Ujumbe wa JUMUIA YA MADOLA unatakiwa kujadiliwa zaidi kuliko huo UPUMBAVU wenu wa "miaka 30 ya mama".
Jamaa wametoa siku 30 LISSU aachiwe.
Ujumbe ule ni mkubwa sana kuachwa upite hivi hivi.
JIHESHIMUNI.
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 8
Mheshimiwa Hakimu namwambia Tundu Lissu kwa mujibu wa kifungu cha 263(3) cha mwenendo wa makosa ya jinai.
Kinakutaka useme kama una lolote hasa kama unakiri kosa au unakana kosa au utanyamaza au utasema tutakutana nao huko mbele.
Anaanza Lissu kuwa anaomba maelekezo kama kauli hii inaruhusiwa kuwa live streamed
Amri ya mahakama kuu inahusu ushahidi wa kirai wa upande wa mashitaka tu.
Na haihusu ushahidi wa mtuhumiwa hivyo naomba kwa vile maelezo yangu hayahusiani na mashahidi naomba yawe live streamed.
Katuga anasema Mahakama imeshatoa maelekezo kuwa committal haitarushwa live kwahiyo ni Functus Officio kwahiyo haiwezi kuwa live streamed. Tulipofikia hatua hii ni kifungu cha 263 na sio mambo ya kufanya live streaming.
Mahakama imetoa maelekezo kwahiyo tusirudi tena nyuma. Tunashangaa mwenzetu kusema twende live tena.
Hakimu ameinama anaandika kidogo. Naona mambo yameshabadilika. Anasema Hakimu kuwa hata maelekezo yake pia hayataenda live pia.
Lissu amesemaa nilitaka kujua kama amri hii inanihusu na mimi.
Hakimu anasema naomba sasa nitoe maelezo yangu kutokana na kifungu cha 263 kinasema mtuhumiwa aseme lolote kuhusu mashitaka yake.
Lissu anasema na mimi naomba niseme chochote kuhusu mashitaka yangu. Nasema chochote sio ambacho anakitaka jamhuri au mtu yeyote.
Part 9 itaendelea post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 4
Tarehe 09/04 nikapata taarifa akaniambia kuwa Lissu amekamatwa. Tulifika eneo la mkutano pale songea na mkutano ukawa umezuiliwa. Na nilipofika nikakutana na viongozi wa kitaifa na wengine. Walikuja polisi na kuchukua viongozi wote pale uwanjani.
Tarehe 18/04 kutakuwa na matembezi ya hiari ya kuunga mkono msimamo wa No Reforms No election.
Niliambiwa niende stand ya majengo kuchukua Flana yangu na maandamano hayo yangeanzia DS Kitimoto
Baadae tulikamatwa na nikaenda kuandikwa maelezo polisi kuhusu mambo haya
P7 ni shaidi anayefuata ambae ni shahidi wa 11 atakuwa
Mashahidi wa Mchongo hawa. Anasema yeye anatokea arusha.😂
Pale kijiweni kwetu arusha iliibuka mijadala kuhusu video za LISSU na namna ambavyo chadema watakinukisha na mimi niliingia YouTube nikaona hiyo video. Na vijana tukaanza kuhamsishana na wengi wetu tukaonesha kuunga mkono msimamo wa Lissu na tutashiriki kuzuia uchaguzi.
Pale kijiweni kuna watu wengi sana na wao walikuwa wanaunga mkono. Tukiwa hapo walikuja polisi na mimi na P4 tukakamtwa na baadae tukapelekwa polisi na nikasema namna nilivyoounga mkono ile kauli ya Lissu na kuhamsisha wenzangu.
Nilipofika leo Polisi nikaletwa hapa Kwako. Amemaliza ushahidi wake.
P8 shahidi 12 anaanza sasa.
Mimi mkazi wa Njiro, nimezaliwa mengwe. Najishughulisha na biashara ndogondogo katika soko la Manyema na mbuyuni Moshi mjini ni mwanachama wa Chadema.
Napenda misimamo ya Viongozi wangu nikiwa sokoni tar. 04 nilisikia tamko la Mwenyekiti wetu.
Nilianza kufanya hamasa tufanye uasi ili serikali ifanye marekebisho maana niliamini serikali imeharibu uchaguzi ndani ya taifa hili.
Amemaliza ushahidi wake kuwa alikamatwa na kuhojiwa na Polisi.
P9 ni Shahidi anayefuata
Anasema nimesoma shule ya Mwakidete, nimesoma Highland Iringa na nimekuwa nikijishughulisha shughuli ya viazi mbeya.
Nimesoma umeme Mbeya 2010 nikahitimu nikawa fundi umeme. 2009 nikafunga ndoa na 2024 nilivutiwa na sera za Chadema.
Nimehamsishwa kushiriki kongamano la vijana mbeya ambalo lilizuiwa.
Nikiwa nyumbani kwangu niliona video ya Lissu na nikiwa mwanachama wa Chadema nilihamsika na kuwa tayari kufanya vurugu. Tukiwa tunajadili na wenzangu mtaani aliniomba namba yangu ambae huwa tunashirikiana kuzuia uchaguzi.
Alinipigia mtu akitaka fundi wa umeme nilipokutana nae alikuwa ni polisi akasema niko chini ya ulinzi kwa tuhuma za uchochezi na kupanga njama kufanya fujo. Nilidhaminiwa na nikawa naripoti. Leo nimepigiwa simu nilivyokuja ndio unaniuliza haya.
Detective Koplo Michael ni shahidi wa 12 ni shahidi anayefuata sasa ameapa na kusema yafuatayo.
Ni Askari upeleezi kule kilimanjaro maeneo ya Njoro tulimkamata kijana aliyejitambulisha kama P8 aliyekuwa akihamsisha wenzake kufanya vurugu. Tulipata taarifa za Intelligence hivyo tukamkamata.
Kijana huyo alikuwa anasema serikali inafanya mambo ya hovyo hivyo basi tunapaswa kuzuia huu uchaguzi wa kihuni kwenye taifa letu. Tulimpeleka kwa afande RCO. na akahojiwa mtuhumiwa na leo nimeambiwa ahojiwe kama shahidi na tumemuhoji.
Amesema kuwa yeye ni mwanachama wa Chadema na anafanya hamasa za vijana kufanya fujo.
Anafuata shahidi wa 13 nae maelezo yake yatakuwa kama ifuatavyo
Alitoa maelezo Polisi Mwanjelwa. Naishi Block T Mbeya, nimezaliwa Tabora Hospital ya nzega, nimesoma Kakola huko tabora vijijini hadi darasa la saba 2004 na 2008 kidato cha nne.
2011 nikachaguliwa kuingia jeshi la Polisi na nimejifunza mambo mengi ndani ya jeshi la Polisi.
Nalinda raia na mali zake na nina miaka 6 kama askari mpelelezi.
Tarehe 05/04 nikiwa Mwanjelwa Polisi nilipokea maelekezo kutoka kwa mkuu wa kituo kuwa yupo mtuhumiwa anapanga na wenzake taarifa za kuzuia uchaguzi.
Nikajua mtuhumiwa huyo anafanya kazi za umeme na nikampigia kama mteja baadae nikamkamata mtuhumiwa huyo.
Part 5 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Retweet yako.