Hotuba ya Madam Samia imekuwa nzuri kwa sababu imebeba ishara za msaada wa Mwenyezi Mungu juu ya Nchi. Kama Mungu alivyofanya wakati akiwatoa Waisraeli Misri alipouacha moyo wa Farao uwe mgumu ili ajitukuze mbele ya watu wake, vivyo hivyo utukufu wa Mungu umeonekana Tanzania, tunahitaji mambo magumu ili kuthibitisha alama za nyakati na tujue tulikuwa na yeye ktk safari ya haki. Ninaiona kesho iliyo bora, yenye heshima na utukufu wa Mungu, maana dalili zote tayari zimekamilika. Basi tusifikiri mabaya juu ya mtu yeyote bali tuendelee kutafakari haki na wala tusichoke kutenda wema maana tutavuna pasipo kutarajia. Mtamshangaa sana Mwenyezi Mungu. Mimi, ingawa ni mdhaifu na sina uadilifu mbele zake, lakini ninautambua uwezo wake usio na kifani. Leo imekuwa siku ya ishara kubwa. Jipeni Moyo Mkuu. Tutavuka salama. Msizimie Moyo.
Nina taarifa za uhakika kutoka kwa watu waliokamatwa na kubambikiwa kesi za uhaini fake.
Hii imekua njia ya watu wa serikali kujipatia kipato..
Tarime kuna watu wametoa fedha laki tano mpaka milioni 1 kununua uhuru wao.
Lakini kuna watu wana majeraha makubwa Bado wanashikiliwa kwenye vituo vya polisi na mahabusu za magereza..
Hali hiyo iko Shinyanga, Dar, Mbeya, Arusha na Nchi nzima..
Kilichoitwa msamaha limegeuka biashara za watu.
Kwasasa pia kila mtu akikatwa polisi wanamtishia kumpa uhaini na wengine ili kujiokoa wanatoa fedha.
Utawala umefitinika.
"Badala ya kutoa takwimu rasmi, Serikali inatoa kauli za dhihaka zilizoonyesha ukosefu wa heshima kwa familia za waliofiwa. Serikali hadi leo imekataa kuweka wazi idadi ya waliokufa, licha ya ukweli kwamba miili mingi ilikusanywa na vyombo vya dola." Mhe. @amanigolugwa
"Ndugu Mwigulu hakutoa mpango wowote wa Serikali kupambana na kuendelea kwa matukio ya utekaji, upoteaji na mauaji ya wananchi. Badala yake, alitoa kauli pana zisizokuwa na mwelekeo, akijificha nyuma ya maelezo mengi yasiyo na maana kwenye hoja ya msingi" Mhe. @amanigolugwa
"Serikali inataka vyombo vya habari visitoe simulizi zinazoibua ukweli wa yaliyotokea, na hii ni hatari kwa mustakabali wa demokrasia." Mhe. @amanigolugwa
"Ndugu Mwigulu alijaribu kuelekeza lawama nje ya nchi kwa madai yasiyo na ushahidi. Hii ni mbinu ya tawala zinazotengeneza adui wa kufikirika ili kufunika makosa ya ndani." Mhe. @amanigolugwa
"Mandela alisema: 'When a man is denied the right to live the life he believes in, he has no choice but to become an outlaw.' ikimaanisha, 'Wakati mtu anaponyimwa haki ya kuishi maisha anayoyaamini, hana chaguo lingine ila kuwa mkosaji wa sheria'.” Mhe. @amanigolugwa
"Tunataka uwajibikaji wa viongozi waliotoa kauli, ruhusa au maagizo yaliyozalisha mauaji
· Kushindwa kwao kulinda uhai ni kosa la uongozi na la kisheria." Mhe. @amanigolugwa