Huyu mzee amenifanya nimetokwa na machozi!
Sometimes the voice of courage comes from a frail old man who has the heart of a lion!
Huyu mzee anatuhimiza SOTE si @HecheJohn - tupiganie nchi!
Alafu kuna midume yenye vitambi na matako makubwa kuliko sisi wanawake wanawaza kuua na kuteka ndo wanaona ushujaa! Tukishajikomboa hii mianaume tutashughulika nao na watawajibika! Na huyo kijana anayebwia unga na kutoa amri kama vile nchi ya mamaake ndo kabisaaa!
Mzee huyu Mungu amtunze aje kuona Ukombozi wa Pili wa Taifa 🙏🏽
Sisi tupambane jamani hakuna kurudi nyuma - tumeshashinda sema mafedhuli wamekaza fuvu
#TutaelewanaTu
Baada ya kuwasili jijini Luanda, Angola kwa ziara ya kikazi, nimekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wangu, Rais wa Jamhuri ya Angola, Mheshimiwa João Manuel Gonçalves Lourenço.
Katika mazungumzo yetu, tumesisitiza umuhimu wa kuendeleza uhusiano wa kihistoria na ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Angola. Wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika mataifa yetu yalishirikiana kufanikisha uhuru wa kisiasa; sasa ni wajibu wetu kuimarisha ushirikiano huo katika nyanja za uchumi, biashara, uwekezaji na maendeleo ya kijamii kwa manufaa ya wananchi wetu, tukitekeleza maono ya waasisi wa mataifa yetu.
Ninaipongeza Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars), kwa kuanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 nchini Morocco kwa ushindi dhidi ya Timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini, (Banyana Banyana).
Ninaungana na Watanzania wote kuitakia kila la kheri Twiga Stars inapoendelea kupeperusha bendera ya Taifa letu katika michezo inayofuata. Endeleeni kupambana kwa moyo huo huo, mkionesha uzalendo, nidhamu na ari ya ushindani inayolitangaza vyema Taifa letu.
Mpaka sasa tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 218, hatua kubwa inayotupeleka karibu zaidi na lengo la TSh. Milioni 334.
CHANGIA SASA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
ASANTENI WATANZANIA!
TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 130.2
Asanteni kwa mwitikio wenu mkubwa. Mpaka sasa, tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 130.2 katika Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334 kwa ajili ya kufanikisha Baraza Kuu la Umma.
Safari inaendelea.
TUENDELEE KUCHANGIA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Leo ni siku muhimu na ya kihistoria kwa nchi yetu ambapo tumehitimisha safari tuliyoianza miaka miwili iliyopita kwa kuzindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ikiwa ni mara ya pili kwa Taifa letu kufanya hivi tangu Uhuru. Dira hii ni maoni ya wananchi wote ambapo kwa miaka 25 ijayo wamedhamiria kujenga Taifa jumuishi, lenye ustawi, haki na linalojitegemea.
Tumefikiri wenyewe, tumepanga wenyewe, tumeandika wenyewe na hatua inayofuata ni utekelezaji. Hatua hii inahitaji kila mwananchi kufanya kazi kwa ari, nguvu, maarifa na bidii na kuwepo ushirikiano wa dhati kati ya serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo. Aidha, hatuna budi kuendelea kudumisha amani, umoja, mshikamano na utulivu nchini ili tufikie shabaha na malengo tuliyojiwekea.
Ninawapongeza wote, hasa wananchi, walioshiriki katika maandalizi ya dira hii, na hivyo kuipa umiliki na taswira ya kitaifa. Mmetimiza wajibu wenu, nami ninawahakikishia kuwa, tumeweza kutekeleza mengi, tutaweza kutekeleza dira hii.
Hii ndio ilikuwa maana halisi ya No Reforms No Election ya Chadema kabla ya Uchagizi wa January 21, 2025. Tulikuwa na mkakati mzuri sana unaotekelezeka, tuliamini wagombea wetu sasa hawatakatwa, mawakala hawatazuiwa vituoni, na washindi watatangazwa. Bahati mbaya uongozi mpya ulipokwenda retreat ya Bagamoyo ukaja na mkakati mpya wa utekelezaji wa No Reform No Election ambapo tuliambiwa tutaitekeleza tukiwa nje ya uchaguzi kwakuzuia uchaguzi, japo leo imebadilika tena tunawasusi ccm uchaguzi wapite bila kupingwa!
Ni faraja kubwa kuona Boti ya Utafutaji na Uokoaji imeshushwa kwenye maji ili kuanza kazi katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM (2020-2025) unaolenga kuimarisha usalama wa watumiaji wa ziwa hilo ambalo ni muhimu kwa uchumi na maisha ya wananchi.
Takribani wananchi milioni 6 wanajishughulisha na uvuvi na wanahitaji nyenzo hizi muhimu kwa usalama wao. Mpango wa serikali ni kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya uokozi na huduma za dharura majini, ili kuhakikisha kila mwananchi anakuwa salama anapokuwa kazini au safarini.