau jingi vyuku nyama choma kama zote ila ye dingi anataoka mishemishe anarudi anaomba kupikiwa ugali mrenda kisa ndo mwenye mji wanakuaga jau kinoma😁
Jana Mtoto wa Rais Museveni yaani Jenerali Muhoozi alisema hajui Iran wanafikiria nini na kama wanadhani wanaweza kulishinda jeshi la Uganda basi hawana akili. Tena akatangaza kuwapa Iran siku 7 waiombe Uganda msamaha. Leo account yake yenye zaidi ya wafuasi 1M haipo mtandaoni.
KIUMBE HUYU NI MZIGO.
Mtu ‘anayejiita mbunge’ anasema Serikali ya CCM imeongeza bei kidogo sana ya mafuta kulinganisha na Kenya. Huyu mtu hajajishughulisha vya kutosha.
Huwezi kulinganisha uchumi wa nchi na nchi kwa kutaja tarakimu tu. Kulinganisha uchumi wa Tanzania na Kenya anatakiwa kutumia vipimo viwili vikuu ambavyo ni;
GDP per Capita (Pato la Taifa kwa kila kichwa) na GDP per Capita PPP (Pato la Taifa kwa kuzingatia Uwezo wa Kununua - Purchasing Power Parity). Zingatia hivyo.
1.GDP Per Capita (Nominal); Hiki ni kipimo cha thamani ya fedha ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa nchini, ikigawanywa kwa idadi ya watu katika nchi.
GDP (pato la Taifa) inatumia viwango vya soko vya kubadilisha fedha (USD). Hii hutumia viwango vya soko vya kubadilisha fedha (market exchange rates).
Tofauti na Tanzania ambayo uchumi wake unategemea zaidi rasilimali za asili (kama madini), Kenya imejenga msingi wake katika sekta ya huduma na ubunifu.
Kenya ni kiongozi wa kidijitali barani Afrika, jambo lililoipa jina la utani la “Silicon Savannah.” Mapinduzi ya huduma za kifedha kwa njia ya simu yalianzia hapa.
Nairobi ni makao makuu ya makampuni makubwa ya teknolojia duniani (Google, Microsoft, na Amazon) yanayofanya shughuli zake katika bara la Afrika.
Benki za Kenya (kama Equity na KCB) zimepanuka na kutawala soko la kanda ya Afrika Mashariki na Kati, zikiwa na matawi nchini DRC, Rwanda, South Sudan
Uchumi wa Tanzania kwa sasa unapitia kipindi cha mpito ambapo matokeo yake katika thamani ya sarafu na soko la kimataifa yanachukua muda sana kuonekana.
Tanzania inasafirisha madini ghafi. Thamani kubwa ya soko inabaki nchi za nje ambako madini hayo yanasafishwa na kutengeneza bidhaa za mwisho.
Thamani halisi inayobaki ni asilimia ya mirahaba na kodi, wakati thamani kubwa ya soko la madini hupimwa masoko ya hisa ya kimataifa (London au Toronto).
Uchumi wa Tanzania una sehemu kubwa sana ya sekta isiyo rasmi inayozalisha fedha nyingi, lakini hazionekani kwenye takwimu rasmi za thamani ya soko la kidunia.
Kwa wastani, raia mmoja wa nchi ya Kenya anaonekana kuzalisha thamani ya fedha karibu mara mbili ya raia mmoja wa Tanzania katika soko la kimataifa.
2.Purchasing Power Parity (PPP); Hiki ni kipimo cha “uwezo wa kununua.” Kinarekebisha tofauti za gharama za maisha na bei za bidhaa kati ya nchi hizi mbili.
Kwa mfano, kama $1 inaweza kununua mikate miwili Tanzania lakini kwa bei hiyo, unaweza kununua mkate mmoja tu nchini Kenya, PPP inazingatia ukweli huo.
Kenya ina kipato kikubwa, gharama za maisha ni kubwa. Tanzania ina gharama ndogo za maisha baadhi ya sekta (vyakula vya asili na baadhi ya huduma za kijamii).
Kenya ina sekta ya huduma (Banking, Tech, Tourism) iliyoendelea zaidi, ambayo huzalisha thamani kubwa ya fedha. Tanzania inategemea zaidi Kilimo na Madini.
Kenya imekuwa kitovu cha kibiashara (Regional Hub) kwa muda mrefu, jambo linalovutia makampuni mengi ya kimataifa kufanya uwekezaji mkubwa Kenya.
Kwa sasa nchini Kenya, bei za mafuta zilizotangazwa na Mamlaka ya Kudhibiti Nishati na Petroli (EPRA) zinazotumika hadi Aprili 2026 kwa Mombasa;
Petroli (Super Petrol) KSh 189.60 kwa lita (Tsh3,771. Dizeli (Diesel) KSh 173.10 kwa lita (Tsh 3,452). Mafuta ya Taa (Kerosene) KSh 163.00 kwa lita (Tsh 3,253).
Hizo habari lita moja ya mafuta ya petroli Kenya inauzwa Tsh 5,450 ametoa wapi? Au amesogezewa kipeperushi na KIHONGOSI kutoka ma’group yao ya WOSAPU?
Mtu ambaye anayejiita ‘mbunge wa CCM’ alitakiwa apitishe ubongo wake maeneo hayo, halafu ajenge hoja zake. Vinginevyo ni MPUMBAVU mwenye ujasiri.